Watendaji wa wilaya ya Kwimba waamliwa kufanya kazi za kampuni binafsi

nhobola ye2

Member
Dec 22, 2013
24
1
Watendaji wa wilaya ya Kwimba mkoani Mwanza wameamriwa na mkuu wa Wilaya hiyo kufanya kazi za kuuza mbengu za pamba za kampuni binafsi bila malipo wala posho yoyote kwao.

Amri hyo imetolewa na mkuu wa Wilaya bila kujali kuwa watendaji hao wameajiliwa na serikali!.

Je, kwa sheria za utumishi wa umma ni sawa?

Karibu kwa mjadala.
 
Waliipenda wenyewe,wakaishabikia wenyewe,wakaichagua wenyewe..acha waisome namba eeee,ccm mbele kwa mbele!!..kufika 2020 watakuwa wametenda kweli hadi watahisi kutendwa au kutendewa!!
 
watendaji wa ofisi ya mkuu wa wilaya au halmashauri ya wilaya?

je hiyo tenda ilipaswa mzabuni afikishe mzigo kwa wakulima au ktk idara ya serikali?

tuanzie hapo
 
Wacha wauze tu maana wameamriwa na mkubwa wao. Hawakuelezwa kwenye job description kuwa watafanya kazi nyinginezo kadiri watakavyokuwa wameamriwa na mkubwa wao.
 
Back
Top Bottom