Watoto wa Nyerere wanadai viwanja Kinyemela!! Kila Mtu anawaogopa!! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Watoto wa Nyerere wanadai viwanja Kinyemela!! Kila Mtu anawaogopa!!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Kamundu, Dec 23, 2010.

 1. K

  Kamundu JF-Expert Member

  #1
  Dec 23, 2010
  Joined: Nov 22, 2006
  Messages: 2,109
  Likes Received: 455
  Trophy Points: 180
  Nimesikitishwa na vitendo vya watoto wa Nyerere kutumia jina la baba yako na kudai viwanja vingi msasani ambavyo si vyao. Kuna watu wengi wana viwanja karibu na nyerere na wameshutushwa kwa kuambiwa baada ya miaka mingi kwamba watoto wa Nyerere wanadai ni mali ya baba yao. Raisi kwasababu ya uwoga wa siasa ame revoke hati za kihalali za viwanja vyote pembeni mwa nyerere kwani watoto wanadai ni vya kwao na kesi ziko mahakamani!. Kwa kuwa hawa watoto hawafanyi vizuri kibiashara na kimaisha wameona kitu pekee wanachoweza kufanya ni kudai viwanja kwani viwanja vimepanda thamani sana hivyo hawakudai wakati baba yao yupo sasa miaka mingi imepita na mama yako haelewi haya maovu basi wameona ni wakati wa kutumia jina na baba yao ambaye alipewa nyumba na watanzania kwa manufaa binafsi. Hali hii imemfanya raisi ku revoke viwanja na itabidi serikali ilipe fidia kwa viwanja ambao havikuwa vya nyerere. Raisi ame revoke vibali hivyo kwani kihalali hawawezi kushinda. Siamini kama nyere angekuwepo leo angeachia watoto wake waanze kupagania viwanja ambavyo siyo vyao.
   
 2. Geza Ulole

  Geza Ulole JF-Expert Member

  #2
  Dec 23, 2010
  Joined: Oct 31, 2009
  Messages: 11,068
  Likes Received: 4,000
  Trophy Points: 280
  kama vipi hivyo? maana usiandike upupu ilhali hutoi vielelezo taja na namba za viwanja basi...
   
 3. Kiranga

  Kiranga JF-Expert Member

  #3
  Dec 23, 2010
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 34,607
  Likes Received: 6,185
  Trophy Points: 280
  Where Ganesh@ when you really need him ?
   
 4. U

  Uwezo Tunao JF-Expert Member

  #4
  Dec 23, 2010
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 6,947
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Nashukuru kwamba ni kiwanja tu na wachukue, Kuzuia mafisadi wanaobaka nchi kila kukicha ndio unaona nini?? Tofauti na hapo, ulishawahi kuwasiki hawa watoto wa Mwalimu Nyerere wakilalamikiwa kumnyang'anya mtu kitu???
   
 5. m

  mtemiwao JF-Expert Member

  #5
  Dec 23, 2010
  Joined: Sep 5, 2010
  Messages: 384
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Wapeni bwana kama ni viwanja tu,sasa hv watoto wa vigogo wanafilisi nchi, ije viwanja?wapeni wapeni jamani acheni upupu
   
 6. Mwanajamii

  Mwanajamii JF-Expert Member

  #6
  Dec 23, 2010
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 7,080
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  wewe ni miongoni na unaweza kuwa mmoja wa wale waliokwenda kuiba viwanja vya nyerere na kisha unasema Nyerere alipewa nyumba na watanzania kwa manufaa binafsi au ulitaka nyerere achukue nyumba zote alizotaifisha kwa manufaa binafsi? Eneo lililobaki bila kujengwa pale msasani kwa mwalimu ni lile lilipo mbele ya nyumba yake kwani maeneo yote yamejengwa nyumba kuzunguka nyumba yake. Eneo hilo ni kweli la mwalimu na kama angekuwa na utajiri mkubwa kabla hajafa angekuwa amejenga nyumba hapo.

  Nyumba ya msasani nyerere alikopa fedha kwa iliyokuwa benki ya nyumba Tanzania (THB) na nyumba ya butiama mkoani Mara ilijengwa na JKT lakini baada ya yeye mwenyewe kukataa sana na baada ya kumshawishi akakubali.

  Mwalimu wakati anastaafu alipata zawadi nyingi sana nchi nzima zikiwemo ng'ombe lakini aliziacha kutumika katika mikoa husika kwa manufaa ya jamii nzima na kama angekusanya zawadi hizo ingekuwa ni utajiri tosha kwa familia yake.

  mwache mzee wa watu apumzike mahali pema peponi, familia ya mwalimu sio moja ya familia tajiri nchi hii kutokana na msimamo wa mwalimu kujali taifa zaidi kuliko familia yake. Suala hili ndilo limeendelea kumtofautisha mwalimu na viongozi wengi wa Afrika enzi zake za kudai uhuru na kukaa Ikulu kwa miaka 23 bila kuwa tajiri.

  wewe uliona wapi Rais na mkewe kwenda kumalizia maisha yao ya ustaafu kijijini tena katika mazingira magumu ya kukosa nyumba bora hadi pale walipopewa msaada wa kujengewa nyumba bora na Jeshi? hadi sasa mama maria nyerere yuko kijiji butiama anakuja mjini tu wakati kuna hitaji la muhimu au mwaliko wa shughuli za kitaifa. Kumbuka butiama haina maji ya bomba kama ilivyo pale msasani lakini kachagua kuishi huko.
   
 7. Ng'wanangwa

  Ng'wanangwa JF-Expert Member

  #7
  Dec 23, 2010
  Joined: Aug 28, 2010
  Messages: 10,179
  Likes Received: 895
  Trophy Points: 280
  acha kuchokonoa watoto wa Baba wa Taifa wewe.

  utalaaaniwa.
   
 8. Mwanajamii

  Mwanajamii JF-Expert Member

  #8
  Dec 23, 2010
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 7,080
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  Suala la viwanja vya nyerere liko wazi, Rais Kikwete hajakurupuka kuvirudisha bali kuna watu baada ya kuona mwalimu hayupo tena waliona njia bora ni kuchukua viwanja hivyo vinavyoonekana mbele ya nyumba yake.

  Kinachoighalimu familia ya nyerere ni uwezo wa kuendeleza viwanja hivyo hawana.
   
 9. Mwanajamii

  Mwanajamii JF-Expert Member

  #9
  Dec 23, 2010
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 7,080
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  Kumbuka kwamba wakati mwalimu anaanza kujenga nyumba ya kwanza na ya mwisho pekee maishani mwake katika miaka ya sabini mwanzoni eneo hilo lilikuwa msitu na viwanja vilikuwa havijapimwa. Unafikiri mwalimu angetaka kiwanja upanga, masaki, mjini kati au osyterbay angeshindwa? kama viwanja hivyo vya msasani vimepimwa basi ni hatua iliyokuja baadaye sana.
   
 10. Tambara Bovu

  Tambara Bovu JF-Expert Member

  #10
  Dec 23, 2010
  Joined: Dec 19, 2007
  Messages: 586
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  me naona haya maneno yamekaa kizushi kutaka kuwachafua hao watu.mbona sijawahi kusikia maovu yao katika tamaa yoyote ya kifisadi.
  Nyerere ulale pema peponi.AMINA
   
 11. Mwanajamii

  Mwanajamii JF-Expert Member

  #11
  Dec 23, 2010
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 7,080
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  Unapongelea watoto wa nyerere bila shaka jumla yao wako 8 watuhumiwa basi ni Makongoro, Rose na Madaraka tu ambao angalau wanaweza kufuatilia jambo kati ya watoto wote wa mwalimu wengine wote hawako sawa sawa. kuna wengine wameathirika kiakili au kisaikolijia kama vile aliyekuwa rubani wa ndege,John na rubani wa jeshi Andrew huyu dini yake ni Budha. Mhandisi, Magige anaishi kijijini butiama bila kazi sijua kama amewahi kuja hapa Dar kabla na hata baada ya kifo cha baba yake Nyerere. Emel yuko kwenye dini ya padri nkwera aliyetengwa na kanisa katoriki kazidiwa kabisa na imani yake huko ni kama hayuko duniani tena bali yuko ulimwengu wa kiroho. Ni yupi kati ya hao unayemtuhumu kupora ardhi ya watu?

  Walinyang'nywa ardhi yao na watoto wa mwalimu wameonana na mama nyerere kuhusu suala hilo?
   
 12. andrewk

  andrewk JF-Expert Member

  #12
  Dec 23, 2010
  Joined: Apr 13, 2010
  Messages: 3,103
  Likes Received: 55
  Trophy Points: 145
  Naogopa hata kuchangia, tusiwachafue hao watoto wa mzee wetu wanamaadili sama hao,
   
 13. V

  Venoo Member

  #13
  Dec 23, 2010
  Joined: Oct 14, 2010
  Messages: 31
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Basically, wanaodai viwanja kwa jina la mwalimu Nyerere (R.I.P) sio watoto wake, bali 'ndugu' wakiongozwa na bwana anayeitwa MASANZA anayedai ni mpwae mwalimu huyu ndiye aliyesababisha kuvunjwa kwa ofisi ya kata pale namanga - msasani!

  Nashauri kiongozi wa familia atoe tamko la madai haya.
   
 14. Mwanajamii

  Mwanajamii JF-Expert Member

  #14
  Dec 23, 2010
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 7,080
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0

  ndio maana na mimi nilipata shaka na madai dhidi ya watoto wa mwalimu ambao maadili yao ni mfano wa kuigwa kwa watoto wa viongozi japo na wao ni binadamu wanaweza kufanya kile ambacho wote hatukutarajia kufanywa na wao.

  Kutokana na tabia ya watoto wa mwalimu kutopenda makuu inawezekana wajukuu wa mwalimu wameamua kurejesha mali za babu yao. Jambo la msingi sio kuvunjwa kwa ofisi za kata bali kujua kama ofisi za kata zilipanga kiwanja cha nyerere.
   
 15. M

  Mkira JF-Expert Member

  #15
  Dec 23, 2010
  Joined: May 10, 2006
  Messages: 425
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  Hicho kiwanja kilikuwa chake cha siku nyingi na hati anayo ndiyo maana alikubwageni MAHAKAMANI pamoja na hiyo ofisi ya kata. Kuna mtu mmmoja alivamia hapo akajifanya kuwa ni kiwanja chake NA AKARUHUSU SEHEMU KIDOGO IJENGWE OFISI YA KATA , simply kwa kuwa Masanza alikuwa hajakiendeleza!! ni kweli Masanza ni mpwaye mwl kabisa mto wa dada yake, HEBU TUAMBIE NI KIWANJA GANI TENA KACHUKUA!!!?? wACHAg.... KWA KUVAMIA VIWANJA WAKO JUU!!
   
 16. F2S

  F2S JF-Expert Member

  #16
  Dec 23, 2010
  Joined: Feb 16, 2008
  Messages: 216
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Hivi kwa yale yote aliyotenda Mwalimu mpaka kuitwa baba wa Taifa kwanini Serikali isipaendeleze paonekane pazuri na nyumba za kisasa akabidhiwe mama Maria. Kwani bei gani kama hawawezi waanzishe move watu hata nje ya nchi watachangia. Sio mpaka ajenge mpwa yeye analinda eneo mana WaCHaG.. wakilivamia iseee wagumu kuachia. Serikali hebu liendelezeni kumuenzi mwalimu mbona viongozi wengine wastaafu wanamahekalu japo walikuwa wezi tu. Inauma sana kumbe ukifanya kazi kwa uaminifu hupati stahiki yako siku hizi ila ukifanya uovu unavuna stahiki bomba. Mungu tusaidie tunakoenda hatukuoni.
   
 17. hashycool

  hashycool JF-Expert Member

  #17
  Dec 23, 2010
  Joined: Oct 2, 2010
  Messages: 5,899
  Likes Received: 442
  Trophy Points: 180
  duh!
   
 18. F

  Fundi Mchundo JF-Expert Member

  #18
  Dec 23, 2010
  Joined: Nov 9, 2007
  Messages: 4,706
  Likes Received: 61
  Trophy Points: 145
  Uhuni ulifanyika awali. Viwanja vyote vya eneo hilo viliacha eneo kubwa mbele. Hili eneo halikupaswa kujengwa na mtu yeyote. Lakini kutokana na uroho wetu tukaanza kugawa viwanja mpaka kwenye maeneo haya na wale ambao walipewa viwanja wakati wa Nyerere nao wakayaingiza katika milki yao. Sasa mandhari imechafuka kabisa hakuna tofauti na usawa wa gaza.

  Amandla...........
   
Loading...