Ghazwat
JF-Expert Member
- Oct 4, 2015
- 23,718
- 66,262
Vilio na simanzi vimetawala Ukonga Magereza kufuatia vifo vya watoto wawili wa maofisa wa Jeshi la Magereza waliofariki dunia kwa kukosa hewa, baada ya kujifungia kwenye gari la mmoja wa wazazi wao walimokuwa wakicheza
Tukio hilo limetokea juzi jioni katika Kota za Magereza Ukonga wakati wazazi wao wakitengeneza gari hilo
Watoto waliopoteza maisha ni mtoto wa Mrakibu wa Jeshi la Magereza (ASP) Demetrus Masala, aitwaye Mariam (6) ambaye alikuwa darasa la kwanza katika shule ya St. Theresa Ukonga na Sajini Francis, ambaye ni Esther (4) Mwanafunzi wa Chekechea
Kwa mujibu wa mashuhuda ambao hawakupenda majina yao yaandikwe gazetini, Watoto hao walipoteza maisha katika gari lenye namba za usajili T291 CXR aina ya Toyota Passo, mali ya ASP Masala
Imedaiwa kuwa siku ya tukio gari hilo liligoma kuwaka na ndipo Masala alipokwenda kumuomba jirani yake Francis anayeishi chumba cha pili aje amsaidie kuliwasha. Francis ambaye ni dereva katika Ofisi ya Mwanasheria Mkuu, walishirikiana na Masala kuliwasha gari hilo kwa muda mrefu lakini hata hivyo lilishindikana kuwaka
Wakati wazazi hao wakiendelea kulitengeneza gari hilo ndipo watoto hao waliposogelea. Hata hivyo, waliwafukuza lakini kumbe watoto hao waliingia kwenye gari bila wao kufahamu kwa sababu gari hilo lilikuwa na vioo vya giza(Tinted).
Alisema baada ya kushindikana, ndipo Francis alipomwelekeza mwenzake kwa fundi ambaye angeweza kulitengeneza gari hilo
"Kutokana na ushauri huo, Masala aliamua kulifunga gari lake na kuondoka kumfuata fundi bila kufahamu kama watoto wameingia ndani ya gari", kilisema chanzo hicho
Ilidaiwa baada ya kukaa kwa muda mrefu Francis, alibaini watoto hao wawili hawaonekani na ndipo walipoanza kuwatafuta bila mafanikio. Wakati wakiendelea kuwatafuta, kuna kijana akawadokeza kuwa wakati gari hilo likiendelea kutengenezwa, Watoto hao walikuwa ndani ya gari yake
Kauli hiyo inadaiwa ndiyo iliyomshtua Francis na kuamua kuchungulia ndani ya gari hilo ambapo alibaini watoto hao wakiwa wamekaa kiti cha nyuma wamelala fofofo, huku mwingine akivuja damu puani.
Hali hiyo ilisababisha Francis na wengine waliokuwepo eneo hilo kusogea na kuvunja kioo cha gari na kuwatoa watoto hao wakiwa katika hali mbaya
Inadaiwa kuwa kwasababu ya hali hiyo waliyokuwa nayo, waliamua kuwawahisha katika Hospitali ya Kardinali Rugambwa iliyoko Ukonga kwa ajili ya matibabu ya haraka, lakini hata hivyo walibaini mtoto Mariam tayari amefariki dunia
Madaktari walijaribu kumpa huduma ya kwanza mtoto Esther kwa kumwongezea Oksijeni na baadaye walimpeleka katika Hospitali ya Amana iliyoko Ilala na kubaini tayari naye amekufa.
Akizungumzia tukio hilo, Mwenyekiti wa Serikali za Mtaa wa Mwembe Madafu, Deus Nchimbi, alisema kifo cha watoto hao ni pigo kwa familia hizo marafiki.
"Kikubwa ni kuomba amani na kuwaomba marehemu lakini watoto wamekufa kifo cha uchungu kwa kukosa hewa huenda wangekuwa wakubwa wangeweza kufungua gari,"alisema Nchimbi
Alisema kilichobaki ni kuikumbusha jamii kuwa makini na vyombo vya moto na kuwapa uhuru watoto waweze kufahamu aina ya mali zilizopo nyumbani.
Chanzo : JamboLeo