Watoto wa Dar wanakosa nidhamu

Stroke

JF-Expert Member
Feb 17, 2012
34,631
40,789
Ukitaka kuhakikisha hili, panda basi za mwendokasi.

Utawakuta bila aibu hata kidogo wamekaa kwenye viti na hawataki kuwapisha watu wazima. Yaani mtoto mdogo kabisa kakaa kwenye siti bibi yake kasimama na kuegemea mlingoti.

Sijui wanatoka katika familia zipi ambazo nidhamu ni msamiati.
 
Kwani watoto hawastahili kukaa?

Mimi naona kwenye subway watu wazima wanapisha watoto. Kwa fikra kwamba watu wazima wanaweza kustahimili kusimama kuliko watoto.
 
Mlizoea kuwanyanyasa kwenye daladala. Unakuta mtu wa miaka 24-40 ana afya nzuri tu anakubali kukaa kiti anachonyanyuliwa mwanafuzi wa darasa la tatu aliekaa shule siku nzima kachoooka!!! Na wewe na utu uzima wako unakaa kisa wewe umelipa 400 mwanafunzi kalipa 100, mtakoma sasa hiviatainuka mwanafunzi kwa heshima na sio kwasababu analipa nauli ndogo.
 
Maadili yameporomoka ndugu yangu! mie hata kanisani kwetu huwa ninashangaa mama kaja na mwanae amekaa naye, akija mkubwa, wasimamizi wa kanisa wakimwambia mtoto aende kukaa sehemu ya watoto ampishe mkubwa, mama mtu anakuwa mkali, "hebu mwache mwanangu, yaani amewahi kiti halafu umtoe kisa huyo aliyechelewa" sasa huyu mtoto unategemea awe na adabu ya kupisha wakubwa kiti?
 
Mkuu huku kajamba nani alielipa nauli kubwa ndio anakaa....utashangaa kitoto cha la kwanza kinainuliwa akae mtu wa 25yrs kisa nauli yake kubwa.
 
Mlizoea kuwanyanyasa kwenye daladala. Unakuta mtu wa miaka 24-40 ana afya nzuri tu anakubali kukaa kiti anachonyanyuliwa mwanafuzi wa darasa la tatu aliekaa shule siku nzima kachoooka!!! Na wewe na utu uzima wako unakaa kisa wewe umelipa 400 mwanafunzi kalipa 100, mtakoma sasa hiviatainuka mwanafunzi kwa heshima na sio kwasababu analipa nauli ndogo.
upo nchi gani ?
 
Yaani hawana utu kabisa watu wengine. Unakuta mtu mzima na afya yake anakenua tu mtoto wa darasa la tatu anainuliwa akae yeye!
tena kuna mwingine mtoto akisimama halafu akamuegemea,anamkemea mtoto km kamkojolea au kamuomba nauli vile
mi nshaona Dada mmoja anamkemea katoto ka darasa kwanza mi nkamchukua na kumpakata yule mtoto
 
Maadili yameporomoka ndugu yangu! mie hata kanisani kwetu huwa ninashangaa mama kaja na mwanae amekaa naye, akija mkubwa, wasimamizi wa kanisa wakimwambia mtoto aende kukaa sehemu ya watoto ampishe mkubwa, mama mtu anakuwa mkali, "hebu mwache mwanangu, yaani amewahi kiti halafu umtoe kisa huyo aliyechelewa" sasa huyu mtoto unategemea awe na adabu ya kupisha wakubwa kiti?
Kwa nini tunafikiri mtoto hastahili kukaa kwenye kiti?
 
6 Reactions
Reply
Back
Top Bottom