Watergate scandal ya mwaka 1974 kule USA mnaikumbuka?

mdukuzi

JF-Expert Member
Jan 4, 2014
16,037
35,903
Waliokuwepo au wanaofuatilia siasa hebu tupeni utamu zaidi nini unajua au kukumbuka kuhusu hii kitu
 
Kama unaweza pakua epub Format ya vitabu hivi:

a601e3b71a1620b35a3d7aa633b97412-d.jpg

Library Genesis: Lamar Waldron - Watergate: The Hidden History: Nixon, The Mafia, and The CIA

And

76d18f99e7c539409923530f68e993c8-d.jpg

Library Genesis: James Rosen - The Strong Man: John Mitchell and the Secrets of Watergate

mdukuzi

ukifungua link hizo gona penye picha za vitabu hivyo uanze kushusha
 
9k=

waliokuwepo au wanaofuatilia siasa hebu tupeni utamu zaidi nini unajua au kukumbuka kuhusu hii kitu

Hahahahaha, wengi wa wana JF walikuwa hawajazaliwa na wengi wengine walikuwa hawajajulikana kama watazaliwa. Nashukuru nilikuwepo.

Watergate ni scandals nyingi za kisiasa kuanzia mwaka 1972 mpaka kilele chake mwaka 1974.

Watergate ni jina la moja ya hoteli ya kifahari hapo Washington DC.

Ni kahadithi karefu kidogo chenye mambo mengi ya hapa na pale na mengine yanarudi mpaka miaka ya vita vya Vietnam 60s.

Kuna wizi (burglary) ulitokea white house uchunguzi wake ukasasambuwa mengi.
 
Bimkubwa umekula munyu si mchezo...ila unavyomwaga radhi za kutetea wevi wako balaa....
 
wanasema you cant judge the book by its cover ila hicho cha juu kina cover nzuri hapo kwenye WATERGATE ingekaa TEGETA ESCROW,Kwenye jina na picha ya NIXON ikawa ZITTO au PROFESSA kitauza sana
 
ungekuwa mwanamume ningesema kidevu kimekua nyembe sana sasa we mdada niseme nini kimekula nyembe ahahahahaha

Sema upendacho wala haitakuwa mara ya kwanza kuyasikia, nadhani ungemuuliza na mama'ko hana ndevu viwembe vya nini? utapata jibu.

Ukiona mtu anakosa adabu ujuwe kwa wazazi wake kulikuwa hakuna adabu.
 
Siasa za wenzetu ndo zona demokrasia ya kweli Watergate ni Scandal ambapo Rais Richard M. Nixon alijiuzulu kwa kusema maneno Haya " by taking this process I will have hastened the start of the process of healing that American need so desparately" kwa tafsiri yangu isiyo rasmi "kwa kuchukua hatua hii nitakuwa nimeharakisha hatua ya mwanzo ya uponyaji wanayohitaji wa Amerika" Tukiangalia maskendo Tz jk angetakiwa wa kwanza kuwajibika Kabla ya E.Lowassa Dowans& Richmond& na sasa Escrow ila kwa kuwa tuna mifano demokrasia Hawa majamaa wanafanya watakavyo kwani mifumo ya utawala huwafanya miungu watu!.
 
Sema upendacho wala haitakuwa mara ya kwanza kuyasikia, nadhani ungemuuliza na mama'ko hana ndevu viwembe vya nini? utapata jibu.

Ukiona mtu anakosa adabu ujuwe kwa wazazi wake kulikuwa hakuna adabu.
Iseeeeee.....!!!????
 
9k=

waliokuwepo au wanaofuatilia siasa hebu tupeni utamu zaidi nini unajua au kukumbuka kuhusu hii kitu

Bwana Mdukuzi omba jamaa moja wa humu JF akijulikana kwa jina ebaeban aione hii nafikiri atakueleza yote , huyu jamaa namwamini sana kwa mambo ya kale yuko vizuri,huwa naona anawapa sana blockbuster wawongo kwa kuwadadavulia vizuri kwa maana ya kuwaelewesha mahali walipokosea , kama akiona hii lazima atakuja labda awe kwao Israel.
 
KASHIFA YA WATERGATE (WATERGATE SCANDAL)

Wakati kashifa hii inagonga vichwa vya habari katika vyombo vya habari duniani miaka ya sabini hapa bongo sisi tulikuwa tunaisoma sana katika gazeti la Newsweek gazeti hili lilikuwa linatoka Marekani kila week na ndege ya shirika la ndege la marekani la TWA ( Trans world Airline) na lilikuwa linauzwa sh 7.

Ilikuwa na very interesting (thrilling) kuisoma ikianza huachi.

Kwa kifupi sana kashifa hii ilitokana na uchaguzi wa urais wa Marekani mwaka 1972. Mgombea wa chama cha republican alikuwa ni rais aliyekuwa madarakani bwana Richard Nixson. Chama cha republican kilikuwa kina dalili ya kushindwa kutokana na kukosa imani nacho kwa wanainchi wa Marekani hasa kushindwa kwa marekani katika katika vita vya Vietnam zote mbili Hanoi na Saigon. Kutokana na sababu hiyo republican ilipunguwa kabisa mvuto kwa maana wakati wanashindwa wanakimbia wenyewe ndio walikuwa madarakani. Vita ya Vietnam na Marekani ilikuwa miaka ya sitini mwishoni kwa hapa Tanzania ilikuwa inatangazwa katika taarifa ya habari ya RTD saa mbili, nakumbuka kuna siku taarifa ya habari hiyo ilitangaza mambo mawili tu ikaisha nayo ni Azimio la Arusha na Vita ya Vietnam.

Republican haikuwa tayari kabisa kushindwa uchaguzi huo kwa hiyo walifanya kila mbinu washinde, hizo mbinu ndizo zilizaa kashifa ya Watergate.

Watergate yenyewe ni hotel ya kifahari iko ufukweni kabisa mwa bahari katika jiji la Washington, mahari hapo ndipo walipokuwa wanafanya mikutano ya kimbinu ya chama pinzani cha democratic, sasa nimesema chama tawala cha republican hakikuwa teyari kushindwa uchaguzi huo kwa hiyo basi walifanya kila mbinu ili washinde moja wapo ya mbinu hizo ni kujua democratic walikuwa wanajadili mbinu gani za ushindi katika ukumbi wa mkutano wa hotel ya Watergate? Walichofanya walipeleka watu wao wakatege kanda za kunasa mazungumzo ya wapinzani wao ndani ya mikutano ili wazijue mbinu zao pia kunasa mawasiliyano yao ya simu. Kwa hili walifanikiwa ila Democratic walianza kushangaa kwa nini kila wanachopanga Republican wanajua na wanatekeleza kila walichoazimia?

Kwa bahati mbaya vyombo walivyotega viliacha kufanya kazi inakisiwa kuwa chama cha Democratic kiligundua mtego huo kikategua na wakaweka na wenyewe mtego. Sasa si ma ba-burglary (kama wezi) wakarudi tena Watergare hotel kutengeneza hiyo hitilafu ili mawasiliano yawafikie tena repulican, ni kama unaenda kuiba mwenyewe anakuona, Democratic wakapiga simu polisi wale jamaa walikamatwa red-handed wakifanya hiyo kazi.

Kwa kifupi hicho ndicho chanzo cha kashifa yenyewe, ofcourse republican walishinda ila democratic walifungua kesi ya udukuzi kwa kutumia private investigator waliwabana vilivyo republican kwa kutumia kanda walizozinasa na zingine zilikuwa teyari ziko kwenye chama tawala ambapo mahakama iliamuru kiongozi wao Richard Nixson azitoe kama ushahidi , alikataa kwani kwa kufanya hivyo ni kama unapeleka kidhibiti Polisi.

Kwa sheria za Marekani alibidi Rais Nixson ajihudhuru ili ashitakiwe mahakamani kwa kashifa hiyo. Rais Nixson alijihudhuru kwa kashfa hiyo ya Watergate mwaka 74 na Makamo wake bwana Gerad Ford aliendeleza urais wake na akamsamehe rais wake asishitakiwe mahakamani.

Hii ni kwa kifupi sana.

Ebaeban
Tel.Aviv
 
Ilikuwa na very interesting (thrilling) ukianza kusoma topic hiyo ndani ya newsweek huachilii.

Kwa kifupi sana kashifa hii ilitokana na uchaguzi wa urais wa Marekani mwaka 1972. Mgombea wa chama cha republican alikuwa ni rais aliyekuwa madarakani bwana Richard Nixson. Chama cha republican kilikuwa kina dalili ya kushindwa kutokana na kukosa imani nacho kwa wanainchi wa Marekani hasa kushindwa kwa marekani katika katika vita vya Vietnam zote mbili Hanoi na Saigon.

Kutokana na sababu hiyo republican ilipunguwa kabisa mvuto kwa maana wakati wanashindwa vita wanakimbia wenyewe ndio walikuwa madarakani. Vita ya Vietnam na Marekani ilikuwa miaka ya sitini mwishoni kwa hapa Tanzania ilikuwa inatangazwa katika taarifa ya habari ya RTD saa mbili, nakumbuka kuna siku taarifa ya habari hiyo ilitangaza mambo mawili tu ikaisha nayo ni Azimio la Arusha na Vita ya Vietnam.

Republican haikuwa tayari kabisa kupoteza uchaguzi huo kwa hiyo walifanya kila mbinu washinde, hizo mbinu ndizo zilizaa kashifa ya Watergate.

Watergate yenyewe ni hotel ya kifahari iko ufukweni kabisa mwa bahari katika jiji la Washington, mahari hapo ndipo walipokuwa wanafanya mikutano ya kimbinu ya chama pinzani cha democratic, sasa nimesema chama tawala cha republican hakikuwa teyari kushindwa uchaguzi huo kwa hiyo basi walifanya kila mbinu ili washinde moja wapo ya mbinu hizo ni kujua democratic walikuwa wanajadili mbinu gani za ushindi katika ukumbi wa mkutano wa hotel ya Watergate? Walichofanya walipeleka watu wao (burglaries) wakatege kanda za kunasa mazungumzo ya wapinzani wao ndani ya mikutano ili wazijue mbinu zao pia kunasa mawasiliyano yao ya simu. Kwa hili walifanikiwa ila Democratic walianza kushangaa kwa nini kila wanachopanga Republican wanajua na wanatekeleza kila walichoazimia? Kwa msemo wa Kiswahili kila Democratic wanakolalia republican ndiko wanakoamkia.

Kwa bahati mbaya vyombo walivyotega viliacha kufanya kazi inakisiwa kuwa chama cha Democratic kiligundua mtego huo kikategua na wakaweka na wenyewe mtego. Sasa si ma ba-burglary (kama wezi) wakarudi tena Watergare hotel kutengeneza hiyo hitilafu ili mawasiliano yawafikie tena repulican, ni kama unaenda kuiba mwenyewe anakuona, wale burglaries waliingia hotelini kwa kuvunja mlango au kwa kutumia funguo malaya Democratic wakapiga simu polisi wale jamaa walikamatwa red-handed wakifanya hiyo kazi.

Kwa kifupi hicho ndicho chanzo cha kashifa yenyewe, ofcourse republican walishinda ila democratic walifungua kesi ya kufanyiwa udukuzi na chama cha republican na walitumia private investigators waliwabana vilivyo republican kwa kutumia kanda walizozinasa na zingine zilikuwa teyari ziko kwenye chama tawala ambapo mahakama iliamuru kiongozi wao Richard Nixson azitoe kama ushahidi , alikataa kwani kwa kufanya hivyo ni kama unapeleka kidhibiti Polisi. Kwa sheria za Marekani alibidi Rais Nixson ajihudhuru ili ashitakiwe mahakamani kwa kashifa hiyo.

Rais Nixson alijihudhuru kwa kashfa hiyo ya Watergate mwaka 74 na Makamo wake bwana Gerad Ford aliendeleza urais wake na akamsamehe rais wake asishitakiwe mahakamani.

Katika sakata hilo mchunguzi mmoja alikuwa anaitwa Robart Cox alipoteza maisha dola ilimumaliza maana alikuwa anajifanya kihelehele sana ninaposema dola ninamaana usalama wa taifa kwa hapa kwetu.

Hii ni kwa kifupi sana.

Jee! Haya mambo kwetu yapo? Hebu toa mfano hai, na jee! Nini kifanyike ? Ili kuzuia?

chrismas njema wana bodi wote wa JF.

Ebaeban
Tel.Aviv
 
KASHIFA YA WATERGATE (WATERGATE SCANDAL)

Wakati kashifa hii inagonga vichwa vya habari katika vyombo vya habari duniani miaka ya sabini hapa bongo sisi tulikuwa tunaisoma sana katika gazeti la Newsweek gazeti hili lilikuwa linatoka Marekani kila week na ndege ya shirika la ndege la marekani la TWA ( Trans world Airline) na lilikuwa linauzwa sh 7.

Ilikuwa na very interesting (thrilling) kuisoma ikianza huachi.

Kwa kifupi sana kashifa hii ilitokana na uchaguzi wa urais wa Marekani mwaka 1972. Mgombea wa chama cha republican alikuwa ni rais aliyekuwa madarakani bwana Richard Nixson. Chama cha republican kilikuwa kina dalili ya kushindwa kutokana na kukosa imani nacho kwa wanainchi wa Marekani hasa kushindwa kwa marekani katika katika vita vya Vietnam zote mbili Hanoi na Saigon. Kutokana na sababu hiyo republican ilipunguwa kabisa mvuto kwa maana wakati wanashindwa wanakimbia wenyewe ndio walikuwa madarakani. Vita ya Vietnam na Marekani ilikuwa miaka ya sitini mwishoni kwa hapa Tanzania ilikuwa inatangazwa katika taarifa ya habari ya RTD saa mbili, nakumbuka kuna siku taarifa ya habari hiyo ilitangaza mambo mawili tu ikaisha nayo ni Azimio la Arusha na Vita ya Vietnam.

Republican haikuwa tayari kabisa kushindwa uchaguzi huo kwa hiyo walifanya kila mbinu washinde, hizo mbinu ndizo zilizaa kashifa ya Watergate.

Watergate yenyewe ni hotel ya kifahari iko ufukweni kabisa mwa bahari katika jiji la Washington, mahari hapo ndipo walipokuwa wanafanya mikutano ya kimbinu ya chama pinzani cha democratic, sasa nimesema chama tawala cha republican hakikuwa teyari kushindwa uchaguzi huo kwa hiyo basi walifanya kila mbinu ili washinde moja wapo ya mbinu hizo ni kujua democratic walikuwa wanajadili mbinu gani za ushindi katika ukumbi wa mkutano wa hotel ya Watergate? Walichofanya walipeleka watu wao wakatege kanda za kunasa mazungumzo ya wapinzani wao ndani ya mikutano ili wazijue mbinu zao pia kunasa mawasiliyano yao ya simu. Kwa hili walifanikiwa ila Democratic walianza kushangaa kwa nini kila wanachopanga Republican wanajua na wanatekeleza kila walichoazimia?

Kwa bahati mbaya vyombo walivyotega viliacha kufanya kazi inakisiwa kuwa chama cha Democratic kiligundua mtego huo kikategua na wakaweka na wenyewe mtego. Sasa si ma ba-burglary (kama wezi) wakarudi tena Watergare hotel kutengeneza hiyo hitilafu ili mawasiliano yawafikie tena repulican, ni kama unaenda kuiba mwenyewe anakuona, Democratic wakapiga simu polisi wale jamaa walikamatwa red-handed wakifanya hiyo kazi.

Kwa kifupi hicho ndicho chanzo cha kashifa yenyewe, ofcourse republican walishinda ila democratic walifungua kesi ya udukuzi kwa kutumia private investigator waliwabana vilivyo republican kwa kutumia kanda walizozinasa na zingine zilikuwa teyari ziko kwenye chama tawala ambapo mahakama iliamuru kiongozi wao Richard Nixson azitoe kama ushahidi , alikataa kwani kwa kufanya hivyo ni kama unapeleka kidhibiti Polisi.

Kwa sheria za Marekani alibidi Rais Nixson ajihudhuru ili ashitakiwe mahakamani kwa kashifa hiyo. Rais Nixson alijihudhuru kwa kashfa hiyo ya Watergate mwaka 74 na Makamo wake bwana Gerad Ford aliendeleza urais wake na akamsamehe rais wake asishitakiwe mahakamani.

Hii ni kwa kifupi sana.

Ebaeban
Tel.Aviv
thanx mkuu big up
 
Bwana Mdukuzi omba jamaa moja wa humu JF akijulikana kwa jina ebaeban aione hii nafikiri atakueleza yote , huyu jamaa namwamini sana kwa mambo ya kale yuko vizuri,huwa naona anawapa sana blockbuster wawongo kwa kuwadadavulia vizuri kwa maana ya kuwaelewesha mahali walipokosea , kama akiona hii lazima atakuja labda awe kwao Israel.
amekusikia na amemwaga nondo tayari
 
jamani ya kale dhahabu.....! hongereni mlioishi kale . Ila nasi tuwe rafiki wa nyaraka. Nixon wa USA alijihudhuru kwa uponyaji wa Waamerika ila hapa kwetu NIXON anatetea wezi kwa kuumiza watanzania...../!
 
Back
Top Bottom