Mugishagwe
JF-Expert Member
- Apr 28, 2006
- 300
- 58
Nakuja na habari hii ambayo inasikitisha sana lakini chanzo chake ni uongozi mbaya na rushwa kutawala Musoma na kulindana kuanzia Mkoani hadi Wizarani.
Ndugu zangu, nimekuwa katika hospitali hii kwa muda wa wiki moja sasa, nimekuwa nashuhudia watoto wanakufa kwa wingi, ama wakiwa mapokezi ama wodini, kwa idadi ya wastani ya watoto 5 na watu wazima 4. Leo pekee nimeshuhudia Mwalimu mmoja wa shule moja hapa Musoma anakufa, na maiti yake kubebwa na ndugu zake kupelekwa Mortuary, na wagonjwa wengine ambao sikupata taarifa zao.
Hospitali ya Mkoa wa Mara inaongoza kwa rushwa na uongozi mbovu ambao unakumbatiwa na Mkubwa mmoja Wizarani na Acting Katibu Tawala wa Mkoa huu anaitwa Mulemwa. Inasemekana kuna Dkt. Muniko ambaye yeye ameshindikana kuondoka, na yeye ni Mganga mfawidhi hapa. Rushwa kwake ni sehemu ya maisha yake, na huhamishia madawa katika hospitali iliyopo Mtaa wa Iringo hapa Musoma iitwayo Manga.
Huhamisha wagonjwa na kuwapeleka kwake kwa consultation pekee ni Tshs 5000 na huu ni mradi wake. Mganga Mkuu ndugu Bangi yupo tu, na inasemekana naungana na wenyeji kula mlungula bila ya wasiwasi. Nimeshuhudia matukio madhaa ambayo hata Nurse alifikia kutamka kwamba wao ma Nurse na ma daktari wao siri ni moja na hakuna wa kuwafanya lolote.
PCCB ya Hosea hapa Musoma ina ubia na hawa wakubwa, hakuna lolote wafanyalo maana wao huingia hapo na kulambishwa.
Kuna mengi ya kueleza hapa, lakini baada ya hapa juu nadhani kama kuna mtu ana access na Wizara ya Afya, basi anitafute chemba anipe info zaidi ili niende Dar kuelezea hali ilivyo, maana hata mimi nimeombwa rushwa kwa uwazi, ikabidi nimwite Mganga Mkuu na kumuuliza uhalali ule. Hakuna risiti baada ya malipo, na pia kila Nurse huomba rushwa wazi wazi, maana wanajua ubaya wa Uongozi, kwa kuwa wote wanakula na hakuna wa kumfukuza mwenzake. Vifo Musoma vinatawala, maana kama huna pesa kwanza, basi utawekwa hadi pesa ije. Hata kupata shule inakubidi kulipa 2000 na kusukuma mgonjwa pia malipo achilia mbali adha za ndani ya wodi.
Wenyeji wanasema kwamba ukitaka kuijua Musoma, fika Wodi ya watoto na namba 6 huko, utajua taabu zaidi.
Nimechukua hatua. Je, nianzie wapi, maana Wizarani Dkt. Muniko ana mtu wake na kuondoka Musoma imekuwa ngoma. Watu wanakueleza kwamba Muniko na Meneja wa Uwanja wa Karume hapa Musoma hawawezi kuondolewa na wana mizizi minene. Je, Prof. Mwakyusa, haya ndiyo maisha bora kwa wananchi wa Mkoa wa Mara, hasa kwenye huduma?
Muniko hata haki za watumishi anazima na vifaa vya hospitali, ikiwamo TV nk anahamishia kwake. Marupurupu Musoma ni ndoto, na ukichonga mbele Muniko unaondolewa kama Mbwa mwizi.