Watoto wa mitaani ni Bomu linalosubiri kulipuka: Watawala amkeni | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Watoto wa mitaani ni Bomu linalosubiri kulipuka: Watawala amkeni

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by We can, Jan 27, 2011.

 1. W

  We can JF-Expert Member

  #1
  Jan 27, 2011
  Joined: Sep 4, 2010
  Messages: 681
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Ndg wana JF.

  Siku zote huwa naguswa sana na hawa watu wanaoitwa watoto wa mitaani. Mara nyingi hawa watoto hawana baba na mama, na wakati mwingine hawana ndugu kabisa. Watoto hawa hulandalanda mchana na kulala popote usiku. Hupigwa jua mchana na baridi usiku. Wakiomba chakula hufukuzwa na wakati mwingine hujibiwa vibaya. Matokeo yake watoto hawa wanajikuta wakotoa maneno machafu mara kwa mara. Je, hili si bomu kwa Taifa?

  Wanaonekana kabisa kuwa hawana chembe ya maadili, hawajui neno HURUMA, hawatambui neno NISAMEHE. Wengine hawajawahi hata kuambiwa NAKUPENDA, POLE, nk. Watoto hawa hawaendi shule, hawajui maana ya matibabu. Je, hili si bomu kwa Taifa?

  Kadri Taifa letu linavyofumbia macho uwepo wa bomu hili, ndivyo Taifa linapojiweka kwenye hatari zaidi. Je, bomu hili likilipuka, nani atalizuia? Hawa hawatatishwa na dola, kwani hawajui nini maana ya dola. Huwezi kuwatishia jela, kwani jela kwao ni afadhali kuliko maisha waishiyo. Je, hili si bomu kwa Taifa?

  Ndg zangu hebu tuorodheshe hatari zingine za kuwa na kundi hili la ndugu zetu waitwao watoto wa mitaani...
   
Loading...