Watoto wa mwisho kwenye familia wanaharibika kutokana na malezi ya wazazi

msemakweli2

JF-Expert Member
Jul 28, 2013
1,627
1,880
Ni hivi majuzi tu mdogo wangu wa mwisho kafunga chuo akaja nyumbani kwangu kukaa DSM, nikaona nimtafutie shughuli ya kufanya ofisini kwangu, amefanya asubuhi naondoka naye na kurudi naye jioni.

Chaajabu baada ya week moja ameacha ile kazi analala tu nyumbani week iliyopita nimemtafutia tena kazi nyingine trip ya kusafiri nje ya mkoa wa DSM wanalipwa laki kila siku wanakaa mwezi mmoja.

Lakini chaajabu bi mkubwa ananiambia huko ni mbali afadhali akae nyumbani tu, duuuh! Nimeshangaa kweli mtu yupo third year bado anabembelezwa kama mtoto na ni mtoto wa kiume huyu.
 
sawa mwache akae nyumbani bi mkubwa atakapo sepa na kuenda kwa baba atapata akili
 
Kaa na huyo dogo mwelezi maisha yalivyo asifikiri bi mkubwa anamtakia mema baadaye atakuwa mzigo wako.
 
Mwache siku hilo kochi aliloegemea likiondoka atajua wapi na nini afanye ili aishi
 
sasa mkuu humu ndan wapo watu weng sana wanaotafuta kaz sasa hyo nafas ya mwanao bora mmpe kijana mmoja apate hata pa kujishkiza kwa muda
 
Mungu ni wa ajabu sana kwenye kutoa riziki kwa watu... Watu wengne tunakosa ndugu wenye mioyo safi ya kutusaidia kutupa michongo ya ukweli halafu mtu anakuwa na watu wa kumpa michongo halafu hana habari na michongo yenyewe...
.dah nimetamani sana uwe bro wangu ila ndo hivyo tu ushazaliwa kwa huyo dogo....ila sa nyingne dogo inawezekana mnamwaribu wenyewe yaani unakuta kila kitu akiomba mnampa kwa hiyo hajui shida sasa anaona haangaike na kazi ili agundue nini.
 
msemakweli2 naomba hiyo dili mie ntakupa percent zako :p
Kinamama wengine sijui vipi anamlea mtoto utadhani ataishi nae milele pole zake
 
Si peke yako msemaukweli2! Na mimi ninae ndugu yangu last born dizaini ni hizo hizo! Akiharibu huku anaenda kwa sis, akivuruga huko anaenda kwa bro! Ukimtamfutia shughuli haitaki na bimother anamkingia kifua mwanae! Yaani tuwe nao tu lkn hawana kheri hawa
 
Ndio maana wazee wa zamani walisema Upele humkua asie na kucha.
100000x30 =3,000,000= aisee kwa kuanzia tayari Dogo anakamladi kitaa Tigo pesa/m pesa
 
Ni hivi majuzi tu mdogo wangu wa mwisho kafunga chuo akaja nyumbani kwangu kukaa DSM, nikaona nimtafutie shughuli ya kufanya ofisini kwangu, amefanya asubuhi naondoka naye na kurudi naye jioni.

Chaajabu baada ya week moja ameacha ile kazi analala tu nyumbani week iliyopita nimemtafutia tena kazi nyingine trip ya kusafiri nje ya mkoa wa DSM wanalipwa laki kila siku wanakaa mwezi mmoja.

Lakini chaajabu bi mkubwa ananiambia huko ni mbali afadhali akae nyumbani tu, duuuh! Nimeshangaa kweli mtu yupo third year bado anabembelezwa kama mtoto na ni mtoto wa kiume huyu.
Nichukue mm mkuu unitreat kama mmdogo wako
 
Wallah mi wa mwisho ila nabeba majukumu utadhani ndo wa kwanza ila namshkuru bi mkubwa mkali kinyama yani ndugu zangu ndo walikua wananibebisha bi mkubwa akawaambia mwacheni akomae mtoto mpende kwa tonge na mavazi mengine akomae na kweli chuo nimeatruggle mpaka namaliza, field nimetafuta mwenyewe na kazi nimepata mwenyewe na ni nje ya mkoa unapewa kianzio kidogo na Biblia mwanangu maisha mema kila la kheli sala na neno la Mungu ndo kiongozi wako heshimu kila mtu mkubwa kwa mdogo utafanyiwa sala ya ulinzi na baraka kushnehi hahahaaa aiseee aafu ni mtoto wa kike leo hii wa kiume anapiganiwa na kaka anazingua daaah
 
Msemakweli yaan wahanga tuko wengi. Me nilijua tu huyu wangu ndo pasua kichwa...aisee me nishaka nakaaga kimya tu. Amalize tu chuo arud kwa wazazi wake ambao kila cku wao kazi kumtetea. Yan ata kupika hataki na wala hawezi
 
Back
Top Bottom