Watoto ni wageni katika ndoa yenu, hawana Mkataba na ninyi!

Robert Heriel Mtibeli

JF-Expert Member
Mar 24, 2018
21,339
51,864
WATOTO NI WAGENI KATIKA NDOA YENU; HAWANA MKATABA NA NINYI

Ni Yule Mtibeli, Robert HERIEL.

Hawakukuomba uwazae, hwakukuomba uwe Baba au mama Yao, hawakuomba lolote lile. Na kamwe hukujua Kama ungewazaa watoto wa namna hiyo, na hata wao hawakujua Kama wangezaliwa na mtu Kama wewe. Labda Kama ingekuwa uchaguzi wao wasingetaka wazaliwe na Mama au Baba Kama wewe. Tena hata wewe Kama ungeambiwa uchague watoto wa kuwazaa basi Baadhi ya watu wasingetaka kuzaa watoto kama walionao.
Anyway nayo ndio maisha.

Wapo watu wanachanganya madesa, hufikiri Wana Mkataba na mtoto au watoto wao.

Nataka kukuambia nature jinsi ilivyo haitambui mkataba wako na watoto wako, isipokuwa unatambua mkataba wako na mwenza wako.

Unapomuoa au kuolewa na mwenza uliyenaye lazima ujue huyo ndiye mwenzako, mshirika, Msaidizi, waubani, huyo ndiye msalaba wako, nawe ndiwe msalaba wake.

Huyo ndiye alikula kiapo kuwa mtakuwa pamoja siku zote za maisha yenu. Huyo ni Mume wako, huyo ni mke wako.
Siku hizi watu hawajui maana ya maneno hayo, Mke na Mume, wanafikiri ni Jambo la kawaida.
Lakini sivyo.

Mke ni zaidi ya rafiki, zaidi ya Mama kwani yeye ndiye aliyekula kiapo cha kuishi nawe na kufanya maisha pamoja.
Mume ni zaidi ya rafiki, zaidi ya Baba kwani ndiye aliyekula kiapo cha kuwa nawe siku zote za maisha yako.

Sio watoto wako wala wazazi wako waliokula kiapo kuwa nawe siku zote za maisha yako.

Msaidizi, mwili mmoja!

Baadhi ya watu hutengana na wenza wao kisa watoto, wakidhania kuwa hao ndio watu wao WA karibu.
Wengine hunyanyasa mpaka wake zao au waume zao kisa watoto.

Lakini wanashindwa kujua kuwa watoto ni wageni tuu katika maisha yenu ya ndoa.

Ipo siku watawaacha Kama ninyi mlivyowaacha wazazi wenu!

Sijasema muwatendee vibaya watoto wenu, wala sijasema muwatendee vibaya wazazi wenu. Ila najaribu kuwakumbusha kuwa Mkeo au mumeo ndio familia yako, ndio mwenza wako.

Huyo ndiye mliingia Mkataba mkawa washirika, huyo ndiye anajukumu la kukulinda, kukuangalia, kukutunza na kukupenda.

Hao wengine hamjawahi kukubaliana mahali popote pale, hata kisheria IPO hivyo. Nature pia ipo hivyo.

Ninaoushahidi wa kutosha katika Jambo hili. Watoto mamilioni duniani wamewatelekeza wazazi wao. Na kuwaacha solemba lakini kimsingi hawapaswi kulaumiwa, kwani nature ndivyo ilivyo,

Nature haiongopi!
Jambo lolote linalolazimishwa Kwa mtu ujue sio nature ya mtu huyo.
Jambo lolote linalosisitizwa Sana ujue sio nature ya watu hao, nature ipo automatically. Yaani unajikuta unafanya bila mtu kukuambia.

Nawatakia ijumaa kuu njema Wakristo wote!

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Dar es salaam
 
HEBU TUMIA KONDOM AFU UONE KAMA HAO WATOTO UNAOWAITA WAGENI WATAKUJA. 😂😂😂
WATOTO NI BARAKA, WATOTO NI ZAWADI.
 
Kuna wale wanaotudai urithi hadi kutishia uhai wetu

Hao tuwaitaje

Ni Haki Yao!

Uliwazaa wa nini sasa!

Au uliwazaa waje wateseke huku, hawakukuomba Ila uamuzi wako ndio uliwaleta.

Hakuna mzazi anayemuachia mtoto Urithi alafu mtoto asimpende!

Lakini tatizo wazazi wa siku hizi wengi wetu tunafikiri kuzaa tuu inatosha mwishowe na watoto wanafikiri kuzaliwa tuu inatosha kwani hata Sisi tutazaa tuu Kama wazazi wetu.

Lakini ukiacha Urithi mtoto anaona analodeni Kwa mzazi Kwa kumhangaikia

Mzazi asipoacha Urithi anakuwa Sawa na wanyama tuu ndio maana mnyama akishazaliwa akakua kila mmoja anapambana na maisha yake.

Kama nikuzaa Naye atazaa mbele Kwa mbele.
 
Sasa mbona na hawa wake zetu siku hizi Wanatutanguliza mbele ya haki au Mikataba feki?
 
Back
Top Bottom