Watengenezaji wa pombe walioipa jina linalomaanisha ''nywele za siri'' waomba msamaha Canada

Wakulonga

JF-Expert Member
Oct 29, 2012
762
772
Watengenezaji wa pombe nchini Canada wamelazimika kuomba msamaha kwa kuipatia pombe jina ambalo katika jamii ya Maori kwa kawaida hutumiwa kutaja ''nywele za sehemu za siri''.

Watengenezaji wa pombe wa kampuni ya Hell's Basement Brewery mjini Alberta walisema kuwa walitangaza kinywaji chao kwa jina la Huruhuru miaka miwili iliyopita, wakidhani neno hilo lina maanisha "manyoya".

Lakini mtangazaji maarufu wa kituo cha televisheni cha kabla la Maori-Hamua Nikora alieleza maana ya neno hilo kupitia video aliyotuma kwenye Facebook, kudhihirisha kuwa kweli neno Huruhuru linamaanisha ''nywele za sehemu za siri''katika jamii ya Maori.

Muasisi wa kampuni hiyo ya kutengeneza bidhaa za pombe aliwaahidi watu wa Maori kuwa bidhaa hiyo sasa itapatiwa nembo mpya ya kuinadi.

"Tunakubali kwamba hatukuzingatia matumizi ya kawaida ya neno huruhuru linalomaanisha nywele za sehemu za siri, na tungefanya mashauriano na wawakilishi wa Maori tungeweza kuelewa vema kuliko kutumia kutegemea kamusi za mitandaoni ," Mike Patriquin aliuambia mtandao wa habari wa CBC.

Makampuni yaliyotumia jina ''Huruhuru'' kunadi bidhaa zo yameonywa yaache kulitumia


Makampuni yaliyotumia jina ''Huruhuru'' kunadi bidhaa zo yameonywa yaache kulitumia

Tungependa kueleza bayana kwamba haikua nia yetu kukiuka maadili, au kuukera utamaduni wa Maori ama watu wake kwa njia yoyote ile, kwa wale wanaoihisi kuwa wamevunjiwa heshima, tunaomba msamaha ."

Bwana Nikora pia amekosoa kiwanda cha ngozi cha New Zealand kwa kutumia jina Huruhuru na akasema kuwa aliwasiliana na viwanda vyote viwili, cha bishaa za ngozi na cha pombe juu ya kosa hilo walilolifanya .

"Baadhi ya watu wanasema kupatia jina hilo bidhaa ni kupongeza , mimi ninasema kuchukua bira idhini neno letu ," alisema.

"Ni ugonjwa wa kuchukua majina ya watu bila idhini walionao. Acheni. Tumieni lugha yenu wenyewe."

Msemaji wa kiwanda cha bidhaa za ngozi cha New Zealand aliuambia wavuti wa shirika la habari la RNZ kwamba hawakuwa na nia ya kumkosea yeyote kwa kutumia jina Huruhuru, ambalo walidhani lina maanisha pamba au manyoya.

BBC
 
Oooh kumbe umejua kama yapo haya. Ahsante.

Cc

My lovely naiman64.
Nilijua ni maeneo yaliyotengwa kwa mambo ya siri kama yalivyotengwa mengine yanayoitwa maeneo ya wazi,maeneo ya makazi,maeneo ya viwanda ,maeneo ya shughuli za kijamii km shule hospital and so forth! Naona chini umemtumia nakala your lovel , vipi yeye maeneo anayomiliki ni ya siri ama ni ya public?
 
Kuna Petrol station Iringa ilikuwa inaitwa Munio(nafikiri ni jina kwenye moja ya koo za wachaga) , Wahehe wa kasema kwao linamaana nyingine isiyo nzuri, wahusika wakabadili na kuwa Muniu.
 
Nilijua ni maeneo yaliyotengwa kwa mambo ya siri kama yalivyotengwa mengine yanayoitwa maeneo ya wazi,maeneo ya makazi,maeneo ya viwanda ,maeneo ya shughuli za kijamii km shule hospital and so forth! Naona chini umemtumia nakala your lovel , vipi yeye maeneo anayomiliki ni ya siri ama ni ya public?

Halafu ukishayajua...?
 
Hizi ni dharau kwa walevi. Yaani bia inaitwa v.uzi. Walevi andamaneni.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom