Watoto wa rafiki wa mke wangu ni wangu, nawahitaji

inaelekea unajichanganya kwa sababu umesema kuwa mwenye tatizo amekuomba na ametia saini yake, pia ukasema mwenye mke hajui kuwa wale watoto si wake na anahitaji mtoto wa tatu na pia amethibitika hawezi kuzaa.Sasa kipi ni kipi ktk maelezo yako.

Udhibitisho anao mke wake ambaye hana tatizo hilo.
 
Ndugu, kweli mwenzenu ni na shida na sijui zitaishaje. Juzi tu nilikuwa na tatizo la mke wangu na bado halijakwisha. Likaja hili la GF wangu wa zamani. Lakini, ninao watoto wawili nje ya ndoa kutoka kwa rafiki wa mke wangu. Mmoja ni mtoto wa kike (7 yrs) na mwingine wa kiume (4yrs). Rafiki wa mke wangu ambaye bado ana urafiki na mke wangu, alinililia sana baada ya kukaa miaka 2 bila kupata watoto kwamba wasingeweza kupata mtoto. Baada ya kudhibitika kwamba yeye hakuwa na tatizo la kupata watoto na mme wake ndo mwenye matatizo, aliniomba nizae nae watoto. Mimi niliyaweka kwenye maandishi na yeye akakubali kutia sahihi. Watoto hawa ni wazuri na wana afya njema, jamaa hajui lolote na anawapenda sana watoto hawa. Lakini ili niweze kuwalea watoto wangu vizuri, nimeona sasa wakati umefika niwachukue watoto wangu kwa vile tayali ninaushahidi wa kutosha kwamba ni wangu vikiwepo na vipimo vya vinasaba.

Lakini wasiwasi wangu ni kwamba yule ni mke halali wa mtu! Kisheria, japo sio kosa la jinai kuzaa na mke wa mtu, ni kosa la kawaida ambapo naweza kulipa fidia kubwa sana na pengine kutenganisha hata ndoa yao. Mke anataka nimpatie mtoto wa tatu kutokana na mme wake kuhitaji mtoto wa tatu. Sasa nifanyeje jamani? Nisaidie jamani nifanyeje? Mi nataka watoto wangu na sitaki tena kumpatia mtoto mwingine.

Kabla sijakupa ushauri, labda nikuulize kwanza una watoto wangapi kwa huyo mke wako wa ndoa ??
 
Sasa watoto ndo nipotezee? Hii si damu yangu kabisa?
Sikio la kufa Wiliyeye, kazana mwisho wake utaujua, ila nakukanya tena , na tena kuwa ACHA KABISA KUJARIBU KUJUA UBAYA WA MTU UKO WAPI, UTACHINJWA WEWE , HUYO MWANAMKE NA HAO WATOTO WOTE SASA UTAKUWA UMEAMBUA NN? KAMA MAISHA YAMEKUCHOSHA KUTOKANA NA NDOA YAKO KUWA MBAYA KILA KUKICHA MM NAKUSHAURI KUNYWA SUMU UFE TARATIBUUUUUUUUU BILA KWENDA NA MTU.
 
Sasa watoto ndo nipotezee? Hii si damu yangu kabisa?

Ndio ni damu yako lakini hukufuata utaratibu katika kuwapata waache walelewe na wazazi wao kama wajuavyo wao. Ukitaka kuleta zako za kudai damu yako utalikoroga kuliko ulivyolikoroga sasa. Amani yako iwe katika kujua kwamba watoto wanalelewa vizuri na mama na baba yao. Wapende hivyo hivyo kimbali mbali.
 
Sikio la kufa Wiliyeye, kazana mwisho wake utaujua, ila nakukanya tena , na tena kuwa ACHA KABISA KUJARIBU KUJUA UBAYA WA MTU UKO WAPI, UTACHINJWA WEWE , HUYO MWANAMKE NA HAO WATOTO WOTE SASA UTAKUWA UMEAMBUA NN? KAMA MAISHA YAMEKUCHOSHA KUTOKANA NA NDOA YAKO KUWA MBAYA KILA KUKICHA MM NAKUSHAURI KUNYWA SUMU UFE TARATIBUUUUUUUUU BILA KWENDA NA MTU.

Lisa acha vitisho, yawezekana jamaa akijua kwamba hana nguvu na amepata watoto hao akanishukuru sana kwa kumuondolea aibu katika jamii. Mi nataka identity ya watoto wangu itambulike tu ili kama akiamua kuishi nao basi iwe kwake.
 
Kweli kabisa!
 
Mi nina watoto wa kike wote kwa mke wangu wa ndoa, wako wawili

Nashkuru kwa jibu lako!

Ushauri:
1. Kwa vile unao watoto japo ni wa kike, Mungu anaweza kukupa mwengine wa kiume, achana kabisa na huyo rafiki wa
mkeo, katisha mahusiano ya kimapenzi na wala usikubali kuzaa nae tena, mwambie ajaribu bahati yake kwa mwengine!

2. Kama hao watoto aliozaa na huyo mwanaume, amewazaa ndani ya ndoa, basi huna haki yeyote ya kimila au kisheria
juu yao, ni sawa na mtu aliedondosha mbegu kwenye shamba la mtu, mbegu hiyo ikamea vizuri na kutoa matunda bora.
Hiyo itakuwa ni faida ya mwenye shamba!

Hitimisho:
Kumbuka/elewa kwamba sio wote wenye watoto ndani ya ndoa, ni watoto wao wa damu, bali busara au ukorofi wa wakezao !!
 
Lisa acha vitisho, yawezekana jamaa akijua kwamba hana nguvu na amepata watoto hao akanishukuru sana kwa kumuondolea aibu katika jamii. Mi nataka identity ya watoto wangu itambulike tu ili kama akiamua kuishi nao basi iwe kwake.

Wewe kweli sikio la kufa! Khaaaaaaaaaaaaaaaaaaa!
 
Sikio la kufa Wiliyeye, kazana mwisho wake utaujua, ila nakukanya tena , na tena kuwa ACHA KABISA KUJARIBU KUJUA UBAYA WA MTU UKO WAPI, UTACHINJWA WEWE , HUYO MWANAMKE NA HAO WATOTO WOTE SASA UTAKUWA UMEAMBUA NN? KAMA MAISHA YAMEKUCHOSHA KUTOKANA NA NDOA YAKO KUWA MBAYA KILA KUKICHA MM NAKUSHAURI KUNYWA SUMU UFE TARATIBUUUUUUUUU BILA KWENDA NA MTU.

Hapo kwamba ninywe sumu ndo umekoroga kabisa
 
Nashkuru kwa jibu lako!

Ushauri:
1. Kwa vile unao watoto japo ni wa kike, Mungu anaweza kukupa mwengine wa kiume, achana kabisa na huyo rafiki wa
mkeo, katisha mahusiano ya kimapenzi na wala usikubali kuzaa nae tena, mwambie ajaribu bahati yake kwa mwengine!

2. Kama hao watoto aliozaa na huyo mwanaume, amewazaa ndani ya ndoa, basi huna haki yeyote ya kimila au kisheria
juu yao, ni sawa na mtu aliedondosha mbegu kwenye shamba la mtu, mbegu hiyo ikamea vizuri na kutoa matunda bora.
Hiyo itakuwa ni faida ya mwenye shamba!

Hitimisho:
Kumbuka/elewa kwamba sio wote wenye watoto ndani ya ndoa, ni watoto wao wa damu, bali busara au ukorofi wa wakezao !!

Sasa inamaana haya makubaliano pamoja na ushahidi wa vinasaba hautanisaidia? Sawa naweza kumezea ila nisaidie kwa swali hili la ushahidi nilionao
 
Hapo kwamba ninywe sumu ndo umekoroga kabisa
Mm nimekupa njia nzuri na ya rahisi ya kuondoka katika ulimwengu huu ambao umekupa mgongo kwenye maisha yako ya NDOA, sasa unatapatapa ili uondoke na mtu, la hasha mm naokuomba WIliyeye acha hao watoto wa watu wakae kwa amani na utulivu walionao,
pili usije ukawakatishia maisha yao na mama yao , maana wanaweza hukumiwa bila hatia yoyote.
tatu, sijawahi kusikia mtu anachekelea mkewe kumletea watoto wa nje ya ndoa. sana sana atakutafuta wewe uliyelima kwenye shamba lake akufyeke mbali.

KILA LA KHERI KATIKA KUWAPATA HAO WATOTO. ILA WILIYEYE KIFO CHAKO KIKO KARIBU SANAAAAAAAAA!
 
We askari nini? Unataka niyavulumushe megine tena?

si unataka kuweka heshima vzr au? sasa unategemea uwachukue kwa njia gani bila mkeo au mume wa huyo mwanamke kujua mi sijakuelewa unless uwaibe na uwatoroshe mbali.
 
Lakini si ushahidi ninao? Siendi kwenye nyumba nafikiri kwenda mahakamani

Acha mbwembwe zako, nani alikuwa shuhuda wa tatu wakati mnakubaliana huo mkataba wenu wa Mangunga. Ebu weka hapa hiyo nakala ya mkataba, hatutaki hypothetical ideas hapa. Mkataba hu0 ungekuwa valid kama wewe, mke, mme halali wa mke na shahidi mwingine wangetia sahili makubaliano hayo yasiyo na kichwa wala miguu.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom