Watetezi na wapambe wa Paulo wa Mzizima nifikishieni maswali haya kwake ikiwakera msaidieni kujibu

Freyzem

JF-Expert Member
Jun 29, 2013
10,049
24,428
Kuna video inasambaa kwenye mitandao ya kijamii PAULO kipenzi cha wateule akiwachimba mkwara maafisa elimu kuhusu matokeo mabaya ya eneo lake la uteule, amewapiga mkwara kweli kweli utadhani wao ndiyo walifanya mitihani kwa niaba ya wanafunzi waliofeli anyway naomba wapambe, wamwaga sifa, watetezi wake mnisaidie kufikisha maswali haya machache kwake kwa nia njema kabisa.

1. Kwenye video ametoa agizo kila Afisa elimu atoe maelezo kwanini watoto wamefeli au atoe taarifa ya kuacha kazi , vipi yeye amewahi kufikri kuacha kazi kwa kushindwa mambo haya @ kuondoa omba omba eneo lake la utawala @ utaratibu wa kusafiri bure walimu @ kukomesha ushoga @ kulifanya eneo lake la utawala kuwa safi , nk au anadhani tumesahau . ?

2. Kwa kuwa anaumizwa na matokeo mabaya ktk eneo lake la utawala aseme yeye alipata ufaulu upi ktk masomo yake akiwa elimu ya msingi, sekondari mpaka chuo kama ni mazuri aseme kwanini alifanya vizuri wengine vibaya na kama alifanya vibaya aseme kwanini Wakati wenzake walifanya vizuri ktk mazingira hayo hayo . ?

3. Kwa kuwa anaonekana yeye ndiyo mwenye majibu ya mwisho ktk kuboresha elimu kiasi cha kufanya hitimisho lenye vitisho kuliko kujadili na wadau atusaidie haya @ walimu wangapi eneo lake wana nyumba @ vipi kuhusu malipo ya fedha ya likizo kwa walimu @ vipi kuhusu vitendea kazi kwa walimu @ vipi kuhusu ushirikiano kati ya walimu na wazazi @ vipi kuhusu malimbikizo ya madai .?

4. Hivi anajua sifa za watoto wanaochaguliwa kujiunga kidato cha kwanza na anajua kama kuanzia kidato cha kwanza hakuna mchujo isipokuwa kidato cha pili tena kwa alama za mzaha mtoto akitoka hapo mpaka mtihani wa mwisho kidato cha nne ndiyo wastani wake wa 9 unaleta majibu ya miaka minne ya elimu bure, atusaidie kujua kwanini seminar na shule za private watoto wanafanya vizuri atambue kama mchujo unaleta matokeo chanya ktk ufaulu.?

5. Hivi kati ya mzazi , mwalimu, Afisa elimu , serikali akiwemo yeye yupi mwenye kuthibiti tabia mbovu za wanafunzi hasa wa kutwa kama @ kubeti kuliko kusoma @ ngono na starehe za watu wazima @ kukesha club na kumbi za starehe @ kuvuta bangi @ utoro @ dharau kwa walimu na walezi, nk . ? Je waliowapiga mkwara mzito ndiyo wanaweza kutatua haya . ?

6. Kwa kuwa anatumia matokeo mabaya kuhitimisha kuwa kwenye elimu kuna uzembe ktk utendaji @vipi kuhusu vifo vya mama na mtoto ni uzembe wa sekta ya afya,@ vipi kuhusu ajali za mara kwa mara ni uzembe wa watendaji wa usalama barabarani, @ vipi tatizo la vibaka ktk eneo lake la utawala , @ vipi tatizo la maji , nk au huko ni bahati mbaya sekta ya elimu ndiyo makusudi . ?

7. Kwa kuwa anaamini ktk vitisho kuboresha elimu atusaidie kwa historia ni sekta na eneo lipi la utawala yamewahi kutokea matokeo chanya kutokana na vitisho iwe kwenye elimu au kilimo na kama inawezekana kutumia vitisho walio juu watatishwa na nani au anataka taifa la kila mtu na mnyonge wake yaani @ RC amtishe Dc @ Dc amtishe DED @ DED amtishe mkuu wa idara @ Mkuu wa idara amtishe mtendaji nk taifa litakuwa lenye afya njema . ?

8. Kutokana na mwendelezo wa matukio yake amewahi kujiuliza kama anawapa kazi ngumu watetezi wake @ unga na vita ya kuvuana nguo bila utaratibu @ Shilawadu na askofu wa mipasho @ Ziara ya eneo la utawala na vitisho kwa wataalam @ star TV na majibu yenye sarakasi, nk hivi amewapa nini watetezi wake kiasi cha kuwajaza mizigo ya utetezi kila leo bado hawachoki. ?

9. Hivi amewahi kujiuliza kama cheo ni mara chache sana kufa nacho , anajua kama viongozi wa leo anaweza kuwa mwananchi wa kawaida kesho, amewahi kujiuliza wa chini anaweza kuwa juu kesho, amewahi kujiuza atapata mapokezi gani mtaani baada ya madaraka kukoma....?

10. Hivi amewahi kujiuza madhara ya kuamin ktk kundi la kupongeza, kusifu, kutetea, kutetea na kuunga mkono kila kitu , anajua kama hili kundi lipo kwa faida ya cheo chake bila cheo litakaa pembeni , anajua kama kundi la kukosoa, kupinga kwa hoja , kutoa madhaifu ni kioo cha kujisahihisha na kusonga mbele ...? Amewahi hata kufuatilia matokeo ya viongozi walioishi kwa kuamini sifa, pongeza, shangwe, na utetezi mpaka ktk makosa ...?

NITAKUWA WA MWISHO KUTETEA MAKOSA YA VIONGOZI , KIONGOZI NI MWANADAMU KUKOSEA INATOKEA LAZIMA TUKUMBUSHANE KWA MASLAHI YA TAIFA KWA KIZAZI CHA LEO NA KESHO.

KUJISAHIHISHA SIYO DHAMBI..!!

Lamu Elizayo Pascal Kilimba
lamuelizayo@gmail.com
+255766033331
 
Anafanya kitu ambacho yeye binafsi kashindwa kuuthibitishia umma
 
Back
Top Bottom