Ni muhimu sana kuzingatia uzazi wa mpango siku hizi kwani kutokana na kuporomoka kwa maadili, baadhi ya watoto wamekuwa ni mizigo badala ya hazina katika familia.
Watoto hawawezi kuwa tofauti sana na wazazi wao yaani baba na mama. Mchongoma hauwezi kuzaa machungwa na mtoto wa simba si wa chura.
Mtoto aliyetoka kwenye damu ya 'viroba' hawezi kuwa sawa na mtoto wa baba aliyekunywa mbege!!
Kuna wimbo unauliza mdudu ndani koko la embe kaingiaje? Ni wazi mdudu huyo huingia na kuanza kuharibu tunda hilo likiwa katika hatua ya maua. Na mdudu huyo hulifanya embe lioze.
Wanasema mtoto umleavyo ndivyo akuavyo. Kama mtoto amedekezwa tangu mdogo atakuwa na tabia mbaya hadi akiwa mkubwa.
Mzazi akiwa mvivu na mtoto atakuwa mvivu tu. Mzazi akiwa na tabia ya kutoa matusi mtoto ataiga.
Wazazi wanakosea sana kufanya mambo ya ovyo mbele ya watoto. Kwa mfano baba kumtukana mkewe au mke kumjibu vibaya baba mbele ya watoto hupanda mbegu mbaya.
Na mzazi akizoea kuvaa mavazi yasiyoendana na maadili it's likely mtoto naye atakuwa akivaa nguo za ajabu ajabu.
Baba ukiwa unavaa mavazi au vitu vya kike mtoto wako wa kiume ataiga tu!
Watoto wengi siku hizi hawana adabu kwa sababu walidekezwa sana na wazazi wao.
Akiitwa na baba au mama yake anavuta mdomo kisa anachatii. Kutwa kwenye tv na kazi hawataki kufanya. Akina mama wengi siku hizi kazi zote wanawaachia house girls.
Matokeo yake ni kwamba watoto hawawezi hata kuosha vyombo, kufagia, kupika au hata kufua nguo zao. Ukweli ni kwamba Watanzania wengi wameanza ku lose control ya watoto wao. Malezi imekuwa kazi ngumu.
Katika baadhi ya familia watoto ndio wanawa control wazazi kwa kufanya wanavyotaka almost with impunity!!
Hakuna kazi wanayofanya watoto wengi siku hizi zaidi ya kuchati kwenye simu na ku bet.
Wazazi wengi wanawalea watoto kama mayai na hawawafundishi stadi za maisha. Inakuwaje mtoto binti wa miaka 15 ashindwe kufua nguo zake au kijana wa miaka 17 ashindwe hata kufyeka majani au kulisha mifugo?
Baadhi ya watoto hasa wavivu na wasio na heshima ni mizigo kwa wazazi wao, jamii na taifa kwa ujumla.
Wengi wanasingizia kuwa busy na masomo lakini hii si kweli kwani wanafunzi wengi hawazingatii shule na ikifika wakati wa mitihani baadhi ya wazazi wao huhangaika 'kununua' mitihani.
Wazazi wanachangia nchi kutengeneza kizazi cha watu wanaotaka njia za mkato kimaisha. Wazazi waongeze ukali kidogo kwa watoto wao vinginevyo wanawapoteza.
Wawafundishe kufanya kazi, mila na desturi nzuri, adabu kwa wakubwa na upendo kwa binadamu wote.
Watoto wapunguze kuchati kwenye simu na ikiwezekana wazazi msiwanunulie vijana wenu cm. Wengi wanaangalia mambo ya ovyo yanayozidi kuwapumbaza.
Cm na mitandao inaharibu vijana wetu na wazazi tusipoziba ufa.........