Watoto 100...!

Mentor

JF-Expert Member
Oct 14, 2008
20,328
23,879
Watoto 100
2016, Januari 5 Jumatano

We mzee unatania!” Yalikuwa ni maneno yangu ya kwanza baada ya kumsikiliza mzee Izadin.

Mimi nilipokuwa kijana niliwahi kumuomba Mungu kuwa nitakapokuja kuoa basi anijaalie watoto 100.” Ndiyo sentensi aliyokuwa ameitamka mwanzoni kwenye maongezi yetu.

Utawaleaje?” nilijikuta nikimuuliza.

Mzee Izadin, dereva wa bosi wetu hapa kazini, alinijibu, “Kwani mimi ndo nawalisha mdogo wangu Mentor? Mimi ni njia tu ya kupitishia riziki yao, ila mtoa riziki ni Mungu pekee

2007, Desemba 22 Jumamosi

Victor, akiwa na miaka 36, alikuwa akifunga ndoa. Ilikuwa ni siku ya sherehe hoi hoi nderemo na vifijo kwani wengi wetu tulikuwa tumeshahisi kuwa kaka Victor hatooa tena. Kila siku alikuwa akituambia kuwa anajipanga na maisha,
anawaandalia watoto wake maisha mazuri. Tulibaki tukijiuliza hao watoto wako wapi maana hatuoni hata dalili za yeye kuwa na ukaribu na mabinti hata wa jirani.

Kaka Victor – kwa jina lingine Mchungaji – ni katika wale wakaka ambao wakati tunakua walikuwa ndio wakaka wa kutolewa mifano majumbani mwenu (role models). Yaani ukifanya jambo baya/kosa unaambiwa, “Muangalieni kaka yenu, kwa nini msimuige hata robo tu ya tabia zake?

Kuna kipindi rafiki yake aliwahi kuniambia, “Yani siku nikimkuta mchungaji na mwanamke chumbani na wote wako uchi na mchungaji akaniambia, ‘sijamfanya chochote’, nitamuamini.” Hivyo ndivyo jinsi kaka Victor alikuwa amejijengea sifa katika jamii.

Zaidi ya yote, kaka Victor alikuwa mfano wa kuigwa hata kimasomo kwani baada ya kumaliza shahada yake ya kwanza katika masomo ya uchumi na kufaulu vyema, alibahatika kupata ufadhili wa kwenda kusoma masomo ya shahada ya uzamili katika chuo kikuu cha Havard huko Massachussets, nchini Marekani.

Alikuwa na akili ya peke yake na mtu wa kujituma. Kwani alipomaliza chuo yeye kabla hata chuo kikuu cha Dar es salaam hawajamuita kuwa mkufunzi msaidizi alikuwa ameshajiajiri kwenye kampuni yake ndogo ya BIMA.

Ngoja nikurudishe nyuma kidogo; wakati yuko mwaka wa pili chuoni yeye pamoja na mwenzake waliandika proposal ambayo ilishinda na walipewa kila mtu fedha taslimu shilingi milioni tano.

Katika vitu alivyovifanya ilikuwa kununua kiwanja huko Kigamboni jijini Dar es salaam, eneo kubwa huko ambako kwa sasa kuna kijiji kiitwacho Avic town. Fedha nyingine alianzisha ‘agency’ yake ya mambo ya BIMA. Ni wakati anajiandaa kwenda kusoma nje alipofuatwa na wawekezaji waliojenga hiyo Avic town ili wanunue eneo lake kwani lilikuwa limepakana sana na eneo lao.

Kwa fedha zile aliwekeza zaidi kwenye ‘agency’ yake na kuongeza mtaji hadi kufanikiwa kuwa ‘brokerage’.

Pamoja na yote hayo alikuwa na vibiashara vya hapa na pale ambavyo vilifanya maisha yake mjini hapa kuwa mazuri na alizidi kutufanya wadogo zake sisi tuonekane bado sana.

Kaka Victor alikuwa mcheshi na mchangamfu na kama kawaida wadada wengi walijisogeza kwake lakini nahisi katika mambo yaliyokuwa mwishoni mwa mawazo yake ni hilo la wanawake.

Kila alipokuwa akiulizwa suala la mahusiano alijibu, tena kwa kizungu, “I worry about things that I have to struggle for, not those that are provided by nature” akimaanisha yeye anahofia juu ya mambo ambayo inabidi kuyapigania kuyapata na sio yale ambayo yapo tu. Kwamba siku mtu akitaka kuoa ataoa tu lakini huwezi kutaka kuwa na mali na ukawa nazo, lazima uweke bidii kuzipata.

Akiulizwa na watu wazima zaidi kuhusu ndoa alikuwa akijibu, “najipanga na kuwaandalia maisha wanangu” Siku zote hakukosa jibu la kwa nini hakutaka kuoa na kwa hilo alifanikiwa kwani alifanikiwa kuwa na biashara ambazo zilikuwa zinaenda vizuri, nyumba ya kuishi na nyingine za kupangisha tena si kwa hela zetu za madafu, uwezo wa kubadili magari japo si kwa kila siku n.k.

Siku kaka Victor anatuambia anataka kuoa hakuna aliyeamini, hata alipomleta binti ambaye kwa hali ya kawaida wengi tungemkataa basi ilibidi tutafute justifications (vihalalishi) za kuonesha kuwa anaweza kuwa wa tofauti.

Na siku hii ya Jumamosi, Desemba 22, 2007 kaka Victor alifunga pingu za maisha huku akiwa kwa hakika amejiandaa na kujipanga vyema kwa ajili ya wanae ambao sasa tuliona wanaweza kupatikana.

Kuanzia Januari 2009

Mafanikio yalizidi kumiminika kwa kaka Victor ambapo wakati huu Mungu alikuwa amewabariki na mtoto mmoja, James. Ni wakati huu pia alipopata ufadhili kwenda nchini Ufaransa kwa ajili ya shahada yake ya uzamivu. Aliondoka akiwa na amani kabisa akijua kuwa kila kitu amekiacha kikiwa katika mikono salama.

Hadi wakati kaka anasafiri hatukuwa na ukaribu sana na shemeji yetu – mke wake – kwani hakupenda sana kututembelea na wala hakuwa akipenda tukienda kwake. Hata hivyo tulimheshimu kwani kaka alikuwa akimpenda sana na kumuamini.

Mwezi wa tano kaka alinipigia simu kuwa amepata safari kwenda jijini Rio de Janeiro kwa ajili ya mkutano. Nilimtakia kila la kheri na hata alipofika alinieleza jiji hilo lilivyo zuri na kunitumia baadhi ya picha kupitia barua pepe.

1 Juni, 2009

Nilipata habari kuwa ndege ya Air France iliyokuwa ikitokea Rio de Janeiro kuelekea jijini Paris imepata ajali na abiria wote 216 waliokuwamo wamefariki. Kwanza haikuniingia akilini hadi nilipokumbuka kuwa hiyo ndiyo siku ambayo kaka alikuwa asafiri kurudi chuoni kwake huko Ufaransa. Nilijikuta nikisali kumuomba Mungu kaka asiwepo kwenye ndege hiyo. Nilijaribu kutumia njia mbalimbali kuhakiki kama alikuwepo bila mafanikio yoyote. Ni hadi walipotangaza orodha ya abiria waliokuwa wamepanda ndege ile ndipo tulipofahamu kuwa kaka Victor hatunaye tena duniani.

Mipango ya mazishi ilifanyika na kwa kuwa miili yao haikupatikana – kwani ndege iliangukia baharini – tulifanya tu ibada na kila mtu kutawanyika. Tulimuuliza shemeji kama aliacha wosia wowote na kama ilivyo ada hakuwa ameandika chochote isipokuwa tu kwa kutumia fomu alizokuwa akijaza kazini na kwingineko alikuwa akimuandika mkewe kama mrithi pekee wa mali zake endapo kifo kitamkuta.

Hivyo sisi kwa kuamini walikuwa wanapendana hatukuona shida na tulimsaidia kupata vibali vyote vya kuhakikisha mirathi na stahiki zote za mumewe anazipata yeye. Tulimuonea sana huruma shemeji yetu kwani bado alikuwa binti mdogo.

Januari 6, 2016

Mpaka naandika hapa, shemeji yetu, aliyekuwa mke wa kaka yangu Victor, amehamia nchini Uganda ambako ameolewa na mwanaume aliyekuwa akifanya kazi ubalozi wa Tanzania nchini Uganda. Miezi michache tu baada ya kaka kufariki, shemeji alitokomea kusikojulikana na kumuacha James mwanaye kwa mama yetu. Tulipojaribu kufuatilia mali za mumewe alizoziacha tulikuta zote zimeshabadilishwa umiliki na hata kampuni ndogo ile ya BIMA aliiuza kwa mchaga mmoja bila taarifa kwetu.

Hakurudi kumuangalia mtoto na hata alipokutana na ndugu yetu mwingine alisema yeye ni mdogo mno kukaa peke yake na huyo mtoto anamnyima fursa hivyo hatomrudia.

Ni jana tu ndiyo nilitoka kumlipia ada James ili aweze kuanza darasa la kwanza mwaka huu.

2016, Januari 5 Jumatano

Tena mdogo wangu asikudanganye mtu, wewe kula yako ya kesho huijui, ni riziki ya Mwenyezi Mungu. Akiamua ule utakula, akiamua ukose, utakosa tu!

Alinishitua kutoka katika lindi la mawazo na kujikuta naendelea kumsikiliza.

Sasa hivi nina watoto 12 na watoto wa ndugu zangu 6 hivyo jumla 18, lakini kwa mshahara wangu huu huu wote wamesoma na wameishi kwangu, wamekula na kulala."

Nilimtania kama bado ana ndoto hiyo ya watoto 100 akanijibu, “unadhani! mke wangu hapa analea mtoto ana miezi nane. Hivyo bado ninaendelea mdogo wangu. Na hapa nina miaka karibia 50 ila ninapiga shughuli kushinda nyie vijana…

Nilimuacha mzee Izadin akiendelea kujisifu huku nikitafakari…sijui na mimi niombe watoto 100???!

Wasalaam wapendwa,

Mentor.
 
Mbona kunzeesha mkuu...

Anyway nahukuru kama umenisoma.
Unajua pamoja na kujificha nyuma ya screen na keyboard's ila bado unaweza kumjua mtu kwa kuanalyse wazo lake,ama kwa frequency anayozungumzia ama kwa uzito wa maada anazoanzisha na kushiriki...siamini katika uzee, mimi ni moja kati ya wachache wanaoamini kwamba uzee ni 'utu ukubwa' ila kuwa smart ni 'utu uzima'...perhaps kuna wazee watu wazima na kuna ambao wamejaaliwa uzee kwa kigezo cha umri...mapini yako ni ya uhakika kaka mkubwa,afande mwandamizi Mentor!
 
Nimekuelewa sana ndugu Mentor but nadhani bado tuna haki ya kutafuta maana kitabu cha NENO la MUNGU kinasema "Baba mwema huacha urithi kwa mwanawe" na "Asiyefanya Kazi asile" so kwa upande wangu ni kweli Riziki inatolewa na MUNGU lakini sio kwa huruma bali ni kwa struggling ambazo mtu unafanya so Kama unaomba watoto 100 inakubidi ufanye struggling za kulisha watoto mia
 
Kaka Victor amenisikitisha..
Wifi amenisikitisha sana..

Huwa nikimuangalia James nakumbuka ule wimbo wa "Mungu akileta mtoto analeta sahani yake..." #nerea

Kujiandaa na kujipanga ni muhimu SANA lakini kujua kuwa kesho yako huiamui wewe ni muhimu zaidi.
 
Huwa nikimuangalia James nakumbuka ule wimbo wa "Mungu akileta mtoto analeta sahani yake..." #nerea

Kujiandaa na kujipanga ni muhimu SANA lakini kujua kuwa kesho yako huiamui wewe ni muhimu zaidi.

Ni kweli usemayo..
 
nakumbuka kitabu cha watoto wa mama ntilie, mwishoni mwandishi akamaliza kwa kuandika, NANI ANAJALI? hii inanikumbusha hadithi ya kisasi niliyoisoma humuhumu JF juu ya tukio alilofanya binti mary, dah! ngoja niishie tu hapa
 
chessboxing13.jpg
 
afande mwandamizi Mentor!

Nimeshaacha hiyo kazi siku mingi...

Kaka Mentor nakusalimia
Shemeji ndo hivyo bado anataka ujana kuzeeshwa hataki bana

Nimekwepa kumuelezea sana shem ili nisilete mgawanyiko wa mawazo. Ila kaka....niseme tu binadamu ni binadamu wa ajabu sana...from your own womb!! From your own waist!!!

Nimekuelewa sana ndugu Mentor but nadhani bado tuna haki ya kutafuta maana kitabu cha NENO la MUNGU kinasema "Baba mwema huacha urithi kwa mwanawe" na "Asiyefanya Kazi asile" so kwa upande wangu ni kweli Riziki inatolewa na MUNGU lakini sio kwa huruma bali ni kwa struggling ambazo mtu unafanya so Kama unaomba watoto 100 inakubidi ufanye struggling za kulisha watoto mia

Kaka Victor alijiandaa kwa ajili ya watoto wangapi mkuu? James amefaidi nini cha baba yake?

Nashindwa nikubaliane na wewe au mzee Izadin.

Duu mentor napenda story zako ila najiulizaga ni za kweli au kiburudisho mkuu?

Siuzi chai mkuu...
 
Back
Top Bottom