Watoto kuzaliwa hawana sehemu ya haja kubwa

Dem wangu Diana aliwai kupata mtot wa namna hyo ila hajawa riziki

Pole Sana mkuu ila pia usiwapuuze kina mwamposa narudia usiwapuuze kina mwamposa na wengine
Pole sana naamin atapona tu
 
Pole sana na hongera kwa mtoto ila nna swali kwanini unasubiria miezi mitatu? Au ni mimi tu nnae panic saivi?
 
Ni tatizo lipo na lipo la aina tofauti tofauti, pia si kwa haja kubwa tu bali hata njia ya haja ndogo kwa watoto wa kiume 'Hypospadias'

1. Kuna watoto huzaliwa bila kuwa na tundu la njia ya haja kubwa 'anus'

2. Kuna watoto ambao huzaliwa tundu la haja kubwa likiwa sehemu isiyo sahihi

3. Kuna ambao huzaliwa njia ya haja kubwa imeungana na njia ya mkojo au uke, hii wengi huijua kama fistula

Uzuri ni kwamba hali zote zinarekebishika kwa ama procedure moja hadi tatu, itategemea na ukubwa wa tatizo...

Ahsante mkuu kama kawaida hua hauachi kuelimisha jamii.

Sasa kama anavyouliza Dinazarde , chanzo Cha ongezeko la hii Hali siku za hivi karibuni ni Nini?

Ahsante
 
Pole Sana, Hilo jambo ni la kawaida, Cha msingi ni kusikiliza tu madaktari wanasema nini Kwa Sasa. Mimi nilikuwa na mtoto Hana sehemu ya uke, pameziba kabisa. Baada ya miez 2 tukaenda hospitali, wakamtoboa Ili paonekane, tushukuru ndani kulikuwa wazi sema Kwa nje ndiyo paliziba. Walivyomtoboa akawa sawa Mpk Sasa ana miaka 8
 
Ahsante mkuu kama kawaida hua hauachi kuelimisha jamii.

Sasa kama anavyouliza Dinazarde , chanzo Cha ongezeko la hii Hali siku za hivi karibuni ni Nini?

Ahsante

Imperforate anus ni tatizo ambalo wataalamu wanaliita congenital (yaani ni hali ya kuzaliwa nayo)...

Kwa mantiki hiyo ni ngumu kung'amua chanzo cha ongezeko hadi labda utafiti ufanywe na taasisi za udhibiti wa magonjwa...

Uzuri ni kwamba ni tatizo linalorekebishika, na maisha yanasonga...
 
Leo amepata haja mwenyewe nimefurahi sana
 
Pole Sana, Hilo jambo ni la kawaida, Cha msingi ni kusikiliza tu madaktari wanasema nini Kwa Sasa. Mimi nilikuwa na mtoto Hana sehemu ya uke, pameziba kabisa. Baada ya miez 2 tukaenda hospitali, wakamtoboa Ili paonekane, tushukuru ndani kulikuwa wazi sema Kwa nje ndiyo paliziba. Walivyomtoboa akawa sawa Mpk Sasa ana miaka 8

Tumesikiliza kweli tulikuwa tunarudishwa tu kwamba tumpe muda mtoto,kweli leo kajisaidia mwenyewe namshukuru Mola
 
Ahsante mkuu kama kawaida hua hauachi kuelimisha jamii.

Sasa kama anavyouliza Dinazarde , chanzo Cha ongezeko la hii Hali siku za hivi karibuni ni Nini?

Ahsante
Hii mada nimeiona baada ya huo ugonjwa kubisha hodi kwenye Maisha yangu...binti yangu kazaliwa na tatizo Hilo wapo muhimbili wamelazwa mpaka jumatano... kiukweli ata sielewi na kila mtu wa karibu yangu ni mgeni wa tatizo Hilo... mpaka wazazi wetu wa pande mbili hakuna aliewah kuona
 
Chunguza hapo hospital hao watoto wapo kibao wenye matatizo hayo
 
Habari zenu wakuu

Nina mtoto mchanga ana miezi miwili ana mwezi sasa hapati haja kubwa, nasubiria afikishe miezi mitatu aweze kupimwa x-ray inabidi apigwe bomba mara kwa mara, mwanzoni alikuwa anapata wakati anazaliwa, nyie sikieni tu nina mawazo sana.

Kumekuwa na wimbi sasa la watoto wachanga kuzaliwa wakiwa hawana sehemu ya haja kubwa pia watoto kushindwa kujisaidia inapelekea wanatobolewa tumbo ili uchafu uwe unapitia hapo na wakifikisha mwaka mmoja na nusu anafanyiwa upasuaji kutengenezewa sehemu ya haja, mwingine kafanyiwa upasuaji lakini tumbo limejaa ana miaka miwili, na hii nimeona hapo Bugando hospital.

Imekuwaje watoto sasa hivi wanazaliwa na shida sana, ina maana hawachunguzi nini kinasababisha. Watoto ni wengi wenye hio shida. Waziri afya yupo wapi na sioni hata ikizungumziwa?

Je, ni Mwanza tu au hata huko Dar na sehemu zingine hali ni hiyo? Au nyie salama?

Kwa watoto wa kiume vipi?
 
Back
Top Bottom