Watendaji Wizara ya Fedha wasimamishwa kazi kwa tuhuma za matumizi mabaya ya fedha

Comedy show!
Aliye initiate nani?? Au ndiyo kina Kurwa!
Auditors ni mbuzi wa kafara tu!

Everyday is Saturday............................... :cool:
Account holders ndiyo wahusika. Kuna amount fulani haiwezi kutoka bila approval ya juu sana! You are right mkuu.
 
Kwa kweli haijakaa sawa. Accounting Officer aka Afisa Masululi (mwenye vote) ni katibu mkuu wa wizara hiyo ambaye pia anaitwa Mlipaji Mkuu. Pesa ye yote haiwezi kulipwa bila idhini ya Afisa masululi. Mkaguzi mkuu wa ndani si mlipaji na wala hawezi kumzuia afisa masululi kufanya malipo. Kazi yake ni kushauri tu na ushauri wake si lazima ufuatwe.

Hivyo wakuwajibishwa na ubadhirifu huo ni katibu mkuu pamoja na mhasibu mkuu wake. Mkaguzi mkuu wa ndani yeye ni shahidi wa ubadhirifu huo. Of course mwenye mamlaka ya kumwajibisha katibu mkuu si waziri mkuu bali ni rais wa JMT. Waziri mkuu saizi yake ni Mhasibu mkuu - huyu ndiye angaliondoka naye na kumuachia rais kushughulika na katibu mkuu wake. Hao watendaji wengine wadogo wadogo ni kuwaonea tu maana wao wanatekeleza kilichoidhinishwa na hao mabosi wao ie katibu mkuu na mhasibu mkuu.

Ni vizuri sasa Mama akapunguza muda wa kukaa DSM akifanya diplomasia na kukaa zaidi Dom akifanya uendeshaji (executive duties) wa serikali.
 
Account holders ndiyo wahusika. Kuna amount fulani haiwezi kutoka bila approval ya juu sana! You are right mkuu.
Ningeamini PM yuko serious kwa kumuita aliyekuwa katibu mkuu wizara ya fedha, aje kuwajibika, kinyume na hapo, HAYA NI MAIGIZO, na kutafuta cheap popularity.

Ambayo si sawa! Watz siyo wajinga kivile, wana uelewa wa mambo mengi!

Everyday is Saturday :cool:
 
ACHENI KAZI IENDELEE NA RAIS #SAMIA Naa YonaPAVEA

Nimeona malalamiko mengi Mitandaoni hasa kwa Veronica France Nginja Sham

Kimsingi Lazima tujiulize je waziri mkuu amepata wapi hiyo ripoti?

Maake Waziri wa Fedha ameteuliwa Juzi juzi tu na ameapishwa tarehe 01/04/2021 na kwa kuwa wizi umefanyika kipindi hicho labda wezi walitumia uchochoro huo wa Mabadiliko kuiba, na ndo kwanza waziri ameingia ofisini na Waziri mkuu tumemuona na ripoti ya pesa kutolewa haraka haraka mwezi wa nne mpaka wa tano, Lazima wenye Akili tujiulize nani amempa ripoti na nani alimuita pale?
Mimi naamini waziri mkuu anafanya kazi kubwa kama msaidizi wa Karibu wa Rais wetu Mama Samia na ndo Maana tulimuona Mama anamsifia kwa Kazi nzuri hasa Kuhusu magari ya mwendo Kasi UDART.

Na tutambue kila Kiongozi Ana approach yake kiutawala, yawezekana JPM alikuwa akisikia Kitu anachukua Hatua hapo hapo, ila yawezekana Mama #SSH yeye approach yake Ni kujipa siku kadhaa anachukua Hatua, jiulize siku ile waziri mkuu alipofika makao makuu ya UDART UDART akakuta madudu, ila Rais Mama Samia alijipa muda kutafuta Mkurugenzi mpya na leo Mhede kapelekwa pale.
Mama #Samia Ni Mama na Mama hawezi wapatia watoto wake Sumu.

Nasema na namalizia utendaji wa Rais wetu Mpendwa Mama Samia Ni utendaji mzuri na Ni Ule Ule wa Hayati mpendwa wetu JPM, Lakini tambua hatacopy na kupeste kila kitu, atatumia approach nzuri Zaidi kutufikisha Watanzania Kwenye Maendeleo yaliyopiganiwa na watangulizi wake, tena yeye Ana uwanja wa kuchukua kwa woote Mazuri na akaongeza na mengine Mazuri.

IMG_20210601_093307_254.jpg
 
Back
Top Bottom