Watetezi wa Lowasa: Ni kweli ni jasiri, mchapakazi lakini je umepima uzito wa upande wa pili | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Watetezi wa Lowasa: Ni kweli ni jasiri, mchapakazi lakini je umepima uzito wa upande wa pili

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by JUST, Jun 22, 2011.

 1. JUST

  JUST JF-Expert Member

  #1
  Jun 22, 2011
  Joined: Dec 10, 2010
  Messages: 554
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 33
  Kumekuwa na watu mbali mbali hap JF wakimueleze Mh. Lowasa kuwa ni Jasiri, Mchapakazi na Mwenye upeo kufananisha na waliopo sasa.


  mimi nasema mtazamo huo unatokana na mfumo wa CCM uliopo ambao hauwapi watu wengine kuonyesha uwezo na ufanisi wao bali unawaacha walewale kutokea uhuru pamaoja na watoto na wajuu wao. hivyo basi ndo maana wengi wanaona katika lili kundi la wanaoongoza Lowasa ndio anafaa. kwa hilo sipingani nao.

  Ila ukweli ni kwamba viongozi wote walioko CCM kwa sasa hawafai kwasababu wote wanamapungufu makubwa ya kiungozi na kimaadili kiasi kwamba ni bora wapishe waje watu wenye uwezo wa kuongoza nchi.

  kwa mantiki hiyo kashfa ya Lowassa ndiyo inayowapa wakati mgumu wa kumuona kama ni mtendaji mzuri maana hata waswahili wanasema huwezi mkabidhi fisi akulindie bucha.
   
 2. M

  Marytina JF-Expert Member

  #2
  Jun 22, 2011
  Joined: Jan 20, 2011
  Messages: 7,035
  Likes Received: 48
  Trophy Points: 145
  sasa wewe tuambie ndani ya hiyo CCM kati ya wale wanaotwajwatajwa 2015 nani mchapa kazi kama Lowassa pamoja na maufisadi yake???
   
 3. fredmlay

  fredmlay JF-Expert Member

  #3
  Jun 22, 2011
  Joined: Apr 30, 2008
  Messages: 1,855
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 135
  Usichanganye mambo, hapa iko hivi ... ili ccm waweze kumpata mgombea lazima atoke kwenye kundi la vigogo ambao kimsingi kwa level ya chini ni NEC kama sio CC, sasa katika kundi hilo hoja nikwamba hakuna mchapa kazi kama Lowasa kwahiyo wanaopinga wanapaswa kusema ni nani katika kundi hilo anaweza kuzidi record ya utendaji ya Lowasa, hakika wote ni mafisadi hakuna haja ya kuwashindanisha ila uchapaji kazi nani zaidi??

  Wana mageuzi ili kutegua hichi kitendawili tupiganie katiba mpya kabla ya uchaguzi mkuu ujao na hatimaye mkuu wa kaya asitokane na magamba ila awe mwanamageuzi, la sivyo ufisadi utakuwa kama kawa yawezekana na utendaji ukawa sifuru pia
   
 4. NATA

  NATA JF-Expert Member

  #4
  Jun 22, 2011
  Joined: May 10, 2007
  Messages: 4,516
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  Mbona mnampamba sana huyo mtu. Allisha jichafua hasafishiki huyo bado ana ari ileile ya ufisadi na kujitajirisha.
  Hasafishiki!
   
 5. bwegebwege

  bwegebwege JF-Expert Member

  #5
  Jun 22, 2011
  Joined: Jul 30, 2010
  Messages: 1,031
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 135
  My blue text explains it all...
   
 6. M

  Mbopo JF-Expert Member

  #6
  Jun 22, 2011
  Joined: Jan 29, 2008
  Messages: 2,532
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Hivi hakuna lingine la kujadili zaidi ya huu utumbo wenu kila siku? Mchukue akawe kiongozi wa ukoo wenu, kama una upungufu wa uongozi. Tumechoka kusikia kibaka akizungumzwa tena kwa vitu hivyo hivyo vya kibwege kila siku. Your hands off us please!
   
 7. M

  Mbopo JF-Expert Member

  #7
  Jun 22, 2011
  Joined: Jan 29, 2008
  Messages: 2,532
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Tell your god (Lowassa) to go and prove his innocence in court. We, the right thinking persons have already convicted him, and, rightly so!
   
 8. DOUGLAS SALLU

  DOUGLAS SALLU JF-Expert Member

  #8
  Jun 22, 2011
  Joined: Nov 13, 2009
  Messages: 11,635
  Likes Received: 4,738
  Trophy Points: 280
  Kumtetea Lowasa inabidi uwe na roho ya mwenda wazimu, jamani huyu mtu ni sawa na zigo la mavi habebeki.
   
 9. M

  Mbopo JF-Expert Member

  #9
  Jun 22, 2011
  Joined: Jan 29, 2008
  Messages: 2,532
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Tena mavi ya jitu lenye uroho
   
 10. M

  MONTESQUIEU JF-Expert Member

  #10
  Jun 22, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 847
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Kwa haya matower mh kazi kweli kweli kumsafisha!
   
 11. Mamndenyi

  Mamndenyi JF-Expert Member

  #11
  Jun 22, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 29,105
  Likes Received: 6,578
  Trophy Points: 280
  kumkubali lowasa ni kukataa maneno ya baba wa taifa '.............lowasa ni mwizi...........'
   
 12. b

  bikira wa Kimasai Member

  #12
  Jan 6, 2015
  Joined: Oct 30, 2014
  Messages: 24
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  (Soma makala hii hadi Mwisho uwajue na ujihadhari nao)

  Na Jacob Malihoja

  WAKATI Mhe.Edward Lowassa alipokuwa Waziri Mkuu na hata katika nafasi zingine alizoshika hakupenda uzembe, hakupenda vitu vilale,hakupenda madudu mbali mbali yafanyike, hakuwa na mzaa .. hiyo ndio hulka yake kwasababu hiyo aliwashughulikia viongozi na watendaji wazembe wasiotekeleza wajibu wao vizuri, waliofanya madudu katika maeneo yao ya kazi.

  Kwasababu watu walikuwa wakifanya kazi kwa mazoea jambo hili lilikuwa geni na kuona wanaonewa. Watu waliotafuna makaa ya moto wa Lowassa wamejenga chuki kubwa sana.

  Kundi Lingine ni lile la kisiasa ambalo pengine Mheshimiwa Edward Lowassa hakuwaunga mkono wakati wa vinyang’anyiro Mbali Mbali na Labda aliwaunga mkono washindani wao.

  Makundi haya yanaungana “sio rasmi” yanatema chuki kwa watu wanaowazunguka, marafiki, familia zao na jamaa wengine mbali mbali walio karibu nao.

  Makundi haya yamekuwa kwa muda sasa yakitengeneza uongo wa aina mbali mbali. Kwa bahati Mbaya kuna makundi madogo ya watu ambao kimsingi wanamhitaji sana Lowassa, bila kujua wameingia kuwaunga mkono watu hao ambao wanadhani ni watetezi wa wananchi kumshambulia mtetezi wa kweli wa wananchi.

  Wanatunga uongo ama kuuamini uongo uliotungwa kwa chuki binafsi. Kila kukicha uongo fulani unatungwa, watu hawa hata hofu ya Mungu hawana, kazi ni kutunga uongo tu kila siku na bila aibu kung’ang’ana na neno moja tu ambalo halina ushahidi na ni la kufikirika.

  Wanapambana wakijifanya kuwatetea wananchi kumbe wao ndio maadui wakubwa wa wananchi wa tanzania kutokana na madudu yao na uzembe wao uliosababisha watafune makaa ya moto wa Lowassa. Watu hawa wanajaribu kufanya juhudi ili fikra zao zipolewe na viongozi wakuu wa chama na wafanya maamuzi mazito ili kumuanguasha Mheshimiwa Lowassa.

  Mimi Siamini kama Wapanga maamuzi ni wepesi kiasi hicho cha kusikiliza kauli za watu waliotafuna makaa ya moto wa Lowassa kwasababu ya uzembe wao, wala siamini kama Viongozi hawa wafanya maamuzi ya juu watakuwa tayari kumezwa na chuki za kisiasa za kutoungwa mkono la Lowassa wakati wa vinyang’anyiro mbali mbali.

  Watanzania wanatakiwa kuelewa kuwa vita dhidi ya Mhe. Edward Lowassa si vita dhidi ya Lowassa bali ni vita dhidi ya Watanzania masikini wanaohitaji mtu mwenye uwezo mkubwa wa kuongeza kasi ya kupapamba na umasikini, ni vita dhidi ya vijana wote ambao leo wapo wanasoma katika shule za kata, ni vita dhidi ya vijana ambao leo wanasoma vyuo vikuu kikiwemo UDOM waliopita katika shule za kata na hata wengine pia.

  Ni vita dhidi ya wananchi wa miji ya Shinyanga, Kahama ambao leo Janga la maji kwao imekuwa historia. Ni Vita dhidi ya vijana ambao hawana ajira ambao kwao Lowassa ni mtu mwenye vision ya kupanua kasi ya kukabili tatizo hilo.

  Ni Vita dhidi ya Rais Dr. Jakaya Kikwete ambaye kimsingi anahitaji kupata mrithi mwenye nguvu kubwa ya kuendeleza Kazi Kubwa mno aliyoifanya.

  Kwa Muono wangu Mhe. Edward Lowassa ndio mtu pekee atakayeweza kuendeleza kazi kubwa mno aliyoifanya Dr. Jakaya Kikwete na kulifanya deni la Taifa kuwa Tamu badala ya Chungu.

  Mungu Ibariki Tanzania, Mungu Mbariki Edward Lowassa.

  Tunakuombea Dr. Jakaya Mrisho Kikwete umpate mtu huyu Kuwa mrithi wako.
   
 13. MO11

  MO11 JF-Expert Member

  #13
  Jan 6, 2015
  Joined: Mar 23, 2014
  Messages: 14,205
  Likes Received: 12,581
  Trophy Points: 280
  umesikia huu ufalme mpaka mrithishane ??
   
 14. OLESAIDIMU

  OLESAIDIMU JF-Expert Member

  #14
  Jan 6, 2015
  Joined: Dec 2, 2011
  Messages: 19,193
  Likes Received: 182
  Trophy Points: 160
  Hakuna maasai mjinga sana kiasi hiki!!!
  Ungeweza kutumia akilia yako kuandika kitu positive zaid kuliko hili juu ya huyo chaguo lako!!

  Aarbo menye. . . . .!!!!
   
 15. mwamajinja mapunga

  mwamajinja mapunga JF-Expert Member

  #15
  Jan 6, 2015
  Joined: Dec 23, 2014
  Messages: 1,083
  Likes Received: 506
  Trophy Points: 180
  lowasa MWIZI Na nachukizwa wasomi kumuunga mkono wakati mnaona wizi ulotokea....
   
 16. Jp Omuga

  Jp Omuga JF-Expert Member

  #16
  Jan 6, 2015
  Joined: Jan 16, 2012
  Messages: 2,671
  Likes Received: 822
  Trophy Points: 280
  Jamani kumsema mtu kuwa ni mwizi bila ushahidi si vizuri (simtetei)... Ingependeza mwenye ushahidi aulete ili tujadiliane kwa uwazi...!!
   
Loading...