Watetezi wa CCM Hawakitetei Chama ila Wako Katika Elimu Kwa Vitendo(Field)

eedoh05

JF-Expert Member
Apr 20, 2011
632
234
Tafadhari usijisumbue kujibu threads za wana-magamba(aka wana mabwepande) kwa kuwa wenzenu hao hawatetei chama chao ila wako field. Hebu soma sms hii inayopeperushwa katika simu za mkononi. Nawe kama ulikuwa hujaipata inukuu kisha isambaze kama moto wa kiangazi kwa wazalendo wa nchi hii wataka mabadiliko:
UFISADI TRAINING COLLEGE
Chuo kinakutangazia nafasi za kozi zifuatazo kwa
mwaka wa masomo 2010-2015:-


  1. Wizi wa Kura
  2. Utumiaji wa Vyeti Feki ili Kuitwa Daktari
  3. Kulipa Mishahara Hewa
  4. Kuanzisha Makampuni Hewa
  5. Kuiba Misaada na Michango ya Waathirika
Chuo kinakupa nafasi ya Kwenda Field (Elimu kwa Vitendo) EPA, BOT, TRA,
na ukishamaliza kozi utaajiriwa RICHMOND au DOWANS.
CHUO kimetoa wahitimu wengi kama EL, Kara-magi, RA, AC, Chikwete, orodha
ni ndefu.
FOMUzinapatikana Ofisi zote za CCM, Ikulu, BOT na TRA.
WAHI sasa nafasi ni chache.


Kwa kweli, maswahiba na watetezi wa CCM wako field.
 
Hii kali kweli. Mi nadhani wanaotetea CCM wanafanya hivyo kwa kujua kuwa kama itapigwa teke wengi wataishia kuwa walevi na kama siyo kutupwa lupango. Kuna watu hawana hata akili ya kujitafutia kihalali zaidi ya kudhulumu na ufisadi. Hivyo CCM ikizama wamekufa wakiwa hai hawa. Kupe siku zote huishia kwenye mgongo wa ng'ombe hata ngozi yake. Ni maskini hawa wa kuhurumiwa.
 
Back
Top Bottom