Watetezi Waa Maslahi Ya Umma Bungeni Sakata Escrow Mkumbukeni Judge Warioba

DSN

JF-Expert Member
Feb 2, 2011
2,837
1,674
Nawaangukia wana JF kuangalia mgongano huu, ambao kwa wale wenye kusimamia masalahi ya Umma [Fedha Ya Escrow Account Ni Mali Ya Umma dhidi Ya Watetezi Wa Mwekezaji Pesa Ya Escrow Si Mali Ya Umma Ni Mali Ya Singasinga].

Rasimu Ya Judge Warioba ilikuja na Kipengere Cha Mawaziri Wasiwe Wabunge....Leo Muda wote nilipokuwa nikiangalia Utetezi wa Mawaziri Kama Hawa Ghasia, Simba Chawene, Na Waziri wa Sheria nilikuwa natamani kupasuka moyo kwa maumivu kuwa Serikali inachangia Ndani ya Muhimili Wa Bunge Mashihishao Ya Nini Serikali Ikatende Juu Ya Tatizo La Escrow.

Ni Kwa Picha hiyo ambayo Kisaikolojia Ndio ambayo DAIMA imekua ikiwafanya Wabunge Wa CCM Walio Wengi Kujikuta SIKU ZOTE WANAANGUKIA KUWA WATETEZI WA SERIKALI HATA PALE INAPOTAKIWA KUWAJIBISHWA KWA MAKOSA DHAHILI KAMA HILI LA TEGETA ESCROW.

Yani nilipokuwa nawaona Mawaziri wa Serikali wakiinuka na wakichangia maboresho ya maazimio ya Bunge kutoka kwenye mwongozo wa Kamati ya PAC ya ZItto Kabwe ambayo ilikuja na MAPENDEKEZO BORA NA SAHIHI KUIWAJIBISHA SERIKALI na Mawaziri hao chini ya Kinga Ya Kofia Ya Ubunge Nao Wanashiriki Kupanga Nini Cha Kujiwajibisha Nacho Ukweli Kwenye UHALISIA ni Kitu Ambacho HAKIWEZEKANI...Hongera Kwa Mkuu Wa Kambi Ya Upinzani na vijana wake Kwa KUGUTUKIA HILO.

Naomba tujue wavaa kofia mbili yani Ubunge na Uwaziri Ndani Ya Sakata hili ni Sumu Kubwa ya Utatuzi wa MAAZIMIO hayo Ya BUNGE WANAPOPEWA NAFASI HIYO.

Kile Spika Anna Makinda Anachokikwepa Yeye Muhimili Mwenzie Unakitenda Ndani Yake....Kwenye Swala hili,,Kwa Kuwa Kazi Kuu Ya Bunge Ni Kuisimamia Na Kuishauri Serikali..Hivyo kwa Tendo la Kikao Cha Jana Saa Tano Usiku KIUHALISIA NI KWELI BUNGE LINAISIMAMIA NA KUISHAURI SERIKALI ....AU SERIKALI LINAILEKEZA BUNGE NINI KIFANYIKE......

Judge Warioba aliposema mawaziri wasiwe Wabunge alimaanisha Icho kilichotekea Jana Usiku.....pale ambapo sura ya Demokrasia ilipoachiwa itumike kwa kuwa baadhi ya Wabunge ni Waajiliwa Wa Serikali Walijikuta WANAKOSA BUSARA YA KUTAMBUA MAAMUZI YAO WAPI YASIMAME KAMA YA KIBUNGE NA WAPI YASIMAME KAMA YA SERIKALI.

Kwa tukio ilo ata wale Wabunge Wa CCM waliokuwa Wanasukumwa Na Sura ya Utetezi wa UMMA toka kuanzia Kwenye Kamati ya PAC walijikuta Wanamezwa Na kujitanabaisha Na Wabunge CCM na Saikolijia Ya Wabunge Uwaziri Kuwa Swala NI Serikali na Si UMMA.

CHONDE CHONDE WABUNGE WATETEZI WA UMMA .......KUMBUKENI KUTOFAUTISHA MICHANGO YA MIHIMILI YENU BUNGENI KWENYE SAKATA HILI...MSIPOKEE KILAHISI MICHANGO YA MUHIMILI MWINGINE KATIBA AITENDEWI HAKI KWA JAMBO HILO NA UMMA UNATEGEMEA MAAZIMIO YA YA BUNGE YAWE NI YALE YA KAMATI YA PAC NA MABORESHO YENYE TIJA KWA TAIFA.
 
Ni kweli mkuu, nashangaa bibi kiroboto alikuwa analalamika kwa bunge kutaka kuingilia mambo ya serikali, huku serikali kupitia mawaziri ikiingilia waziwazi bunge jana kwa kuwatetea mafisadi mfano kwa kuunga mkono azimio la fisadi chenge!
 
  • Thanks
Reactions: DSN
Ni kweli mkuu, nashangaa bibi kiroboto alikuwa analalamika kwa bunge kutaka kuingilia mambo ya serikali, huku serikali kupitia mawaziri ikiingilia waziwazi bunge jana kwa kuwatetea mafisadi mfano kwa kuunga mkono azimio la fisadi chenge!

Ni kweli Mkuu Kwa Swala La Bunge Kutuma Kamati yake na Kamati Yake Kuleta ripoti yake kisha Watendaji Wa Serikali Kuingilia Maamuzi Ya Bunge ni Uingiliaji Wa Muhimili Mwingine wazi wazi....japo kuna mkoroganyo wa Kikatiba wa Mbunge Kuwa Waziri, lakini kwa hili Bunge likae Kama Bunge na watu wa Serikali Wasiingilie Mapendekezo Ya Maazimio Ya Bunge Kwa kuwa yana INTEREST zao na wale wabunge wa CCM licha ya kuwa ili ni Janga kwao kutetea UOVU pia linachafua Chama Chao Kitaifa Na Kimataifa.....anza na Bunge La KATIBa na Sasa Bunge La Kamati Ya PAC
 
Huyu mama na wenzake wa ccm walikuwa hawana niya ya dhati kila kitu kipo wazi wezi wamejulikana na wengine bado..
Uchunguz ungeendelea kuwatafuta wengine lakini kwa mtu prof muhongo amekuwa akisema uongo waziwazi bado mna mnyenyekea!/????
 
Jee tunaweza kujadili kwa uwazi bila ya kuwa upande wowote wa wabunge wanao komoana ?

1.Tuleteeni mkataba wa escrow hapa tuujadili
2.tuleteeni ripoti ya CAG
Tuleteeni ripoti ya Takukuru.
3. PAP sie mmiliki halali wa IPTL then nani mmiliki halali wa 70% wa iptl?
4.jee mbona hakuna kampuni au mtu yoyote alijitikeza hadharani kupinga umiliki wa PAP ? Na kudai yeye ndie mmiliki ?
5.jee mbona melchar malaysia wako kimya kuhusu shares hizo?
6.kwa nini PAC wameonesha ni halali kwa VIP kuuza share zake 30% kwa PAP wakati PAP sio mmiliki halali wa Iptl na kampuni yenyewe haina uhalali.? ..jee uuzaji huu nao sio haramu ? uuzaji huu nao bila shaka haukuwa na baraka ya waziri kama PAC inavotuambia kwa lazima uhamisho wa share hizi ukubaliwe na waziri?
7. Kwa msingi gani PAC wameiacha kabisa BOT katika hatia? Vipi waliridhia kutoa fedha hizo kama wadhamini wa mfuko kwa mtu ambaye si mmiliki halali ?
8. Vipi BOT walikubali kutoa pesa hizo ? Mkataba unasemaje ? Jee maofisa wake hawahusiki ? Bila shaka wao ndio watuhumiwa wa mwanzo lakimi PAC kwa sababu walishakua na lengo la watu fulani basi wakaacha kabisa suala la uzembe la BOT.
9. PAC inazungumzia juu ya Stanbic na Mkombozi Banks kuhusika na money laundering ...jee Vipi BOT hawahusiki ? Fedha nyingi kama zile kutolewa bila ya shaka zinatoka katika string rooms za BOT bila ya maelezo ya malipo kuhoji fedha zote hizo Banks husika za nini ? uzembe huu wa BOT ambao ndio wasimamizi wa fedha na fiscal policies jee hauja athir mzunguko wa fedha na kushuka kwa Shilling ?
Hakika BOT wanahusika lakini PAC wao walikua na dhamira zaidi za kisiasa.

Muhimu kwa JF ni kuletwa kwa makbrasha yote niliyoyataja hapo juu tukayajadili kama raia wa kawaida njee ya ripoti ya Zitto .hapo ndio kila mtu atajua ukweli bila ya kuwa influenced na PAC ambao dhahiri walikua Biased.
Mpaka hapo the accused are innocent !!
 
Back
Top Bottom