Mystery
JF-Expert Member
- Mar 8, 2012
- 15,480
- 30,152
Katika mfumo wa uongozi wa Taifa letu kuna viongozi wa aina 2 ambao ni Viongozi wa kuteuliwa na Rais na viongozi wanaochaguliwa na wananchi.
Viongozi wa kuteuliwa na Rais ni kama vile maDC, maRC, maDED japo kwa kutaja kwa uchache na viongozi wa kuchaguliwa na wananchi ni kama vile madiwani, wabunge na mameya.
Kwa upande wa viongozi wa kuteuliwa na Rais kama hao maDC na maRC ndiyo pia wenyeviti wa Kamati za ulinzi na usalama wa maeneo yao kwa maana hiyo vyombo vya usalama kwenye maeneo hayo huwa vinapokea maagizo kutoka kwa maDC na maRC hao.
Hata hivyo kumekuwa kukitolewa maoni na wananchi wengi kuwa kwa mfumo wa nchi yetu kuwa wa mfumo wa vyama vingi, hawaoni sababu za kuendelea kuwa na mfumo wa kuwa na maDC na maRC kwenye maeneo husika wakati kwenye maeneo hayo tuna watumishi wa Umma wenye nafasi za wakurugenzi wa miji/majiji ambao wanafanya kazi zinazofanana na hizo za hao maDC na maRC.
Tatizo lingine kubwa ambalo limejitokeza ni kuwa ingawa hao maDC na maRC nafasi zao hizo wanatakiwa kutekeleza majukumu yao wakiwa watumishi wa Umma bila kutumbukiza ushabiki wa kisiasa, kwa bahati mbaya sana maDC na maRC wetu wametumbukiza 'ukereketwa' wao wa wazi kabisa kwa chama tawala cha CCM.
Ndiyo maana tumeshuhudia kwa yale maeneo ambayo wananchi wamechagua viongozi wao kutoka vyama vya upinzani wakifanya shughuli zao katika wakati mgumu sana kutokana na vikwazo wanavyowekewa na wateule hao wa Rais.
Tumeshuhudia kwenye maeneo ambayo yana viongozi wa upinzani mara nyingi wakikamatwa na vyombo vya dola wakituhumiwa mathalani kufanya mikutano ya kisiasa ambayo haikutolewa vibali na Polisi!
Hata hivyo kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Ibara ya 3(1) inabainisha wazi kuwa nchi yetu itakuwa na mfumo wa vyama vingi na vyama hivyo vya kisiasa vinatakiwa vifanye shughuli zao vikiwa Huru.
Wakati viongozi wa vyama vya upinzani wakipata wakati mgumu sana wa kufanya shughuli zao za kisiasa kwenye maeneo yao, hali ni tofauti kabisa kwa yale maeneo ambayo yana viongozi wa kuchaguliwa kutoka chama tawala cha CCM, ambapo maDC na maRC wa maeneo hayo husika huwa hawawanyanyasi hata kidogo viongozi hao wa kuchaguliwa kutoka chama tawala cha CCM.
Tumeshuhudia pia maDC na maRC hao kwenye maeneo ambayo wananchi wamechagua viongozi wa upinzani wakitumia sheria kandamizi ya kuwaweka ndani viongozi wa upinzani kwa masaa 'yao' 48 kwa kile ambacho huwa wanadai viongozi hao wa upinzani wametoa kauli za uchochezi ambao unaweza kuleta kuvunjika kwa amani kwenye eneo hilo husika.
Mfano halisi wa matumizi hayo mabovu ya sheria hiyo kandamizi ni namna DC wa Kinondoni, Ally Hapi alivyomweka ndani Mbunge wa Kawe kwa kile alichokiita kuwa ametoa kauli za kumtukana Rais Magufuli.
Ubovu mwingine wa sheria hiyo ni kuwa inamnyima natural justice mtuhumiwa ya haki ya kusikilizwa na DC au RC huyo anakuwa ndiye anayetuhumu, ndiye Polisi anayepeleleza kesi na wakati huo huo anakuwa Hakimu wa kuhukumu kesi!
Kwa mazingira yanavyoonekana ni kama vile miongoni ya 'job descriptions' za maDC na maRC hao ni kuwanyanyasa viongozi wa kuchaguliwa wa vyama vya siasa vya upinzani kwenye maeneo husika.
Mazingira pia yanaonyesha kuwa unyanyasaji huo wa maDC na maRC kwenye maeneo ambayo yana viongozi wa vyama vya siasa vya upinzani yana all blessings kutoka kwa Mkuu wa nchi mwenyewe.
Kwa kuwa kama Mkuu wa nchi angekuwa habariki vitendo hivyo viovu ya hao maDC na maRC tungeshuhudia kutumbuliwa kwa maDC na maRC wa maeneo husika kutokana na matendo yao maovu.
Mfano wa wazi ni kwa vipi kwa mfano RC wa Dar, RC wa Arusha, DC wa Kinondoni,DC wa Meru na DC wa Hai waendelee kuwepo kazini wakati imethibitika beyond reasonable doubt kuwa utendaji wao wa kazi umelenga zaidi kuwanyanyasa na kuwadhalilisha viongozi wa kuchaguliwa kwenye maeneo yao husika?
Kwa hiyo nadhani wananchi tunapaswa tuipiganie Katiba mpya ya nchi ambayo itazifuta nafasi hizi za maDC na maRC ambazo hazina maslahi kwa Taifa badala yake zipo tu kwa ajili ya kukilinda chama kilichoko madarakani na kuleta chuki na uhasama miongoni ya viongozi wa Chama tawala na wale wenzao wa vyama vya upinzani