Wateule wa rais wanawajibika kwa nani, je mleule wa rais anaweza kumuwajibisha mteule mwingine?

The Evil Genius

JF-Expert Member
Mar 21, 2014
5,902
19,090
Nadhani hapa ni mahala muafaka kujifunza haya mambo.

Naomba kujua wajibu wa wateule wa raisi, je mteule wa rais anaweza kumuwajibisha mteule wa rais mwingine?

Nauliza hivi kwa kua nimesikia mteule wa rais mmoja akidai kua asingeweza kuhojiwa na tume iliyoundwa na mteule mwingine wa rais maana wote waliteuliwa na rais.

Je mteule wa rais hawezi kuwajibishwa na tume yoyote itakayoundwa na mteule mwingine hadi iwe imeundwa na rais mwenyewe, mathlani waziri hawezi kumuwajibisha mkurugenzi wa halmashauri kisa na yeye kateuliwa na rais?

Je bodi haiwezi kumuwajibisha mkurugenzi wa shirika la umma kisa wote wameteuliwa na rais na pia bodi inawajibika kwa waziri husika ambae pia ameteuliwa na raisi?

Naomba kujua ukishateuliwa na rais kwenye cheo chochote mfano ukawa mtendaji wa kijiji, je mkurugenzi anaweza kukuwajibisha wakati wote mmeteuliwa na raisi?

Ahsanteni.
 
Back
Top Bottom