Watoto wa Mengi wamburuza mahakamani Jacqueline Mengi "Klynn"

Kanungila Karim

JF-Expert Member
Apr 29, 2016
20,744
25,438
DAR ES SALAAM:
MJANE wa aliyekuwa mfanyabishara bilionea Dk Reginald Abraham Mengi, Jacqueline Ntuyabaliwe ‘K-Lynn’ hana namna zaidi ya kupambana jino kwa jino kortini na watoto wengine wa Mengi ili kutetea urithi wa mali za marehemu mumewe, Gazeti la Ijumaa linakujuza.

Baada ya kifo cha Mengi aliyekuwa Mwenyekiti Mtendaji wa Makampuni ya IPP Limited, gumzo lilikuwa ni vipi mgao wa mali utafanywa ili warithi wote wapate haki zao akiwemo K-Lynn na wanawe wawili aliozaa na Mengi, Jarden na Ryan.


MAMBO YAIVA
Urithi utakuwaje na na wasiwasi ulipozidi kuwa K-Lynn na wanawe wako kwenye wakati mgumu zaidi kupata haki zao za mirathi wosia uliodaiwa kuachwa na marehemu Mengi ulivuja mitandaoni na kuainisha mgawanyo wa mali zake utakavyokuwa.

Wosia huo uliwataja warithi wa mali kuwa ni mjane wake, Jacqueline, watoto wake, Jarden na Ryan na kuwaweka kando kabisa Regina na Abdiel Mengi ambao ni watoto wakubwa wa marehemu mkewe mkubwa, Mercy Mengi.

Aidha, sehemu ya wosia huo ambao awali ulionekana kuwa ni feki kabla ya kuthibitika ukweli wake, inasomeka kuwa marehemu hakuwapa haki baadhi ya warithi wake halali kwa makusudi.

MPAMBANO WAFIKA MAHAKAMANI
Baada ya wosia huo kutoka na kutangazwa rasmi kwenye Gazeti la Daily News la Julai 30, 2019 kisha kuwasilishwa mahakamani na kuandikishwa kwa kesi ya mirathi namba 39, ya mwaka 2019 ndipo pingamizi lilipotolewa.

Aliyewasilisha pingamizi hilo kwa niaba ya watoto wa marehemu na familia ni mdogo wa marehemu Mengi, Benjamin Mengi ambaye amedai mbele ya mahakama kuwa wosia huo ni batili kwa sababu wakati kaka yake, Dk Mengi akiuandika, alikuwa amechanganyikiwa.


K-LYNN, WATOTO WA MENGI USO KWA USO KORTINI
Septemba 16, mwaka huu ilikuwa siku ya mjane huyo wa marehemu na watoto wakubwa sambamba na familia zao kukutana uso kwa uso mbele ya Jaji Josi Myambina kuanza harakati za kutafuta haki mahakamani.

Upande wa pingamizi unaowajumuisha Regina na Abdiel unaongozwa na Wakili Nikael Tenga huku upande wa usimamizi wa mirathi unamjumuisha K-Lynn na familia yake ukiongozwa na wakili Elisa Msuya.

Mwandishi wetu ambaye alifika mahakamani siku kesi hiyo ikitajwa alizishuhudia pande hizo mbili zikikutana kwa makundimakundi na kuwa na mijadala ya hapa na pale.

Mara zote K-Lynn alionekana akiongoza na wakili wake huku wakizungumza mambo ambayo mwandishi wetu hakuweza kuyafahamu.
Pamoja na yote, msingi ulio wazi uliozifikisha mahakamani hapo pande hizo mbili ni mambo ya mirathi na hasa wosia wa marehemu anaodaiwa kuuandika Agosti 17, 2017.

Katika wosia huo, marehemu Dk Mengi umewataja wasimamizi wanne wa mirathi ambao ni Benson Benjamin Mengi, William Mushi ambaye ni Msimamizi Mkuu wa Bonite Bottlers Limited na Silvia Mushi ambaye ni Mwanasheria wa Makampuni ya IPP.

Mali alizoacha bilionea huyo na kuzirithisha kwa K-Lynn na wanaye kwa mujibu wa wosia huo ni pamoja na fedha, ardhi, magari, nyumba na hisa zake zote kwenye makampuni yake yote.

Baadhi ya makampuni hayo ni IPP Limited, The Guardian, Tanzania Africa Limited, Diamonds Africa Limited, Energy Tanzania Limited na mengine huku nguo za marehemu vito na saa ya thamani kwa mujibu wa wosia vikirithiwa na watoto wake wadogo yaani Jarden na Ryan.

Kikwazo kilichowekwa kwenye wosia huo unaodaiwa kuandikwa na Mengi wakati akiwa si timamu kiakili umeweka zuio la mrithi yeyote halali kuupinga mahakamani na endapo akifanya hivyo na kushinda, wosia huo umeanisha kiasi cha shilingi elfu moja kuwa sehemu ya malipo yake.


MAWAKILI WAGOMA KUTOA UFAFANUZI
Mwanahabari wetu, akiwa mahakamani siku hiyo alitaka kuzungumza na mawakili wa kesi hiyo ili waweze kudadavua machache kuhusu shauri linaloshindaniwa, lakini waligoma kutoa ufafanuzi zaidi.

“Aaah kwa kweli mimi sina la kuzungumza nafikiri kesi umeisikiliza mwenyewe la msingi ni kwamba itaanza kusikilizwa rasmi mwezi ujao basi tusubiri,”alisema wakili upande wa pingamzi.

Wakili kwa upande wa mirathi, Msuya alisema yeye hana la kuzungumza katika maswali yote aliyoulizwa na mwandishi wetu.

Credit : Richard Bukos
 
Hapa ndo unaona logic iliyopelekea waarabu kuoana kindugu ndugu ili kulinda "chao".
Mwisho wa hii kesi unaweza kuta hao watoto wadogo wa Mengi wakaja kuanza kutafuta mali from the scratch (though si scratch kama yetu) wakati baba yao alikuwa business mogul.
 
Back
Top Bottom