Watoto kuanikwa juani muda wote huo ni halali? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Watoto kuanikwa juani muda wote huo ni halali?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Nyati, Oct 14, 2010.

 1. Nyati

  Nyati JF-Expert Member

  #1
  Oct 14, 2010
  Joined: Mar 6, 2009
  Messages: 2,044
  Likes Received: 383
  Trophy Points: 180
  Wadau,

  Leo nimeshuhudia watoto wakishiriki ktk maadhimisho ya Siku ya Mwl. Nyerere na kuhitimisha mbio za mwenge katika kile kilichoitwa harahiki kule Kigoma. Mimi sipingi hizi harahiki bali watoto wale wamechoshwa sana katika mazingira magumu ya vumbi wakati ni watoto wadogo.

  Wamekaa juani karibia masaa matano bila sababu yeyote ile ya msingi. Kwanza kabla ya Raisi hajafika wamekaa pale karibia masaa matatu. Wakati huu tayari wengine walishaanza kusinzia sinzia na kuamshwa kwa makwenzi. Baada ya Rais ya kufika mambo mengine yakaendelea na baadaye wakaanza hiyo harahiki ambayo nayo imechukua muda mrefu wakipiga kwata bila kupumzishwa kama masaa mawili hivi bila kupumzika.

  Hivi Wizara ya akina mama na watoto inatoa mwongozo gani juu ya jambo hili??. Kweli ni haki kwa watoto kupigishwa kwata kwa muda wote huo tena katika vumbi??

  Je Mwl. angekuwepo angefurahia hali hii? Ni wakati muhafaka wa kufuata haki za watoto badala ya kuwatumia isivyohalali kama ilivyofanyika leo. Kwa wale mlioshuhudia mtakubaliana nami katika hili kwani hakukuwa na haja ya kuwaweka katikati ya uwanja katika vumbi muda wote huo. Wangewekwa jukwaani kama washiriki wengine na wakaitwa uwanjani wakati wa harahiki hiyo na vile vile wafanye kwa muda mfupi siyo kama leo.

  Huu ni mtizamo wangu
   
 2. pmwasyoke

  pmwasyoke JF-Expert Member

  #2
  Oct 15, 2010
  Joined: May 27, 2010
  Messages: 3,584
  Likes Received: 189
  Trophy Points: 160
  Sijui kwa nini wasiwatumie maaskari kwa shughuli hizo!
   
 3. j

  jumalesso Member

  #3
  Oct 15, 2010
  Joined: Jul 5, 2008
  Messages: 84
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mtizamo wako Nyati ni sahihi kabisa. Haistahili kuwashirikisha watoto kwenye program kama hizo wakati vikosi vya Ulinzi vipo sidhani kama watoto wa Waheshimiwa walikuwepo hapo!. Hii inaonesha ni jinsi gani tusipojali malezi bora ya watoto na pengine wameshinda hapo hata maji wakasahauliwa! Wizara stahiki inatakiwa iyatupie macho mambo kama haya
   
 4. P

  Preacher JF-Expert Member

  #4
  Oct 15, 2010
  Joined: Aug 25, 2008
  Messages: 328
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Ni mambo mengi sana yanaumiza katika nchi yetu ya Tanzania - halafu eti KIONGOZI - anayesubiriwa akifika hapo anaanza HOTUBA ZA KISIASA - HUKU ANACHEKACHEKA - HIVI KWELI MTOTO WAKE ANGEKUWA KATIKA LILE JUA/VUMBI ANGEJISIKIAJE????? yote hiyo kufanikisha AZIMA AMBAZO HAZIMSAIDII MTANZANIA - KUMUENZI HAYATI MWALIMU NI SAWA LAKINI KUNA NJIA NYINGINE NYINGI SANA ZA KUMUENZI - KULIKO KUWEKA WATOTO WADOGO JUANI - NADHANI NEXT TIME - MAWAZIRI/WABUNGE/VIONGOZI - WASIMAME JUANI KUSIKILIZA HOTUBA - MBONA WANAKAA JUKWAANI NA KUJIKINGA NA JUA??? UKATILI MTUPU ............ LAITI WANGEKUWA GREAT THINKERS - WASINGEFANYA MAMBO KAMA HAYO................... POLENI SANA WATOTO - MUNGU AWAPE KUKUA SALAMA PAMOJA NA MAZINGIRA MAGUMU MNAYOISHI!!
   
 5. Nyati

  Nyati JF-Expert Member

  #5
  Oct 15, 2010
  Joined: Mar 6, 2009
  Messages: 2,044
  Likes Received: 383
  Trophy Points: 180
  Juma Leso Mimi hapa napinga nawe kuwatumia watoto ni sawa kabisa hata mimi enzi zangu nilishiriki na nilipenda sana kitu hiki. Hii inaongeza hali ya utaifa na kumbu kumbu yao pia. Lakini napinga kuwekwa juani wakati wote wakati wasanii walikaa jukwaani na kuitwa wakati wa program yao. Na watoto wafanyiwe hivyo hivyo. Si kuwaweka juani. Nina hakika hata mvua ingenyesha wangeambiwa waendelee kukaa pale.
   
 6. T

  Teko JF-Expert Member

  #6
  Oct 15, 2010
  Joined: Jul 3, 2010
  Messages: 216
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 35
  Mimi pia nililiona hilo na ilinuimiza sana kuona watoto wamewekwa juani muda mrefu na kisha kupigishwa kwata kwa muda mrefu!
   
 7. Papa Mopao

  Papa Mopao JF-Expert Member

  #7
  Oct 15, 2010
  Joined: Oct 7, 2009
  Messages: 3,355
  Likes Received: 387
  Trophy Points: 180
  Kuna mmoja jana alilala pale uwanjani, aisee iliniuma sana nilitamani nimuamshe nimwambie atoke hapo kakapumzike nyumbani!!
   
 8. S

  SNAKE HOUSE Member

  #8
  Oct 16, 2010
  Joined: Oct 4, 2010
  Messages: 62
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ktk hili kuna haja ya kila mmoja wetu kuhoji uzalendo wake kwa nchi yake !!!!!!
  Kinachotetewa hapa ni uselule tu .....
  1) Nchi hailindwi vivulini wakuu.. Bali kwenye matope,mvua,njaa,juani,wanyama wakali,mambo kama hayo.
  Ni agharabu mtu kujipatia Kipato chake kivulini !
  2) Miongoni mwa hao waliokaa juani,walikuwepo Marais,wawaziri,wabunge,madiwani,
  madaktari,wakuu wa majeshi,wamachinga,wafanyakazi,wakulima....unaweza kujaza !! wa kesho ! HIVI ISUBIRIWE MPAKA LINI KUANZA KUWAKUNJA SAMAKI WALE WABICHI ??????
  Isitoshe kwa mujibu wa mira na desturi za Kitanzania, hiki ni kipindi muafaka kwao,pamoja na masuala ya jando na unyago..... kuwawekea misingi imara ili kujenga,
  taifa kakamavu linalowajibika,ambalo halingoji KEA Mwenye gobole kulilinda,au halikai kivulini kusubiri misaaada,au lifanyiwe mambo !!!
  Zama kwenye kumbukumbu zako ,hata Rais naye alicheza halaiki,alikula ngalambe pale JKT,
  na kuendelea ..... Mazingira yaliyomkita pale kileleni kama kiongozi Bora na Mzalendo namba moja kwa nchi yake !!!!!
  Haina kulia.... hata nyerere angeunguruma kwa uchungu akipinga hoja yenu chovu.
  Maana hata yeye alichegama katika mambo hayo ya halaiki halaiki na ujeshi jeshi.
  3) Shule si tu kujifunza kujumlisha,bali hata kujifunza jinsi ya kuishi,uzalendo,kuwajibika,uvumilivu ni sehemu ya mafunzo murua ya shule !!!!!!!
  KUWAJENGA WATOTO SAS HIVI NI KUJENGA TAIFA LENYE NIDHAMU LINALOSONGA MBELE.
  4) Ni vitamini gani inapatikana juani ???? Jua haliuuuiiii wakuu
   
 9. Kibunango

  Kibunango JF-Expert Member

  #9
  Oct 16, 2010
  Joined: Aug 29, 2006
  Messages: 7,639
  Likes Received: 185
  Trophy Points: 160
  Lol... Lazima hapo umeongeza chumvi...
   
 10. Nyange

  Nyange JF-Expert Member

  #10
  Oct 16, 2010
  Joined: Mar 25, 2010
  Messages: 2,180
  Likes Received: 229
  Trophy Points: 160
  Ndo sera zilizo tuletea mtindio wa ubongo. wanatuwahi tukiwa chipukizi
   
Loading...