Watoto hawa wana kosa mpaka wasistahili matunzo toka kwa baba zao!?

BAK

JF-Expert Member
Feb 11, 2007
124,790
288,006
Watoto wa nje ya ndoa hawana haki kisheria
Imeandikwa na Basil Msongo, Dodoma; Tarehe: 29th January 2010
Habari Leo

HAKUNA sheria inayotoa haki kwa watoto wanaozaliwa nje ya ndoa, Bunge limeelezwa leo.

Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Frederick Werema, amekiri bungeni kuwa ni kweli watoto wanaozaliwa nje ya ndoa wanapata matatizo mengi hasa yanayohusiana na mirathi.

Werema amewataka wananchi wafahamu athari za matendo yao ya zinaa na wazingatie maadili ya kitanzania.

Mwanasheria Mkuu wa Serikali ameyasema hayo bungeni mjini Dodoma, wakati anajibu swali la nyongeza la Mbunge wa Viti Maalum, Diana Chilolo na swali la msingi la Mbunge wa Viti Maalum, Dk Getrude Lwakatare.

Chilolo aliiuliza Serikali kuwa inawasaidiaje watoto wanaozaliwa nje ya ndoa ambao mama zao huwaficha kutokana na sababu mbalimbali ikiwa ni pamoja na wanaume kuzuia wasitajwe ili kukwepa aibu.

"Zipo baadhi ya mila na Desturi huruhusu watoto wanaozaliwa nje ya ndoa kurithi pale watoto hao wanapokuwa wametambuliwa rasmi katika familia na wazazi wao kabla hawajafariki dunia" amesema Werema wakati anajibu swali la Dk Lwakatare.

"Changamoto hii ni miongoni mwa hoja ambazo zimeifanya Serikali itake kutunga sheria ya mirathi ambayo itashughulikia pamoja na masuala mengine, watoto wanaozaliwa nje ya ndoa" amesema Werema.

Kwa mujibu wa Werema, Sheria ya Mtoto Namba 21 ya mwaka 2009 iliyopitishwa bungeni Novemba mwaka jana ni chanzo cha kutambua haki za watoto wakiwemo waliozaliwa nje ya ndoa.
 
Viongozi wenyewe, mawaziri wabunge na hata huyu rais wetu Kikwete ndio wanaoongoza kwa kuwa na watoto nje ya ndoa, kwa hiyo sishangai wakijishaua na kukataa.

Hivi kama serikali haina dini "zinaa" ni nini? Maadili ya Kitanzania ni nini?

Huu ni wakati wa kuachia ma DNA yafanye kazi, sio kubabaisha kwa propaganda.
 
Viongozi wenyewe, mawaziri wabunge na hata huyu rais wetu Kikwete ndio wanaoongoza kwa kuwa na watoto nje ya ndoa, kwa hiyo sishangai wakijishaua na kukataa.

Hivi kama serikali haina dini "zinaa" ni nini? Maadili ya Kitanzania ni nini?

Huu ni wakati wa kuachia ma DNA yafanye kazi, sio kubabaisha kwa propaganda.

Nchi za wenzetu ndivyo wanavyofanya hivi. DNA ikirudisha jibu kwamba wewe ni baba wa mtoto basi sheria zinakushika ili umpatie matunzo mazuri mtoto huyo na wakati mwingine hata muajiri wako hushurtishwa na mkono wa sheria kukata mshahara wako moja kwa moja na kumpatia mama au mtu anayemtunza huyo mtoto. Kwa kuwa Tanzania sasa huu utaalamu wa kutumia DNA sioni sababu zozote za msingi za Wanaume kukwepa majukumu yao muhimu ya kuwatunza watoto wao waliopatikana nje ya ndoa.
 
Back
Top Bottom