Papaa Muu
JF-Expert Member
- Nov 6, 2018
- 243
- 292
Madaktari bingwa wa magonjwa ya moyo kwa watoto wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) na wenzao kutoka King Salman Humanitarian Aid and Relief Center wa nchini Saud Arabia wakimfanyia upasuaji wa bila kufungua kifua na kuziba tundu la moyo wa mtoto kwa kutumia mtambo wa Cathlab wakati wa kambi maalum ya matibabu inayofanyika katika Taasisi hiyo. Jumla ya watoto 33 wamefanyiwa upasuaji mdogo wa bila kufungua kifua ambapo hali zao zinaendelea vizuri na wengine wameruhusiwa kurudi nyumbani.