Watoa mada UDASA kuhusu maadhimisho ya Muungano miaka 53

Makusudically

JF-Expert Member
Feb 3, 2014
2,203
1,235
Nilifuatilia Mwanzo Mwisho wa Mjadala, Dk.Bashilu Ally kwa upande wangu nakubaliana naye hususan ktk suala la "Ufahamu" na hasa kwa kizazi hiki cha nyoka.
Prof.Bakari mimi nilimuona dhahiri no "Partson" na anayaangalia mafanikio ya Muungano with a negative eye.
Dr. Hawra kwa upande wake amejaawa na hofu tu lakini pia ni mpendeleaji wa Uzanzibari. Jambo ambalo halina tija kwa Taifa.
Wengine kama Prof.Mwesiga Baregu, hakuna alichochangia cha maana, kwa sababu unaweza je Prof. Mzima unalalamika kuwa Bunge Maalumu la Katiba hakuna kitu lilichofanya, Wakati Watz wote tulishuhudia na kufuatilia kwa karibu na hadi ikapatikana Katiba Pendekezwa. Tume ya Waryoba ilikuwa inatafuta Maoni tu na siyo majibu wala Katiba ya Tanzania, hivyo hoja ya kulazimisha maoni kuwa mjaibu na Katiba huo mimi nauita ni upofu wa kisiasa. Alizavery yeye ni Partson tu na ni emotional, hakuna cha maana alichochangia zaidi ya kutokwa povu na kutukana matusi hali iliyomfedhehesha na kumpinguzia hadhi.
 
kwa hiyo wewe ni mtaalam na mjuaji sana kuliko hao unaosema ati hawakusema chochote..?

ulitaka waseme yale yanayowafurahisha huko chato ndo uje hapa kuwasifia?..

.
 
kwa hiyo wewe ni mtaalam na mjuaji sana kuliko hao unaosema ati hawakusema chochote..?

ulitaka waseme yale yanayowafurahisha huko chato ndo uje hapa kuwasifia?..

.
Ule mdahalo kwa ufupi ulikuwa mdahalo wa UKAWA wakijadili muungano
 
Mdahalo ulikuwa mzuri sana nawakubali sana prof baregu ,bakari, lwaitama, bashiru wote wameshawahi kunifundisha.
Hivyo vichwa huwezi kabisa fananisha na prof pumba. Jamaa kazalilisha sana wasomi.
Mtoa mada naona ni kati ya wale conservative wasiotaka kuikubali ukweli, kwamba huu muungano wetu ulivyo kwa wakati huu wa sasa unahitaji kufanyiwa marekebisho makubwa hususani baada ya zanzibar kufanya mabadiliko makubwa kwenye katiba yake ambayo yamekinzana na katiba ya jamhuri ya muungano.
 
Back
Top Bottom