Watoto 232 mkoani Mwanza wafanyiwa ukatili wa kingono

Suley2019

JF-Expert Member
Oct 7, 2019
1,803
4,464
Akitoa taarifa hiyo kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza John Mongella, Mkuu wa Wilaya ya Ilemela, Dk. Severine Lalika "Kwa mujibu wa taarifa kutoka Jeshi la Polisi mkoani Mwanza inasema kuwa kwa mwaka huu kuanzia Januari hadi Machi jumla ya matukio ni 234 yariripotiwa ambapo kati yao Wavulana wakiwa 17 na Wasichana 219."- amesema Lalika

Kauli hiyo imesemwa katika maadhimisho ya siku ya mtoto Afrika kwa Mkoa wa Mwanza ambayo yamefadhiliwa na Shirika la Plan International.

Amesema kuwa visa vya mimba za wanafunzi ni 143, kubakwa 57 huku kulawitiwa zikiwa 17 hivyo amewataka Maofisa Maendeleo ya Jamii na Ustawi wa Jamii Mkoa na Halmashauri waimarishe utoaji elimu ya malezi na makuzi ya watoto kwa wazazi na walezi ili waelewe wajibu wao wa kulea watoto kwa kuzingatia misingi ya haki na usawa wa kijinsia.
WhatsApp%20Image%202020-06-17%20at%204.13.07%20PM.jpeg


"Lakini pia tukirejea taarifa mkoani hapa kwa mwaka 2019 matukio ya kingono yaliyotokea yalikuwa 420 huku wasichana wakiwa 393,wavulana 37 kati ya hayo mimba za wanafunzi zilikuwa 188,148 kubaka, 39 kulawiti na 34 yalikuwa ya kufanya mapenzi na wanafunzi,"amesema

Amewahimiza watoto kutumia vifaa vya kielektroniki ikiwa ni pamoja na simu na kompyuta kwa usahihi na kwa ajili ya kujifunzia huku wazazi wakielekezwa kusimamia matumizi ya vifaa hivyo kwa watoto wao ili kuwaepusha kujiingiza katika vitendo vya ngono na ukatili mwingine mitandaoni kwani usalama wa mtoto ni muhimu wakati wote.

"Mtoto timiza wajibu wako wa kuheshimu wazazi ,walimu na wana jamii na kufanyia kazi maelekezo wanayopewa ili kulinda haki zao"amesema Lalika.

Naye Meneja wa kitengo kutoka Plan Internation Tanzania Mkoa wa Mwanza Dk. Majani Rwambali amesema wametoa elimu na mafunzo ya kuwahamasisha vijana ambao yameleta hamasa kwa vijana kutoa taarifa pindi wanapofanyiwa ukatili.

WhatsApp%20Image%202020-06-17%20at%204.13.04%20PM.jpeg

Amesema mipango na rasimali zao wamezielekeza katika kumlinda na kumwendeleza mtoto na kutekeleza sheria zote za nchi ili kuweza kufikia malengo mbalimbali yaliyowekwa kwa ajili ya kusaidia na kumwendeleza mtoto huku mkakati uliopo ni utoaji wa elimu katika sehemu mbalimbali za mkoa wa Mwanza.

"Kwa nini idadi ya matukio yanaongezeka kwa sababu watoto wanaopata mimba ni wengi, baada ya kutoa elimu jamii imepata uelewa na ujasiri wa kutoa taarifa kwenye vyombo ambapo inawezekana huko nyuma kulikuwa na matukio mengi zaidi na watu hawakujua wapi pakuyasemea lakini sasa wanatambua haki zao"-amesema Rwambali.

Mwenyekiti wa Baraza la watoto Jamhuri ya Muungano Tanzania, Joel Festo amesema watoto wanakabiliwa na vitendo vya ukatili hasa ya kingono katika sehemu mbalimbali ambavyo vinachochea kuwahasiri kisaikolojia hiyo ni baada ya wazazi wengi kukosa muda na kuwapa majukumu makubwa ikiwemo ya kufanyabiashara.
 
Back
Top Bottom