Watoto kuzaliwa hawana sehemu ya haja kubwa

Dejane

JF-Expert Member
Jan 1, 2014
49,617
68,528
Habari zenu wakuu

Nina mtoto mchanga ana miezi miwili ana mwezi sasa hapati haja kubwa, nasubiria afikishe miezi mitatu aweze kupimwa x-ray inabidi apigwe bomba mara kwa mara, mwanzoni alikuwa anapata wakati anazaliwa, nyie sikieni tu nina mawazo sana.

Kumekuwa na wimbi sasa la watoto wachanga kuzaliwa wakiwa hawana sehemu ya haja kubwa pia watoto kushindwa kujisaidia inapelekea wanatobolewa tumbo ili uchafu uwe unapitia hapo na wakifikisha mwaka mmoja na nusu anafanyiwa upasuaji kutengenezewa sehemu ya haja, mwingine kafanyiwa upasuaji lakini tumbo limejaa ana miaka miwili, na hii nimeona hapo Bugando hospital.

Imekuwaje watoto sasa hivi wanazaliwa na shida sana, ina maana hawachunguzi nini kinasababisha. Watoto ni wengi wenye hio shida. Waziri afya yupo wapi na sioni hata ikizungumziwa?

Je, ni Mwanza tu au hata huko Dar na sehemu zingine hali ni hiyo? Au nyie salama?
 
Ni tatizo lipo na lipo la aina tofauti tofauti, pia si kwa haja kubwa tu bali hata njia ya haja ndogo kwa watoto wa kiume 'Hypospadias'

1. Kuna watoto huzaliwa bila kuwa na tundu la njia ya haja kubwa 'anus'

2. Kuna watoto ambao huzaliwa tundu la haja kubwa likiwa sehemu isiyo sahihi

3. Kuna ambao huzaliwa njia ya haja kubwa imeungana na njia ya mkojo au uke, hii wengi huijua kama fistula

Uzuri ni kwamba hali zote zinarekebishika kwa ama procedure moja hadi tatu, itategemea na ukubwa wa tatizo...
 
Atresia ani...ni congenital anomaly hakuna cha uchawi, na kama hana kabisa hicho alichokuwa anatoa awali kilikuwa kinapitia wapi? na wanapompiga bomba uchafu unapitia wapi?
 
Hizi cases zimekuwa nyingi.

Mwezi uliopita kuna mtoto alizaliwa pasipo na tundu la haja kubwa halafu akanywa maji wakati wa kuzaliwa,aka-survive "masaa" sita hivi akafariki.

Ni Kanda za ziwa hiyohiyo.

Mama ana watoto 4 na huu ni uzazi wa kwanza baada ya kuanza kutumia njia ya uzazi wa mpango.

So ni kama wameshahitimisha chanzo kuwa ni hizo hormonal contraceptives.
 
Pole dear!
Kama wanaweza mfanyia operation hapo baadae na akakaa sawa basi uwe na subra
Kikubwa punguza mawazo ili umlee mtoto vizuri awe na afya njema!
Mungu akutie nguvu,

Asante sana
 
Kazi kweli lakin watoto wengi wanazaliwa wa shida na wengi wanapoteza maisha
 
Back
Top Bottom