Tindo
JF-Expert Member
- Sep 28, 2011
- 58,978
- 103,352
Chonde chonde Wajumbe wa Vikao vya kupitisha majina ya wagombea Ubunge, tunawatahadharisha mapema, mkiwabeba watoa rushwa kwa kisingizio cha funika kombe mwanaharamu apite au eti wagombea walizidiana kura Tunawapigia Wapinzani.
CCM Suala la Rushwa tumeutangazia ulimwengu kuwa tunapambana nal. Leo iweje rushwa ndani ya chama tushindwe kupambana nayo?
Watanzania wote wanajua jinsi wagombea wa CCM walivyoshinda kwa rushwa kwenye majimbo yao, je wakati wa kampeni wananchi tutawambia nini juu ya vita dhidi ya rushwa wakati sisi wenyewe ni watoa na wapokea rushwa?
Agenda ya rushwa wapinzani wataitumia kwa nguvu zao zote. Watoa rushwa wasipitishwe kugombe ubunge au udiwani wamekichafua chama.
Mkuu umetoa angalizo zuri sana. Hata hivyo kwani ccm wanategemea kura kutangazwa washindi au madaraka ya rais? Taasisi zote ikiwemo Takukuru wanaamini kuwa wanawajibu wa kuibeba ccm, ndio maana badala ya watoa rushwa kupelekwa mahakamani, wanawapeleka kwenye kamati ya ccm. Hapo unajiuliza Takukuru kazi yao ni nini iwapo wajibu wao wanawakabidhi wanasiasa. Iwapo rais ataendelea kuachwa bila kushitakiwa, na kupewa madaraka makubwa kama ilivyo sasa, rushwa haitakaa iishe nchi hii.