Watoto wa Kiholanzi watoa msaada wa Sh420milioni kwa watoto Tanzania | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Watoto wa Kiholanzi watoa msaada wa Sh420milioni kwa watoto Tanzania

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Lunyungu, Jul 13, 2009.

 1. Lunyungu

  Lunyungu JF-Expert Member

  #1
  Jul 13, 2009
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,836
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145
  Watoto wa Kiholanzi watoa msaada wa Sh420milioni kwa watoto Tanzania[​IMG]Na Abdallah Bakari,Mtwara

  WATOTO wa kikristo nchini Uholanzi wametoa msaada wa vitu mbalimbali venye thamani ya Sh 420 milioni kwa watoto wenzao wenye itikadi hiyo hapa nchini katika kipindi cha mwaka huu.

  Msaada huo uliotolewa umetolewa kwa watoto wenye umri wa kuanzia umri wa miaka miwili hadi 14 wa mikoa ya Singida, Mbeya, Mwanza, Morogoro, Dar es Salaam na Mtwara.

  Akisoma risala katika hafla ya uzinduzi wa ugawaji wa msaada huo mkoani Mtwara, Askofu wa Kanisa la Maranatha Reconciliation ambalo lilikuwa linaratibu msaada huo kwa niaba ya makanisa mengine, Rodrick Mbwambo alisema msaada huo ulitolewa na watoto hao wakati wa sherehe za Kristmasi.

  “Maono ya ugawaji wa zawadi hizi yalianza katika nchi ya uingereza pale Mzee David Cock alipowaona watoto masikini wa Romania wakiokotaokota vitu vitu katika mapipa ya taka, baada ya kuona hivyo aliomba watoto wa Uingereza wajitolee kuwapelekea wenzao wa Romania zawadi kama kielelezo cha upendo” alisema Askofu Mbwambo.

  Alisema katika Mkoa wa Mtwara, watoto 3,060 watanufaika na msaada huo wenye gharama ya Sh 6 milioni ambapo pia alitumia fursa hiyo kuishukuru serikali kwa kurejesha msamaha wa kodi kwa taasisi za kidini.

  “Iwapo serikali ingeendelea na msimamo wake wa kuzifutia msahama wa kodi taasisi za kidini msaada huu leo tusingeupata, hivyo natumia fursa hii kuipongeza serikali kwa uamuzi wake huo wa busara”alisema askofu huyo.

  Akizindua msaada huo kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya ya Mtwara, Afisa Tarafa ya Mikindani, Hassan Mchopa alisema ni vema kwa viongozi wa dini kuheshimu uwamuzi huo wa serikali kwa kuonyesha uadilifu katika kutekeleza zoezi nzima la kuingiza misaada nchini. “Nawaomba viongozi wa dini kuuenzi uamuzi wa serikali kwa kuwa waadilifu wakati wa kuingiza misaada kutoka nje ya nchi, tunafahamu wapo wachache waliokuwa wanatumia nyadhifa zao vibaya, hima tuwapige vita si wacha Mungu hawa,” alisema Mchopa.
  Tuma maoni kwa Mhariri  Nategemea hili halitapigiwa kelele na waislam wenzetu jamani .​
   
Loading...