Election 2010 Watetezi Wa Haki Za Binadamu Mbona Kimya?

Mtu wa Mungu

JF-Expert Member
Joined
Nov 9, 2010
Messages
445
Points
195

Mtu wa Mungu

JF-Expert Member
Joined Nov 9, 2010
445 195
Sources hizi zinahusika!!
1) Matokeo ya Uchaguzi wa 31.10.2010-Sheria za Uchaguzi na Wabunge wa CCM Waliobebwa kuingizwa bungeni "Kupita Bila Kupingwa", na vituko vya jinsi na mbinu walizotumia kujivika sifa hiyo;
2) Gazeti MTANZANIA Jumanne, 16,Novemba 2010- Mtikila Ajiandaa Kuwashitaki Wabunge 19 wa CCM waliopita bila kupingwa;
3) Gazeti TANZANIA DAIMA Alhamisi, 18 Novemba 2010-Kwa Naibu Spika kumbeba Sophia Simba kuingia Bunge la SADC bila kupingwa, Kanuni za Bungwe zimevunjwa;

Katika kufuatilia mijadala ya WanaJF katika maeneo yaliyotajwa juu, ni dhahiri kwamba Haki Za Msingi Za Kibiandamu za Watanzania Waliojiandikisha na Kushiriki Kupiga Kura katika Uchaguzi Mkuu wa 31.10.2010 zimevunjwa kwa kiwango cha kugusa hisia za kila mwanadamu mwenye akili timmamu!!!!!!!!!!
WanaJF wapenda amani na haki wameonyesha kuumia mioyoni na kutamani kuona hatua zinachukuliwa na jamii kurekebisha dosari.
Ni rai yangu wanaJF ambao tumekuwa pamoja katika mada hii ku-call upon WanaHarakati na Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania na kokot ulimwenguni ambako JFForum insomwa, kujitokeza na kuungana na Rev Mtikila, kutetea na kurudishia haki ya msingi ya KUCHAGUA MWAKILISHI BUNGENI Watanzania walioathirika katika majimbo ya uchaguzi 19; Katika sources zilizotajwa zimefafanuliwa kwa muhtasari vitendo ambavyo vina tafsiri ya kuvunjwa kisheria zinzolinda haki za msingi!!!!!!!!!!!!!!!!!
Tukiendelea tu kuonyesha hisia za huruma na uchungu bila kupiga hatua kufikia na kuchukua hatua za njia za ufumbuzi kurejesha haki, kizazi kipya kinachoona mambo haya kwa mara ya kwanza kitachukulia kwamba kupora haki za msingi ni utamaduni wa kuendeleza!!!!!!!!!!! Tutaishia kuwa taifa linaloishi kwa kanuni ya "LAW OF THE JUNGLE"

WanaJF we have a mouth to speak for the weak!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!! Mimi naogopa sana!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
 

Forum statistics

Threads 1,389,707
Members 528,016
Posts 34,032,400
Top