MADA: Tatizo la Watoto kuchelewa kuongea. Ni kipi chanzo chake? Je, nawezaje kutatua tatizo hili?

Asanten sana wadau maana hata mimi wangu naona manenno mengi hatamki, na ana 1.8year.
ila anaelewa kila kitu.anajua dada, mama,baba, kaka, sante, na mengine machache tu mojamoja tu.

Usiwe na haraka, ataongea bado mdogo, mtoto sasa ana miaka 2.5 ndio ameanza kuiga na kukamata neno.

Hapo awali alikuwa anajua maneno na2 tu,mama na hii hapa, anafahamu unacho mwambia, ipe muda mtoto, na akiongea hata kama hufahamu muitikie, akikuita itika, ongea nae kama unamfahamu, utampa mtoto confidence.
 
Habari wana JF,naombeni msaada na ushauri wenu Tafadhali.mwanangu ana umri wa miaka mitatu na miezi miwili sasa,lakini hadi sasa bado hawezi kuongea.

Zaidi anajua kuita mama,baba na Mara chache sana nimemsikia akitamka Dada na kaka.ila Neno mama ndio limemkaa mdomoni.

Je tatizo linaweza kuwa nini,au nifanyeje mwanangu apate kuongea kama watoto wengine wenye umri wake.

nimempeleka hospital madaktari wamesema hana tatizo,nimempeleka kwenye Maombi lakini bado.

Nisaidieni ushauri tafadhali ndugu zangu.
 
Achana na michepuko yako chap ataanza kuongea au angalia vzur mwenendo wa mkeo
 
Mtafutie hii kitu...mpatie asubuhi mchana na jioni.
13234884051988079243joint-hi.png
 
Kila mtoto anapitia stage tofauti za kukua kwa wakati wake. Kuna watoto wanaanza kuongea baada ya umri wa miaka 5. Ushauri wa haraka, zima TV huko nyumbani kwako.

Yaani angalieni news tu jioni. Kusudi mtoto aongee Na mlezi wake. Pili, nianzishe nursery school. Huko atafunzwa kuongea hadi maneno usiyotaka ayajue.
 
Kila mtoto anapitia stage tofauti za kukua kwa wakati wake. Kuna watoto wanaanza kuongea baada ya umri wa miaka 5. Ushauri wa haraka, zima TV huko nyumbani kwako. Yaani angalieni news tu jioni. Kusudi mtoto aongee Na mlezi wake. Pili, nianzishe nursery school. Huko atafunzwa kuongea hadi maneno usiyotaka ayajue.
Asante kwa ushauri
 
Jaribu pia kimchunguza anasikia? anakijua jina lake? anaweza ku-respond instructions ndogondogo? Hii husaidia kujua kama hana tatizo lolote la ukuaji. Halafu kama unamashaka mpeleke kwa Daktari wa watoto (pediatrician). Sio kila Daktari anafahamu kuhusu ukuaji wa mtoto.

Jingine kwenu familia/ ukoo wenu kuna wenye vigugumizi?? Nimeona watoto wenye asili ya vigugumizi walivyochelewa kuongea
Ndio anasikia,ukimtuma niletee kitu Fulani analeta,na jina lake analijua,ukimuita anakuja.
Pia nilishampeleka hadi kwa dactari wa watoto nae baada ya kumchunguza akasema hana tatizo.

Ktk ndugu nnao wajua hakuna Mwenye kigugumizi na nimejaribu kuuliza kwa bibi na babu.sasa sijui hili nashindwa kulisemea zaidi
 
Usiijalifanu88attament18011399, member: 375372"]Picha haijafungua ndugu.[/QUOTE]
Usiijali hiyo attament. Huyo mjinga kaweka picha ya bangi
 
Hili tatizo nimeliona sana katika familia za watu wa kipato cha kati, ninamaanisha wale wa nyumba za gate, watoto wanaachwa na house girl ikiwezekana wawili, mdada wa kukaa na watoto na mdada wa kufanya shughuli za ndani.

Watoto hawa wanatengwa wasicheze na watoto wenzao, wasifundishwe tabia mbaya, watoto hawa wazazi wanawaacha asubuhi na wanarudi usiku. Mdada aliyeachiwa watoto yuko busy kuangalia bongo movie na tamthilia.

Mtoto unakuta anafikisha miaka miwili na nusu hajaweza kuunganisha maneno mawili bado anaongea neon moja, pia unakuta mtoto wa miaka miwili na nusu bado anajisaidia kwenye pampers na wazazi bado wanaona ni kawaida.

Watoto wa Uswazi kwasababu ya kucheza pamoja, (hii haepukiki kwa kuwa wote wanaishi nyumba moja ya vyumba sita na mabanda ya uani) huanza kucheza pamoja pale wanapoanza kutambaa, kwakweli inawasaidia sana watoto kujenga social skills, kushare toys, kubuild self defence na pia kujenga upendo.
 
Hii imenikuta kwa mtoto wangu , Mpaka amaefikisha miaka miwili na nusu alikuwa hajui kuongea vizuri nikashindwa kumpeleka shule.

Baadae ikabidi nimtoe nyumbani kwangu nimpeleke kwa shangazi yangu kwake ana wajukuu wengi japo napo ni gate kali ila watoto wapo wengi.

Alipokaa pale kwa muda wa mwezi mmoja na nusu tu nikaanza kuona changes hata nikiongea naye kwenye simu anaongea kitu kinachoeleweka. nilimuacha kwa miezi mitano kisha nikamchukua sasa hivi nikirudii kazini huwa ananisimulia kila kitu hata kama dada wa kazi alimchapa anasema tumrudishie.

Naunga mkono hoja ila sishauri kuruhusu watoto wakacheze na hawa wenzao wa uswahilini kwa sababu wanatabia za hovyo sana sijui huwa wanafundishwa na wazazi wao au huwa wanaiga tu bila kujua kuwa hili ni baya.
 
Dadangu haya mambo ni magumu..
Nafikiri inabidi kuwe na checks and balances.

Nyie wanawake ndio wa kwanza kulete kwere za kufungia watoto ndani ka wanaatamia mayai. Nimeliona hilimsehemu nyingi hata kwetu.
Dadangu huwa yuko sensirive ana litoto my nephew lina 7 years limezubaa ka msukuma wa geita.

Shemeji yangu I mean mme wake anambwambiaga mwache dogo aende kitaa amingle na watoto wenzie acheze maringi,acheze chandimu..aka mpira wetu wa kitaa etc..
Ila my sisy...namjua vizuri...atalialia,atacomplain mpaka mzee anakuwa mpole..
But inakera..

Na maeneo wanayoishi sio mabaya sana..ni Tegeta karibu na bunju..some kind of suburban lifestyles..
 
Hii imenikuta kwa mtoto wangu , Mpaka amaefikisha miaka miwili na nusu alikuwa hajui kuongea vizuri nikashindwa kumpeleka shule.

Baadae ikabidi nimtoe nyumbani kwangu nimpeleke kwa shangazi yangu kwake ana wajukuu wengi japo napo ni gate kali ila watoto wapo wengi.

Alipokaa pale kwa muda wa mwezi mmoja na nusu tu nikaanza kuona changes hata nikiongea naye kwenye simu anaongea kitu kinachoeleweka. nilimuacha kwa miezi mitano kisha nikamchukua sasa hivi nikirudii kazini huwa ananisimulia kila kitu hata kama dada wa kazi alimchapa anasema tumrudishie.

Naunga mkono hoja ila sishauri kuruhusu watoto wakacheze na hawa wenzao wa uswahilini kwa sababu wanatabia za hovyo sana sijui huwa wanafundishwa na wazazi wao au huwa wanaiga tu bila kujua kuwa hili ni baya.
Ubaguzi wa kijinga
 
Yeah, umeongea kitu kinataka kufanana na ukweli, ila tafiti zaidi inahitajika, haya mambo ya kisayansi huwezi kuyatolea conclusion kirahisi namna hiyo, tafiti zifanyike, ni eneo zuri la kufanya tafiti
 
Sijafanya utafiti kwakweli na wala siwezi ku quantify hii kitu lakini ni kutokana na experience nilizokutana nazo na ndiyo maana nimeona tulijadili hapa, wataalamu wanaweza kulipeleka mbele Zaidi.
 
Dadangu haya mambo ni magumu..
Nafikiri inabidi kuwe na checks and balances..
Nyie wanawake ndio wa kwanza kulete kwere za kufungia watoto ndani ka wanaatamia mayai..
Nimeliona hilimsehemu nyingi hata kwetu..
Dadangu huwa yuko sensirive ana litoto my nephew lina 7 years limezubaa ka msukuma wa geita..
Shemeji yangu I mean mme wake anambwambiaga mwache dogo aende kitaa amingle na watoto wenzie acheze?maringi,acheze chandimu..aka mpira wetu wa kitaa etc..
Ila my sisy...namjua vizuri...atalialia,atacomplain mpaka mzee anakuwa mpole..
But inakera..
Na maeneo wanayoishi sio mabaya sana..ni Tegeta karibu na bunju..some kind of suburban lifestyles..
Matatizo ya hizo shule za English medium wanakutana watoto wanaotoka katika maisha flani, ule msuba wa kusugua akili kuteneza mpira wa makaratasi mcheze hawaujui, wanaongelea computer games.

Tatizo linguine ni jiji kukosa viwanja vya michezo kwa watoto maeneo ya makazi ya watu, kama kungekuwa na viwanja vizuri ambavyo watoto wanakutana na wazazi wanakuwa karibu kuwaangalia ni muhimu.

Kwa kweli si mlaumu sana dada yako, dunia imeharibika sana, watoto wanafundishwa kuvuta bangi wakiwa wadogo, lakini pia katika maisha kuna risk unazokumbana nazo. Fikiria huyo mtoto wa dada yako anaweza kwenda kusoma boarding school akimaliza darasa la saba?
 
Back
Top Bottom