Watendaji wa serikali Bukoba(M) ni tatizo sugu

Rweye

JF-Expert Member
Mar 16, 2011
16,958
7,512
Idara zifuatazo hawajirekebishi na hawajifunzi,
1 Mazingira
2. Mipango miji
3 Ujenzi
4 Mipango na Uchumi

Ni idara ambazo kulindana kumezidi huku wananchi wakila shida za uhakika. Sisi wananchi tumemwelewa sana raisi wetu na tutamsaidia kwa kila hari. Kulindana kwenu na kujuana kunatakiwa kukoma mara moja ama sivyo tutawashitaki wazi wazi kwa mwajiri wenu mkuu mh. JPM

Tend a zenu, mipango miji yenu, usafi mjini, ujenzi wenu, kusuasua kurasimisha njia za mapato na mihanya inayoachwa makusudi ili watu fulani fulani wale yanatakiwa kukoma. Hii ni rai yetu kwenu, badilikeni mapema
 
Nyinyi ni wataalamu na kwa ngazi zenu mna mamlaka inayotokana na maarifa yenu (expertise). Kuna mategemeo makubwa sana kutoka kwa wananchi kuja kwenu kwasababu tu nyinyi mna maarifa na mmekwenda shule. Inapotokea mkashindwa kuonesha maarifa yenu kinadharia na kimatendo mnakuwa kwanza mmeidhalilisha elimu yenu lakini pili mnaonesha hata kwenye jamii husika kumbe elimu si lolote na wasomi si kitu.

Nianze na Injinia wa manispaa.
Huyu anasemekana anaruhusu ujenzi wa barabara zisizo na viwango kama barabara za mijini zinavyotakiwa. Mbali na hilo inasemwa pia chini yake kuna watu wanapewa ujenzi wa miradi hii wakati hawana ama utaalamu sahihi ama hawana vifaa vyenye kuhimili na vya kutosha.

Wanasema kwasababu hii barabara zinaharibika mara kwa mara na zinarudiwa kutokana na kujengwa chini ya viwango, kwamba makampuni yanayochaguliwa ni kwa misingi ya 10% na kujuana sana. Hapa kuna ukweli mwingi, ukiziangalia barabara za mjini nyingi zinapasuka hovyo, hazina mitaro ya kuhimili mvua kubwa za Bukoba na bado vibarabara ni vyembamba mno kama ulimi wa mbwa. sehemu kubwa ya barabara zinabaki ni udongo ambao baadae unakuwa tope kuingia barabarani na kuharibu lami, kingo zake ziko kama za miaka ya 1960

Injinia wa manispaa kwanini unaruhusu kujengwa mitaro midogo na isiyo imara ambayo zikinyesha mvua za Bukoba za vuli tu hata kabla ya zile za masika mitalo inakuwa ishapasuka pasuka mno?

Tutaendelea na yanayomhusu mhusika Idara ya ardhi na mipango miji......
 
Write your reply...
uzuri mmoja Karibia wafanyakazi wote wa hapo bukoba mc ni wenyeji
wageni ni wachache,endeleen kujididimiza
Kwamba appointments na posting za watumishi chini ya wizara husika zitakuwa za kikabila?
 
ingia hapo angalia maofisa wa idara zote n wawapi then urudi hapa
umaskini wa kagera unasababishwa na nyie wenyewe wala sio serikali
hata mwanahabari Mathias Byabato anajua hilo
Wewe nipatie hiyo link nicheki yanayonihusu hayo mengine siyo yangu kwa sasa na mie siyo muumini wa data za majararani ...Afrika wanaotengeneza data kila kundi lina malengo yake sawia na vigezo vyao, hata mie naweza nikatengeneza za kwangu na nikawa nazitumia kwa malengo yangu napohitaji ..na ajabu zaidi tunaweza tukawa kila mmoja ana za kwake na kila mmoja anameet mahitaji yake kulingana na vipaumbele vyake, so mambo ya umaskini na utajiri wa wapi sihitaji data za Kuchemshwa kwa ajiri ya wanywa kahawa.
 
MBNA umepanic Mkuu
Fanya utafiti umaskini wa kAgera umesababishwa na wana kagera wenyewe
 
Afisa ardhi naye anatajwa sana na wanamanispaa ya Bukoba. Yake yakoje?

1. Kuzagaa kwa majengo/nyumba zilizokwisha mda wake na kugeuka maghofu mjini. Hizi nyumba ziko mitaa ya Hamugembe, Uswahilini, Kashabo n.k. Zingine zilijengwa toka uhuru hadi leo hazijawahi kukarabatiwa, zimechakaa, kuta zimeoza, bati ,zinadondosha kutu n.k lakini bado zipo mjini

2. Kuna majengo na viwanja vya wazi vingi sana vimegeuzwa vichaka na maeneo hatarishi kufuatia kuachwa kama mapagala na maeneo ya wazi. Haya maeneo ya wazi yamekuwa vichaka mjini huku yakiwa yamejaa majani na vichaka. Mji una majengo mengi ya mda mrefu yasiyoisha na yanachafua taswira ya mji wa Bukoba, hili linawakuna wananchi na wanafikia kuuliza sheria za kuendeleza miji na makazi ziko wapi? Huku ni mitaa ya miembeni, Kashai, na mengine mtaa wa soko kuu. Mengine ni maeneo ya Buyekela, Omukigusha n.k

Na kibaya zaidi haya majengo yapo katika maeneo ambayo kwingine yanatakiwa majengo ya ghorofa lakini zilizopo ni zile za kawaida za "kwetu"
 
Katika masuala ambayo siyapendi ni hayo yanayoendelea hapo Bukoba mpaka inafika hatua tunabaki nyuma kimaendeleo kwa uzembe wa mtu au watu wachache
 
MKUU WA MKOA TUTAWALETEA MHAYA; KAMA KILIMANJARO KWA ANNA NGWIRA ; KELELE ZITAISHA ZA UHAMIAJI, KAHAWA NA MIFUGO
 
Afisa ardhi naye anatajwa sana na wanamanispaa ya Bukoba. Yake yakoje?

1. Kuzagaa kwa majengo/nyumba zilizokwisha mda wake na kugeuka maghofu mjini. Hizi nyumba ziko mitaa ya Hamugembe, Uswahilini, Kashabo n.k. Zingine zilijengwa toka uhuru hadi leo hazijawahi kukarabatiwa, zimechakaa, kuta zimeoza, bati ,zinadondosha kutu n.k lakini bado zipo mjini

2. Kuna majengo na viwanja vya wazi vingi sana vimegeuzwa vichaka na maeneo hatarishi kufuatia kuachwa kama mapagala na maeneo ya wazi. Haya maeneo ya wazi yamekuwa vichaka mjini huku yakiwa yamejaa majani na vichaka. Mji una majengo mengi ya mda mrefu yasiyoisha na yanachafua taswira ya mji wa Bukoba, hili linawakuna wananchi na wanafikia kuuliza sheria za kuendeleza miji na makazi ziko wapi? Huku ni mitaa ya miembeni, Kashai, na mengine mtaa wa soko kuu. Mengine ni maeneo ya Buyekela, Omukigusha n.k

Na kibaya zaidi haya majengo yapo katika maeneo ambayo kwingine yanatakiwa majengo ya ghorofa lakini zilizopo ni zile za kawaida za "kwetu"
ndio eti mnafanAnisha kimji cha bukoba na moshi? mpimwe akili
 
ndio eti mnafanAnisha kimji cha bukoba na moshi? mpimwe akili

Mkuu tafuta zile threads zenu mwendelee na ligi zenu hizo hii iache jinsi ilivyo. Niache kuangalia nakopatia ngawila yangu kutwa nianze vichomi vya kwingine ili iweje?
 
Afisa mazingira na usafi wa manispaa nalo ni jipu.

Kabla sijaendelea acha nianze na kile kilichojiri wakati wa ziara ya waziri mkuu mh. Majaliwa hapa mkoani Kagera wiki mbili zilizopita. Kabla ya kuhairisha mkutano wa hadhara na wakazi wa manispaa ya Bukoba pale kwa Mayunga, nilipata kuyasikia mengi kiasi.

Maofisa wa serikali mkoani Kagera inasemekana si wavumilivu hata kiodogo na kwamba ikitokea raia akasimama kufichua uozo ama kwa kushika bango linaloweka maovu yao basi huyo raia ajiandae pa kwenda baada ya mh. kuondoka. Kwamba utasakwa hadi uvunguni na wakikupata utajuta, naambiwa hawa ndo watendaji wa serikali mkoa wa Kagera. Sasa mie nilikuwa na bango langu tayari kwa ajiri ya waziri mkuu na bahati mbaya mkutano haukuwepo, ndo maana nimeamua kutumia jukwaa letu la Jf.
Atakayetaka kuja kunikamata na mie eti kisa nasema maovu yenu/yake na aje.

Sasa turudi kwenye mada, bwana/bibi mazingira ni jipu Bukoba(M). Mji ni mchafu kuanzia kask-kus, mash-magh. Mji umejaa majani kana kwamba ni machungo ya wanyama. Ni ajabu hata maeneo yanayozunguka ofisi muhimu hapa mjini ni machafu kupindukia, kodi zetu watanzania zinatafunwa bure na watu wa hivi. Mbele ya ofisi zao kuna magugu waweza sema labda ni maua, ukienda kwenye bustani kama round about sijui huwa wanakata majani kwa kutumia vidole. Kila jani lina urefu wake jingine fupi jingine lefu, jingine limeinama na jingine limelala. Unajiuliza hivi hata unadhifu wa utunzaji wa bustani unahitaji PhD kweli?

Barabara zinazofagiliwa hazizidi 4 mji mzima, kwingineko ni uchafu wa kila rangi. Kimsingi najua kwamba Kagera ni moja ya mikoa kunakopatikana wagonjwa wengi wa malaria lakini najiuliza kwa mazingira ya hivi kwanini malaria isiweke kambi? Mh. PM ama JPM nakushauri kuhusu hili la malaria Bukoba/Kagera Fanya mpango wa idara ya usafi wa mazingira kwasababu wao ndo wameamua kuwa walezi wazuri sana wa mazalia ya mbu, wanaona raha kuona malaria haikomi eneo hili

Mie nasema na anayeona namsema basi akawatafute wananchi ndo wanaonituma kwa niaba yao.
 
Back
Top Bottom