Watoto ombaomba ni halali kutolewa Mjini? Wakikamatwa Serikali inawapeleka wapi?

John Haramba

JF-Expert Member
Feb 4, 2022
365
1,373
Suala la watoto wa mitaani kwa sasa ni kama halizungumzwi kwa sauti kubwa kwa kuwa hapo kati mamlaka zikishughulika nao kwa kiwango cha juu.

Nakumbuka kuna wakati Mzee Yusuph Makamba miaka ya nyuma alipokuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam alipambana sana na ombaomba wakiwemo watoto waliokuwa wakifanya kazi hiyo, pia kulikuwa watoto wa mtaani ambao hawakuwa wakiomba lakini walikuwa wakizungukazunguka mjini pasipokuwa na kazi maalum ya kufanya.

WATOTO WA MITAANI WEB.jpg
Ondoa ya ombaomba iliwagusa hadi watoto ambao kwa asilimia kubwa jamii iliona kama wanaonewa.

Hata sasa imani hiyo ya kuwa watoto wa mtaani wamekuwa wakionewa bado ipo, ukizungumza baadhi ya mitaa hasa ya Dar es Salaam watoto ambao wanafanya shughuli za kuombaomba wapo na wanaendelea na matendo hayo licha ya kuwa wamekuwa wakiondolewa mara kadhaa.

Leo nataka niwazungumzie watoto ambao wamekuwa waathirika wakubwa katika mazingira ya ombaomba wa mitaani kisha nitarudi kwa ajili ya kuzungumzia watu wazima ambao nao wanahusika katika matukio hayo.

Justine Kaleb ambaye ni Wakili wa Kujitegemea na Mwandishi wa Vitabu vya Sheria, kutoka Kampuni ya Mawakili ya Moriah Law Chambers anafafanua zaidi kuhusu watoto ombaomba na maamuzi yanayochukuliwa na mamlaka kuhusu watoto hao:

“Kuna sheria kadhaa zinazowazungumzia watoto na hata watu wazima wanaojihusisha na masuala ya kuombaomba mitaani, kwanza itambulike kuwa hiyo siyo shughuli rasmi kwao na hata kwa watu wazima.

“Kwanza kabisa sheria inamtambua mtoto ni mtu yeyote ambaye ana umri usiozidi miaka 17, na inataja haki ambazo mtoto anatakiwa kuzipata kutoka kwa mzazi, mlezi au yeyote ambaye anajukumu la kumuangalia na kumlea.

“Baadhi ya haki za mtoto ni kama kupata elimu, afya, matunzo, uangalizi, kuwa na uhusu wa kutoa maoni na mengine mengi.

“Sheria inaweka wazi kuhusu jinai kama mtoto hatapata uangalizi wa kupewa haki zake za msingi kama hizo nilizozitaja, mamlaka zinaweza kuchukua hatua kama mtoto hatakuwa katika mazingira ya kulindwa na muhusika au wahusika.

“Pili, kuna sheria za mamlaka za Serikali za mtaa ambazo zimeweka utaratibu wake wa nini cha kufanya kuhusu haki za mtoto na watoto kwa jumla maeneo yao na majukumu yao katika shughuli wanazotakiwa kufanya.

“Mfano sheria hizo ni za Jiji, Manispaa na nyinginezo, kwa ufupi ni sheria ndogondogo za Serikali ya Mtaa ambazo zinaainisha mazingira ya kufanya shughuli na katika maeneo yapi.

“Watoto ambao wanajihusisha na matukio ya kuombaomba wapo wa aina tofauti, wapo ambao wanafanya hivyo wakitokea kwa wazazi wao, wengine wanatokea vituo vya kulea watoto wakitoroka na mazingira mengine…

MAMLAKA KUWAONDOA WATOTO MITAANI NI SAHIHI?
“Hivyo, kwa mujibu wa kanuni na sheria kadhaa kama nilivyofafanua ikiwemo sheria za majiji na halmashauri, hakuna kosa kuona mamlaka zinaenda kuwatoa watoto mtaani.

“Watoto wanapoenda kuombaomba mtaani inamaanisha kuwa wanakuwa wanakiuka sheria ndogondogo zilizoweka za kufanya shughuli katika maeneo ambayo hayatakiwi, pia kuombaomba siyo shughuli rasmi.

“Ukijumlisha vyote hivyo shughuli kutokuwa rasmi na haki za watoto inamaanisha kunakuwa na sheria za pande mbili zinavunjwa hapo.

KIDS.jpg

ADHABU KWA OMBAOMBA WATOTO
“Adhabu zipo, kwa kuwa kinachofanywa na mamlaka kipo ndani ya sheria inamaanisha kuwa watoto hao wanapofanya kazi ya kuombaomba wanaweza kuadhibiwa kwa faini au kifungo cha muda mfupi.

“Pamoja na hivyo mamlaka zimekuwa zikitumia busara kutowashitaki watoto, badala yake wanatafuta njia ya kuwarudisha kule walikotoka kama ni katika taasisi, walezi, mikoani au kutoka kwa wazazi.

“Lengo ni kuwafanya wale ambao wanakuwa na majukuu ya kuwasimamia watoto husika kutimiza majukumu yao kutimiza zile haki za mtoto ambazo zilizitaja juu.”

Picha: Muungwana, IPP


Nitarudi kufafanua kuhusu ombaomba watu wazima, kwa nini wanaondolewa, adhabu zao na nini kinachotakiwa kufanyia kuhusu wao na mamlaka.
 
Kuna dogo nishawahi kumuona ana omba kwenye magari hapo Ubungo, yule dogo namjua kwao, sio maisha mazuri sana lakini sio level ya kuomba, inaelekea alitoroka kwao kama ameenda kucheza kumbe janja janja.

Kwahiyo sio wote, ni wanauhitaji kuna wengine wanataka tu hela ambazo wazazi wao hawawapi lakini chakula na malazi yapo.

Pia, hawa watoto wasipowadhibiti, wakija kukua wakubwa, mahitaji yakiongezeka wataanza kupiga ngeta. Maana sahivi akipata elfu 2 inamtosha kula, lakini atakavoanza kuhitaji elfu 5 hadi 10 kwa siku, lazima waanze kuiba.
 
Back
Top Bottom