Pdidy
JF-Expert Member
- Nov 22, 2007
- 50,900
- 21,988
HAKUNA sheria inayotoa haki kwa watoto wanaozaliwa nje ya ndoa, Bunge limeelezwa leo.
Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Frederick Werema, amekiri bungeni kuwa ni kweli watoto wanaozaliwa nje ya ndoa wanapata matatizo mengi hasa yanayohusiana na mirathi.
Werema amewataka wananchi wafahamu athari za matendo yao ya zinaa na wazingatie maadili ya kitanzania.
Mwanasheria Mkuu wa Serikali ameyasema hayo bungeni mjini Dodoma, wakati anajibu swali la nyongeza la Mbunge wa Viti Maalum, Diana Chilolo na swali la msingi la Mbunge wa Viti Maalum, Dk Getrude Lwakatare.
Chilolo aliiuliza Serikali kuwa inawasaidiaje watoto wanaozaliwa nje ya ndoa ambao mama zao huwaficha kutokana na sababu mbalimbali ikiwa ni pamoja na wanaume kuzuia wasitajwe ili kukwepa aibu.
Zipo baadhi ya mila na Desturi huruhusu watoto wanaozaliwa nje ya ndoa kurithi pale watoto hao wanapokuwa wametambuliwa rasmi katika familia na wazazi wao kabla hawajafariki dunia amesema Werema wakati anajibu swali la Dk Lwakatare.
Changamoto hii ni miongoni mwa hoja ambazo zimeifanya Serikali itake kutunga sheria ya mirathi ambayo itashughulikia pamoja na masuala mengine, watoto wanaozaliwa nje ya ndoa amesema Werema.
Kwa mujibu wa Werema, Sheria ya Mtoto Namba 21 ya mwaka 2009 iliyopitishwa bungeni Novemba mwaka jana ni chanzo cha kutambua haki za watoto wakiwemo waliozaliwa nje ya ndoa.