Dejane
JF-Expert Member
- Jan 1, 2014
- 49,611
- 68,507
Habari zenu wakuu
Nina mtoto mchanga ana miezi miwili ana mwezi sasa hapati haja kubwa, nasubiria afikishe miezi mitatu aweze kupimwa x-ray inabidi apigwe bomba mara kwa mara, mwanzoni alikuwa anapata wakati anazaliwa, nyie sikieni tu nina mawazo sana.
Kumekuwa na wimbi sasa la watoto wachanga kuzaliwa wakiwa hawana sehemu ya haja kubwa pia watoto kushindwa kujisaidia inapelekea wanatobolewa tumbo ili uchafu uwe unapitia hapo na wakifikisha mwaka mmoja na nusu anafanyiwa upasuaji kutengenezewa sehemu ya haja, mwingine kafanyiwa upasuaji lakini tumbo limejaa ana miaka miwili, na hii nimeona hapo Bugando hospital.
Imekuwaje watoto sasa hivi wanazaliwa na shida sana, ina maana hawachunguzi nini kinasababisha. Watoto ni wengi wenye hio shida. Waziri afya yupo wapi na sioni hata ikizungumziwa?
Je, ni Mwanza tu au hata huko Dar na sehemu zingine hali ni hiyo? Au nyie salama?