Watetezi wa haki za binadamu wa hapa nchini mpo kwa ajili ya kutetea haki gani haswa? Hamuoni tunavyonyanyaswa na hii mitandao ya Mawasiliano?

I am Groot

JF-Expert Member
Jul 20, 2018
3,727
10,023
Yaani nimekaa nikawaza nikajiuliza hivi si kuna kundi kubwa tu la watu wanaojinasibu kuwa ni watetea haki za binadamu hapa Tanzania wako wapi saivi?

Hizo haki ambazo huwa wanatetea na mda mwingine mpaka nchi inazizima kwa kupiga kelele kila pande huwa ni kwa manufaa ya nani?

Wamejitahidi sana kupiga kelele sana na hata kujaribu kuomba msaada wa kusapotiwa na mashirika ya nje hapo mwaka jana katika utawala wa Jpm, haya yanayoendelea mwaka huu hawayaoni, mbona pakiwa sana?

Kama zilivyo haki nyingine, mwaka huu wote tunaona namna haki yetu ya kupata kilicho bora katika sekta ya mawasiliano inavyochezewa hovyo hovyo na watu wachache na hakuna anayesema lolote. Kwa kweli ninashindwa kuelewa mambo haya.

Wananchi wadogo hakika safari hii wako hoi bin taabani wanaangaliana tu wasijue wafanye nini. Na hii ni kwa upande tu wamabando sehemu nyingine ndio usiseme.

Mungu atusaidie kwa kweli.
 
Back
Top Bottom