Watoto wa nje ya ndoa hawana haki kisheria:WE NI MMOJA WAO TUNAOMBA MAONI YAKO | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Watoto wa nje ya ndoa hawana haki kisheria:WE NI MMOJA WAO TUNAOMBA MAONI YAKO

Discussion in 'Jukwaa la Sheria (The Law Forum)' started by Pdidy, Jan 31, 2010.

 1. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #1
  Jan 31, 2010
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 35,996
  Likes Received: 6,820
  Trophy Points: 280
  HAKUNA sheria inayotoa haki kwa watoto wanaozaliwa nje ya ndoa, Bunge limeelezwa leo.

  Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Frederick Werema, amekiri bungeni kuwa ni kweli watoto wanaozaliwa nje ya ndoa wanapata matatizo mengi hasa yanayohusiana na mirathi.

  Werema amewataka wananchi wafahamu athari za matendo yao ya zinaa na wazingatie maadili ya kitanzania.

  Mwanasheria Mkuu wa Serikali ameyasema hayo bungeni mjini Dodoma, wakati anajibu swali la nyongeza la Mbunge wa Viti Maalum, Diana Chilolo na swali la msingi la Mbunge wa Viti Maalum, Dk Getrude Lwakatare.

  Chilolo aliiuliza Serikali kuwa inawasaidiaje watoto wanaozaliwa nje ya ndoa ambao mama zao huwaficha kutokana na sababu mbalimbali ikiwa ni pamoja na wanaume kuzuia wasitajwe ili kukwepa aibu.

  “Zipo baadhi ya mila na Desturi huruhusu watoto wanaozaliwa nje ya ndoa kurithi pale watoto hao wanapokuwa wametambuliwa rasmi katika familia na wazazi wao kabla hawajafariki dunia” amesema Werema wakati anajibu swali la Dk Lwakatare.

  “Changamoto hii ni miongoni mwa hoja ambazo zimeifanya Serikali itake kutunga sheria ya mirathi ambayo itashughulikia pamoja na masuala mengine, watoto wanaozaliwa nje ya ndoa” amesema Werema.

  Kwa mujibu wa Werema, Sheria ya Mtoto Namba 21 ya mwaka 2009 iliyopitishwa bungeni Novemba mwaka jana ni chanzo cha kutambua haki za watoto wakiwemo waliozaliwa nje ya ndoa.
   
 2. M

  Mama Joe JF-Expert Member

  #2
  Jan 31, 2010
  Joined: Mar 30, 2009
  Messages: 1,507
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 145
  Tatizo utaona ni watoto ambao mume anakwenda kufanya maovu nje na kutaka warithishwe walichochuma na mke halali. Kama ndo sheria ikate kotekote mama naye akileta mtoto atarithi. Mie nadhani sio sheria ndo suluhu bali maadili na pia maridhiano kama mume amejutia kosa mama akaridhia mtoto alelewe hapo basi anakuwa mrithi. Tatizo ni mama zao wanafanya kusudi kuzaa wapate matunzo, wasomeshewe watoto shule nzuri, mwisho wa mambo baba akifa wanaibuka wagawanywe mali ambazo familia ilijinyima kuzichuma. Kwakweli mie naona hii haijakaa sawa unapocheza na mume wa mtu gizani unategemea utazaa halali? Ni haramu, so bora mama wagangamae wenyewe unless ulibakwa. Sorry ni mtazamo wangu.
   
 3. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #3
  Jan 31, 2010
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 35,996
  Likes Received: 6,820
  Trophy Points: 280
  [​IMG] Today, 12:07 PM
  Mama Joe [​IMG]
  Mama Joe believes in Prayer
  JF Premium Member
  [​IMG][​IMG][​IMG][​IMG] [​IMG] [​IMG]

  MAMA JOE UMEMALIZA KABISA!!!!!!
   
 4. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #4
  Jan 31, 2010
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 35,996
  Likes Received: 6,820
  Trophy Points: 280
  Wanawake wengi wakisikia mmume wa mtu wanajitahidi kuwasakaziia mimba wakijua watasomeshwa na siku moja watoto wao watawatoa sasa wakikutana na mkibosho ambae ajui kuna watoto wa ndani wala wa nje ni segere tupu
  wanawake amkeni akuna mtoto wa nje ya ndoa ;kam baba akumpa malia akiwa hai akifa itapatikana wapi??komaeni mpaka mwisho acheni kunyanyaswa na hiizi nyimbo "ntoto wa kambo"
   
 5. M

  Mama Joe JF-Expert Member

  #5
  Jan 31, 2010
  Joined: Mar 30, 2009
  Messages: 1,507
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 145
  Ni kweli, P didy Watoto wanatia huruma lakini akinamama tuache tamaa na copy and paste. Utaona mwanamke ana option nyingi tu lakini utaona amekazania mume wa mtu kisa familia yake ni nzuri nami ntatunzwa. Hawajui mama naye anamchango wake hapo matokeo vilio siku ya msiba kutoka kwa watu hata huwajui, ulifikiri mama afanye nini. Wanawake acheni ujinga.
   
 6. Tumain

  Tumain JF-Expert Member

  #6
  Jan 31, 2010
  Joined: Jun 28, 2009
  Messages: 3,158
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Hakuna urithi kisheria, lakini mzazi anaweza kuacha wosia kuhusu huyo mtoto wake wa nje akapata sehemu ya mali kupitia wosia

  Kuruhusu mtoto wa nje kupata urithi kama mtoto aliye ndani ya ndoa ni kuruhusu zinaa na uchafu..hii ni amri ya Muumba
   
 7. b

  bitimkongwe JF-Expert Member

  #7
  Jan 31, 2010
  Joined: Oct 21, 2009
  Messages: 3,051
  Likes Received: 236
  Trophy Points: 160
  Maneno hayo!

  Usiniletee mtoto wa haramu mimi SIMLEI NG'O Ulee mwenyewe mama uliyemzaa. Na wala usitegemee mimi kujinyima kwa kila hali wakati mume yuko hai halafu wewe unaleta mtoto kuja kukusanya urithi.
   
 8. ngoshwe

  ngoshwe JF-Expert Member

  #8
  Jan 31, 2010
  Joined: Mar 31, 2009
  Messages: 4,089
  Likes Received: 42
  Trophy Points: 145

  Hoja za haki za hawa watoto wanaitwa wa "nje ya ndoa (illegitimate child/child born out of wedlock)" ni kwenye suala zima la urithi. Lakini sheria haizuii kwa mzazi kuomba kutambulika kwa mtoto husika na pia kupewa matunzo stahiki.

  Dhana ya kutoa haki kwa watoto wa nje ya ndoa, ni kama ilivyo kwa Mwanamke ambaye hakuolewa rasmi nae ni sawa na hawara (concubine) au waweza pia kumwita "illegitimate wife" lakini bado anaweza kutambulika kisheria na kupata haki zake pindi mahusiano yakikoma (kwa mfano kama ameishi na huyo mume kwa muda wa miaka miwili na zaidi na jamii ikatambua na kuthbitisha kulikuwa na maisha yenye hadhi ya "MUME NA MKE/ BWANA NA BIBI".

  Ukisema huwezi kulea mtoto wa nje ya ndoa, ni kama kwamba malezi ya mtoto yapo upande mmoja (yaani mama tu) kwa fikra kuwa akiletwa ndani ya nyumba ni wewe peeke ndie utakaye mlea. Wapo watoto ambao wa nje ya ndoa ambao walizaliwa "kabla ya ndoa" na wale ambao "wamezaliwa baada ya ndoa, ni yupi ambaye huwezi kulea, hata yule ambaye umejulishwa uwepowake mapema???. Hata hivyo, ipo hivyo kwa wengi, mara nyingi katika jamii ambayo mke au mume anakataa kukaa na mtoto ambaye amezaliwa "nje ya ndoa " tena aliyejulishwa kabla ya yeye kufunga ndoa na mzazi wa huyo mtoto huwa kigezo kikubwa inakuwa ni hisia za ubinafsi kwa kujali zaidi wale waliozaa yeye na matzamo wa "mali" baada ya kifo (urith) na jambo jingine.

  Pengine, Binadamu wengi tumekuwa tunapenda zaidi watoto wetu tuliowazaa wenyewe kuliko, wa wengine au twasema tuna mpenda "YESU" au "MTUME" zaidi ambaye hatujamwona kuliko "Mtoto wa binadamu mwenzio" ambaye pengine inakuwa si kosa lake kuzaliwa!). Wazungu ni balaa zaidi, wanapenda "wanyama kama mbwa,, paka, nyani nk" (Pets) kuliko binadamu wenzao.

  Mara nyingi inakuwa rahisi kwa kina mama kusema "siwezi kulea mtoto wa nje" lakini kwa kina baba ni ngumu kutoa kauli hizi kwa kuwa pengine katika maisha mama anaweza kukuchomekea " mtoto ambaye "physically" huwezi kusema ni wako au si wako kwa kuwa "kazaliwa wakati ndoa inaendelea" na aliyebeba mimba kakuambia ni "wako".
   
 9. Alinda

  Alinda Platinum Member

  #9
  Feb 1, 2010
  Joined: Jun 26, 2008
  Messages: 1,542
  Likes Received: 229
  Trophy Points: 160  Tunapofikia kumuita binadamu mwenzio "haramu" kisa tu kwa vile hakuzaliwa ndani ya ndoa, nafikiri tunakuwa tunatenda makosa makubwa sana kwa huyu kiumbe ambaye hakupenda/ hakuchagua kuzaliwa nje ya ndoa, Tusipenda kuwahukumu, kuwadhalilisha, kuwakebehi watoto kwa makosa yasio yao, tukumbuke mali, fedha sio kila kitu katika hii dunia. Tukumbuke pia mtoto anapozaliwa nje ya ndoa hii ni adhabu tosha kwa mtoto asiye na hatia, hawezi kupata nafasi ya kumjua vizuri baba yake, kudhalilishwa, matusi ni juu yake na nk. na kinachosikitisha zaidi ninapoona mtu mzima mwenye watoto, anamdhalilisha huyu mtoto let say mwenye miaka chini ya miaka 10 katika hii dunia kwangu mimi huu ni uzindikazi na ukosefu wa huruma (samahani kama nitakuwa nimekwaza mtu)

  Nafikiri ufike wakati watunga sheria wawafikirie hawa watoto, watunge sheria ambazo zitawalinda na kuwatambua katika familia zao, hii itapunguza watoto wa mitaani pia inawafanya wanaume wafikirie mara mbili kabla hawajaamua kufanya tendo la ndoa.
   
 10. Kafara

  Kafara JF-Expert Member

  #10
  Feb 1, 2010
  Joined: Feb 17, 2007
  Messages: 1,396
  Likes Received: 80
  Trophy Points: 145
  kwa wale ambao hupata mtoto/watoto na jamaa kabla ya kuoana
  na kisha baadae wakaoana, je kweli watawaita watoto wao waliozaliwa
  kabla ya ndoa watoto haramu? je hao watoto waliozaliwa kabla ya
  harusi watanyimwa urithi?
   
 11. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #11
  Feb 1, 2010
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 80,465
  Likes Received: 117,259
  Trophy Points: 280
  Ahsante sana Alinda kwa mchango wako mzuri sana ambao umenigusa sana. Kuwaita hawa watoto kwamba ni watoto haramu si kuwatendea haki hata kidogo. Labda wengi wetu tumebahatika kuzaliwa ndani ya ndoa, fikiria kama ingekuwa bahati mbaya ungezaliwa nje ya ndoa na watu kukuita wewe kama ni mtoto wa haramu, utaumia sana kwa kuitwa hivyo na hayo yaliyotokea wewe wala hukuwa na uwezo wa kuyabadilisha ili usizaliwe nje ya ndoa.
   
 12. MwalimuZawadi

  MwalimuZawadi JF-Expert Member

  #12
  Feb 1, 2010
  Joined: Sep 1, 2007
  Messages: 643
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Wakuu JF
  Tatizo la miaka hii lina utofauti kidogo na enzi zetu. Kuna baadhi ya wasichana wanafanya makusudi kujiachia wakidhani wakiwa na mtoto ni tiketi ya ndoa. Si unajua tena vijana wengi siku hizi wanadai wanataka familia moja kupunguza gharama, hata kama vi concubine vitakuwepo. Sasa na wanaumewengine akili zao wanazo wenyewe. Hata umfanye nini hata uzae wangapi, kama ameamua kutokukuoa ameamua. Kundi hili la watoto ndio kubwa kwa sasa na linazidi kuongezeka.
  Pia kuna kundi la wanawake wanaodhani ndoa nuksi, bora kuzaa na kuwa na watoto wao bila mume. Sasa nao watoto wao wanakuwa kundi hili la watoto wa nje ya ndoa. Tofauti hapa hawa wanawake wa aina hii huwa hawana shida ya mali toka kwa mwanaume kwani hili ni kundi la wanaoona wamesoma na wana kazi mzuri, mume wa nini.
  Lakini tukubali hawa watoto ni watoto, wawekwe kundi gani, waitwe jina gani sijui, ila ni watoto
   
 13. Ngongo

  Ngongo JF-Expert Member

  #13
  Feb 1, 2010
  Joined: Sep 20, 2008
  Messages: 12,324
  Likes Received: 3,910
  Trophy Points: 280

  Heshima kwako Alinda.

  Maneno yako mazito sana,nimerudia kulisoma andiko lako mata tatu.
  Lazima nikiri kwamba nilikuwa nishushe nondo nzito za kuwakandamiza watoto wa nje ya ndoa lakini baada ya kusoma hoja zako kwa makini nimegundua kitu kimoja kikubwa "mtoto wa nje ya ndoa hakuchagua kuzaliwa nje ya ndoa laiti angepewa fursa ya kuchagua kwa vyovyote asingekubali kuzaliwa katika hali ya kudhalilika".

  Wako watoto wanaozaliwa kabla ya baba ajafunga ndoa "watoto wa ujanani" utakuta mwanamke kabla ajaolewa anaelezwa kabisa kuna mtoto lakini mara nyingi wanawake wanawabaugua kiasi kwamba unashindwa kuwaelewa kabisa.
   
 14. n

  nndondo JF-Expert Member

  #14
  Feb 1, 2010
  Joined: Feb 1, 2010
  Messages: 1,250
  Likes Received: 539
  Trophy Points: 280
  nadhani mmesema yote, ukweli unabaki kwamba kutambulika na familia ya mhusika hakukupi haki ya urithi wa mali, na hata hao wanaharakati wa haki za mtoto wanayasema hayo kwa kutaka umaarufu wa muda mfupi, kwanza wengi wao labda hawajui tu kwamba waume zao wanawatoto chungu nzima wa nje, sasa wameshawahi kufikiria siku wao wakitangulia ama huyo mwenzao, watoto wao waje kwenye majadiliano ya kugawana mali zao na watoto wa wasiowao? hivi kuna faida gani ya kuchuma na kulimbikiza kama sio ku protect wale unaowapenda? si jukumu la kila mtu kupenda watoto wa kila mtu, kila mtu apende na alee wake. Mbona hamzungumzii umuhimu wa hao wakina baba kuwaandalia hao watoto wa nje maisha na mali kabla zao kabisa? tufike mahali tujifunze kuvuna kwa jasho letu, hii sheria ni nzuri sana maana kulikua na confusion, watoto wa nje walishaota mapemba wakitaka migao na kufanya sherehe, concubines nao walishaingia mtaani kutishia amani za watu, huree werema
   
 15. Domo Kaya

  Domo Kaya JF-Expert Member

  #15
  Feb 1, 2010
  Joined: May 29, 2007
  Messages: 530
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Mimi sikubaliani na hii hoja hapo juu kabisa, hakuna mtu anayefanya makusudi kupata mtoto ili aolewe, kwanza nani alisema kuolewa lazima? au nani alisema mtoto ndio ticket ya ndoa, Tendo la kupata mimba mwanamke anayehusika ni mwanaume, kwani nini ukafanye mapenzi bila kinga, then mwanamke akipata mimba usingizie yeye ndio chanzo eti kalengesha apate mimba ili aolewe, wizi mtupu, je ukipata ukimwi utasema aililengesha ili iweje....??????/ Watoto wa nnje ya ndoa ni watoto wetu na wanahaki sawa na watoto wa ndani ya ndoa, wanahitaji malezi mazuri na elimu pia, hawana makosa yoyote, makosa ni ya wazazi wao waliowaleta duniani,

  mimi kiukweli naumia sana na hili swala la watoto wa nnje ya ndoa....WATOTO WOTE NI SAWA, unakuta mtoto anapata shida huku baba yake anakula bata na kuponda maisha huku akiendelea kutembea nnje ya ndoa akipata tena kid huko atasema mtoto wa NNJe ya ndo. Damn it.
   
 16. MwanajamiiOne

  MwanajamiiOne Platinum Member

  #16
  Feb 1, 2010
  Joined: Jul 24, 2008
  Messages: 10,476
  Likes Received: 87
  Trophy Points: 145
  Umenichekesha hapo Mama Joe- tatizo ni kuthibitisha kuwa huyu mtoto kaletwa na mama- au ndo itabidi watoto wote wapimwe DNA?
   
 17. ngoshwe

  ngoshwe JF-Expert Member

  #17
  Feb 1, 2010
  Joined: Mar 31, 2009
  Messages: 4,089
  Likes Received: 42
  Trophy Points: 145
   
 18. akashube

  akashube JF-Expert Member

  #18
  Feb 1, 2010
  Joined: Dec 24, 2009
  Messages: 411
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 33
  Sheria Ikiwa kiongozi cha maadili!!!!!!!!!!

  Wakuu kwenye hili naomba msaada wa kitaalam na kijamii upande wa pili, pengine hapo juu mirathi pale wazazi wanapofariki...n.k

  Je ikitokea mtoto wa nje ya ndoa amekuwa mtu mzima na kufanikiwa sana kimaisha ....suala la kuwatunza ndugu na wazazi inakuaje hapo. Na kama ikitokea huyu huyu tunayemuita 'mwanaharamu' akafariki na kuacha mali, magari, majumba, mashamba, biashara mbalimbali, pesa...naomba niulize wataaluma mnisaidie, ikiwa na yeye hakuacha mwenzi wala watoto..hizi mali zote hizi inakuaje? nani mrithi au serikali?

  Chukulia wazazi wote na ndugu wote wako hai, haooo wasio 'wanaharamu'

  EENH inakuaje hapo wakuu....au ndo kugombea maiti tena!!?? ya nani? 'mwanaharamu'? AU UNAKUWA MWANAHARAMU UNAPOKUWA MUHITAJI. UKIULA KILA MTU HATA YULE ALIYEKUFUKUZA UKAENDA KUWA CHOKORAA MITAANI ANADAI ALIKULEA????????TAJIRI HAKOSI NDUGU???
   
 19. Dark City

  Dark City JF-Expert Member

  #19
  Feb 1, 2010
  Joined: Oct 18, 2008
  Messages: 16,277
  Likes Received: 288
  Trophy Points: 180

  Kweli BAK,

  Mtoto hana hatia na hakuna sababu yoyote ya kumnyanyapaa au kumnyanyasa. Kwa hiyo inabidi sheria iwabane wahusika. Wamlee mtoto kwa kadri ya uwezo wao kama wanavyolelewa watoto waliozaliwa kwenye ndoa na pia wazazi waandika wosia na kuwapa urithi kwa kadri ambavyo wao wangependa badala ya kusubiri mambo yaamuliwe baada ya wahusika kufariki. Haramu au siyo haramu ni matumizi mabaya ya maneno ambayo yanasababisha mateso makubwa kwa binadamu wenzetu. Shida kubwa ni watu kuendekeza kuficha vitu ambavyo vimeshatokea na hawana uwezo wa kubadili historia hadi wanapokuja kuumbuliwa na msiba.
   
 20. Dark City

  Dark City JF-Expert Member

  #20
  Feb 1, 2010
  Joined: Oct 18, 2008
  Messages: 16,277
  Likes Received: 288
  Trophy Points: 180

  Jibu umelitoa mwenyewe. Kuna msemo kuwa, "bibi mwenye ndizi mbivu hakosi wajukuu". Hiyo maiti itakuwa dili na watu wako tayari kutoana macho kama siyo roho. Lakini ngoja mtoto kama huyo aje kuomba uniform wakati anasoma shule, ...hahhh, hilo ni balaa. Kila mtu atakuja uso kama kanyweshwa shubiri!! Maisha ndio yalivyo...dhamani ya mtu ni alichonacho; mkono mtupu haulambwi ndugu!
   
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
Loading...