Watoto wa rafiki wa mke wangu ni wangu, nawahitaji

Wiyelelee

JF-Expert Member
Joined
Nov 9, 2012
Messages
1,072
Points
1,170

Wiyelelee

JF-Expert Member
Joined Nov 9, 2012
1,072 1,170
Ndugu, kweli mwenzenu ni na shida na sijui zitaishaje. Juzi tu nilikuwa na tatizo la mke wangu na bado halijakwisha. Likaja hili la GF wangu wa zamani. Lakini, ninao watoto wawili nje ya ndoa kutoka kwa rafiki wa mke wangu. Mmoja ni mtoto wa kike (7 yrs) na mwingine wa kiume (4yrs). Rafiki wa mke wangu ambaye bado ana urafiki na mke wangu, alinililia sana baada ya kukaa miaka 2 bila kupata watoto kwamba wasingeweza kupata mtoto. Baada ya kudhibitika kwamba yeye hakuwa na tatizo la kupata watoto na mme wake ndo mwenye matatizo, aliniomba nizae nae watoto. Mimi niliyaweka kwenye maandishi na yeye akakubali kutia sahihi. Watoto hawa ni wazuri na wana afya njema, jamaa hajui lolote na anawapenda sana watoto hawa. Lakini ili niweze kuwalea watoto wangu vizuri, nimeona sasa wakati umefika niwachukue watoto wangu kwa vile tayali ninaushahidi wa kutosha kwamba ni wangu vikiwepo na vipimo vya vinasaba.

Lakini wasiwasi wangu ni kwamba yule ni mke halali wa mtu! Kisheria, japo sio kosa la jinai kuzaa na mke wa mtu, ni kosa la kawaida ambapo naweza kulipa fidia kubwa sana na pengine kutenganisha hata ndoa yao. Mke anataka nimpatie mtoto wa tatu kutokana na mme wake kuhitaji mtoto wa tatu. Sasa nifanyeje jamani? Nisaidie jamani nifanyeje? Mi nataka watoto wangu na sitaki tena kumpatia mtoto mwingine.
 
Joseph

JF-Expert Member
Joined
Aug 3, 2007
Messages
3,524
Points
1,225

Joseph

JF-Expert Member
Joined Aug 3, 2007
3,524 1,225
Mpatie mtoto wa tatu uendeleze dhambi kubwa ambayo uliiianza tangu mwanzo,jichunguze mwenyewe pia maana inawezekana hata watoto ulionao inawezekana si wako ni wa mwanaume mwingine.
Endelea kucheza na mke wa mtu ila siku moja utakuja jutia maamuzi yako ya kutaka watoto.
 
Wiyelelee

JF-Expert Member
Joined
Nov 9, 2012
Messages
1,072
Points
1,170

Wiyelelee

JF-Expert Member
Joined Nov 9, 2012
1,072 1,170
Mpatie mtoto wa tatu uendeleze dhambi kubwa ambayo uliiianza tangu mwanzo,jichunguze mwenyewe pia maana inawezekana hata watoto ulionao inawezekana si wako ni wa mwanaume mwingine.
Endelea kucheza na mke wa mtu ila siku moja utakuja jutia maamuzi yako ya kutaka watoto.
Dhambi iko wapi wakati nimewaletea heshima?
 
Lisa

JF-Expert Member
Joined
Aug 13, 2009
Messages
1,561
Points
1,195

Lisa

JF-Expert Member
Joined Aug 13, 2009
1,561 1,195
Wiliyeye una makubwa sana , kila siku unakuja na jipya Khaa! unanishangaza sana, halafu unalalamika kuwa mkeo hakuheshimu, hakupokei mzigo , hakujali kwa hayo tena sijui itakuwaje, Duh! Mimi naona mwisho wa maisha yako umekaribia sana , sasa ukitaka kuthibitisha hilo nenda kwenye hiyo nyumba kadai watoto wale ni wako. Unajua kwa nn Ng'ombe hana meno ya juu!!!
 
NATA

JF-Expert Member
Joined
May 10, 2007
Messages
4,512
Points
1,195

NATA

JF-Expert Member
Joined May 10, 2007
4,512 1,195
Makubaliano yalikuwa uwachukue utakapo amua?
Acha ubinafsi
Elewa kwamba unenda kugusa hisia za watu na unaweza ukasababisha madhara makubwa hata ikiwezekana watu kuchinjana.

Kwani watoto wanaishi kwa shida kule?

Na angalia hata ndoa yako yaweza dhurika vilevile au mkeo anahabari?

Acha choyo na ufedhuri!
 
andishile

JF-Expert Member
Joined
Apr 1, 2012
Messages
1,430
Points
1,225

andishile

JF-Expert Member
Joined Apr 1, 2012
1,430 1,225
wanaume jamani!hawa ndo waume tulionao majumbani!kwa mtindo huu tutapona kweli??? na cha ajabu huyo rafiki wa mkeo anataka mtoto mwingine ina maana bado una uhusiano nae,je huyo mwanamke amefanya hivyo kwa waume wangapi wa marafiki zake?na wewe unasema una kimeo kingine na mkeo,ina maana demu mwingine! LILE TANGAZO LA TUKO WANGAPI?TULIZANA! LIANGALIE UNAWEZA UKABADILIKA MAISHA YAKO,NAKUSHAURI MRUDIE MUNGU WAKO,UACHE UYAFANYAYO!
 
Blaine

JF-Expert Member
Joined
Jan 11, 2012
Messages
2,280
Points
0

Blaine

JF-Expert Member
Joined Jan 11, 2012
2,280 0
kwenye mkataba mlikubaliana ungewachukua watoto baada ya muda au umeamua 'kubadili mawazo'? huyo mume hakushtuka kuona mkewe ana mimba wakati yeye ana matatizo au analeta stori za abraham na sarah? anyway goodluck ku-deal na mumewe
 
Lukolo

JF-Expert Member
Joined
Dec 2, 2009
Messages
5,148
Points
1,250

Lukolo

JF-Expert Member
Joined Dec 2, 2009
5,148 1,250
Makubaliano yalikuwa uwachukue utakapo amua?
Acha ubinafsi
Elewa kwamba unenda kugusa hisia za watu na unaweza ukasababisha madhara makubwa hata ikiwezekana watu kuchinjana.

Kwani watoto wanaishi kwa shida kule?

Na angalia hata ndoa yako yaweza dhurika vilevile au mkeo anahabari?

Acha choyo na ufedhuri!
Si watu kuchinjana tu bali watoto wenyewe kuchomwa moto wakiwa hai. Hivi unajua hasira ya huyo mwanaume itakavyokuwa baada ya kutambua kwamba sasa anakwenda kuishi bila watoto na aibu ya kwamba alikuwa analea watoto wa mwenzie? Ataona ni heri kufia jela kuliko kubaki na aibu hiyo. Atawachinja hao watoto kama kuku. Kama una akili nzuri waache watoto wakue hadi wawe watu wazima ndipo muangalie namna ya kuwaeleza ili wachague wenyewe wanataka kuwa akina nani. Lakini kwenda kudai watoto wa miaka saba na minne ni kama unataka uwakose kabisa hao watoto. Labda hilo la kuongeza mtoto mwingine mimi nafikiri ni bora ukubaliane na huyo mwanamke kwamba wanatosha hao waliopo. Kuwa na watoto watatu kwenye nyumba ya mwenzio mimi sishauri kabisa.
 
LIMANYE

Member
Joined
Nov 16, 2012
Messages
24
Points
0

LIMANYE

Member
Joined Nov 16, 2012
24 0
Kiukweli hamkumtendea haki kabisa Mume wa rafiki ya mke wako na hamjatatua tatizo kwani labda hata jamaa hajui kama ana matatizo ya kutozalisha dhambi hiyo inaweza kuleta madhara makubwa hata kwa watoto kwani wamezaliwa na kukua katika mapenzi ya baba wamfikiriae ni wao kumbe ukweli anao mama yao na wewe baba mpanda mimba naomba uwaache hao watoto waendelee kukua katika mikono wanayo itambua kwa sasa acha wawe watu wazima unaoweza kuwaeleza wakahimili mazito hayo na usiendelee kumzalisha mke wa mwenzio mshauri aende hosp na mumewe Mungu ni waajabu anaweza kufanikiwa kumzalisha mke wake angarau akampatia mtoto halali wa tatu.
 
Wiyelelee

JF-Expert Member
Joined
Nov 9, 2012
Messages
1,072
Points
1,170

Wiyelelee

JF-Expert Member
Joined Nov 9, 2012
1,072 1,170
Wiliyeye una makubwa sana , kila siku unakuja na jipya Khaa! unanishangaza sana, halafu unalalamika kuwa mkeo hakuheshimu, hakupokei mzigo , hakujali kwa hayo tena sijui itakuwaje, Duh! Mimi naona mwisho wa maisha yako umekaribia sana , sasa ukitaka kuthibitisha hilo nenda kwenye hiyo nyumba kadai watoto wale ni wako. Unajua kwa nn Ng'ombe hana meno ya juu!!!
Lakini si ushahidi ninao? Siendi kwenye nyumba nafikiri kwenda mahakamani
 
Wiyelelee

JF-Expert Member
Joined
Nov 9, 2012
Messages
1,072
Points
1,170

Wiyelelee

JF-Expert Member
Joined Nov 9, 2012
1,072 1,170
Makubaliano yalikuwa uwachukue utakapo amua?
Acha ubinafsi
Elewa kwamba unenda kugusa hisia za watu na unaweza ukasababisha madhara makubwa hata ikiwezekana watu kuchinjana.

Kwani watoto wanaishi kwa shida kule?

Na angalia hata ndoa yako yaweza dhurika vilevile au mkeo anahabari?

Acha choyo na ufedhuri!
Sawa, watoto hawana shida kule, lakini wanatumia jina la ukoo wa jamaa! Nataka watumia jina laungu na hili linawezekana wakija kwenye himaya yangu tu.
 
NATA

JF-Expert Member
Joined
May 10, 2007
Messages
4,512
Points
1,195

NATA

JF-Expert Member
Joined May 10, 2007
4,512 1,195
Sawa, watoto hawana shida kule, lakini wanatumia jina la ukoo wa jamaa! Nataka watumia jina laungu na hili linawezekana wakija kwenye himaya yangu tu.
Umepima madhara yake?
Naona huwapendi hao watoto na wewe pia hujipendi !
 
Wiyelelee

JF-Expert Member
Joined
Nov 9, 2012
Messages
1,072
Points
1,170

Wiyelelee

JF-Expert Member
Joined Nov 9, 2012
1,072 1,170
wanaume jamani!hawa ndo waume tulionao majumbani!kwa mtindo huu tutapona kweli??? na cha ajabu huyo rafiki wa mkeo anataka mtoto mwingine ina maana bado una uhusiano nae,je huyo mwanamke amefanya hivyo kwa waume wangapi wa marafiki zake?na wewe unasema una kimeo kingine na mkeo,ina maana demu mwingine! LILE TANGAZO LA TUKO WANGAPI?TULIZANA! LIANGALIE UNAWEZA UKABADILIKA MAISHA YAKO,NAKUSHAURI MRUDIE MUNGU WAKO,UACHE UYAFANYAYO!
Huyu mwanamke anajiheshimu sana na mwenye busara! Sina urafiki nae wa kimapenzi isipokuwa ikifika wakati wa kuhitaji mtoto tu! Kwa hili namtetea? Thuko wangapi? Mi na mke wangu nae na mme wake tu!
 
BHULULU

JF-Expert Member
Joined
Jun 28, 2012
Messages
4,904
Points
1,250

BHULULU

JF-Expert Member
Joined Jun 28, 2012
4,904 1,250
Sawa, watoto hawana shida kule, lakini wanatumia jina la ukoo wa jamaa! Nataka watumia jina laungu na hili linawezekana wakija kwenye himaya yangu tu.
Mkuu naona umeishaamua,fanya unachofikiria ila bahati mbaya hutakuja hapa tena kutoa ushuhuda maana UTAKUFA samahani lakini.
 
Wiyelelee

JF-Expert Member
Joined
Nov 9, 2012
Messages
1,072
Points
1,170

Wiyelelee

JF-Expert Member
Joined Nov 9, 2012
1,072 1,170
kwenye mkataba mlikubaliana ungewachukua watoto baada ya muda au umeamua 'kubadili mawazo'? huyo mume hakushtuka kuona mkewe ana mimba wakati yeye ana matatizo au analeta stori za abraham na sarah? anyway goodluck ku-deal na mumewe
Inaelekea jamaa hajui kwamba ana tatizo lakini vinasaba hata document nikizianika hapa zinaonesha watoto ni wangu. Suala la kuwachukua watoto limo kwenye makubaliano kwamba "iwapo utawahitaji, tutafanya mazungumzo ambayo yatahusisha pande zote, ikiwepo na kutumia ushahidi na vielelezo kwamba watoto watakaopatikana ni wale ambao wametokana na mahusiano kati yetu"
 
Forum statistics

Threads 1,344,500
Members 515,750
Posts 32,823,542
Top