Watendaji wa Magufuli; acheni kuwanyanyasa wakulima wa kahawa, Misenyi- Kagera.

Manton

JF-Expert Member
Mar 27, 2012
1,164
1,520
Heshima yenu wakuu! Nimeshindwa kuelewa kiwango cha weledi wanaotumia baadhi ya hawa watendaji wa serikali ya tano ya awamu yenye falsafa tasa ya 'hapa kazi tu' ya mheshimiwa Magufuli, rais wa nchi ya Watanzania.

Nasema hivi kutokana na manyanyaso wanayoendelea kuyapata wakulima wa kahawa huko Misenyi - Kagera. Kitendo cha kuendelea kuwapekua majumbani mwao wakulima na kuwalazimisha wapeleke kahawa zao kwenye COOPERATIVE SOCIETY,bila kuwalipa chochote na wengine kuzipeleka zikiwa hazijakauka,na kuwa amrisha wazihudumie pale pale hadi zitakapo kauka, ni kukosa utu. Kwanini msiache wazikaushie majumbani mwao?

Pili, kauli yenu ya kupambana na 'wahujumu uchumi' iende sambamba kuwa adabisha, wahujumu utu wa raia wema, maskini na wanyonge. Tatu, tambueni kwamba ni bora kuchukiwa na mfalme kuliko wananchi. Nne, nchi hii ni yetu sote,tukifa sisi mtatuzika nyinyi.

Tano, acheni kuwa nyanyasa wakulima wa kahawa,maana bila kahawa msinge heshimika leo.Tuchukieni mtakavyo lakini mjue sote tuna haki ya kuishi kama nyinyi.
 
Wenzenu kilimanjaro walipoletewa mizinguo walingoa kahawa yore na wakapanda migomba.... Tukose wote hiyo potelea mbali

Ova
 
Wenzenu kilimanjaro walipoletewa mizinguo walingoa kahawa yore na wakapanda migomba.... Tukose wote hiyo potelea mbali
Ova
Bora yao wana mlima Kilimanjaro unawaingizia pesa za kigeni, sasa sisi Wanakagera hata kale kapori kawanyama, tumenyanganywa.
 
Kwani hamjamfahamu?hua anatoa maagizo mbele za watu then anazunguka nyuma ya nyumba anawaambia endeleeni hivyo hivyo...poleni
Mkuu umenitoa fundo la uchungu moyoni, kwa kuwa ulichokiandika kimenipa kicheko cha faraja ya 'kilio (kifo) cha wengi ni harusi'. Kumbe, hata huko yapo hivi hivi! Acha tusonge mbele, imebaki sita kutimiza kumi. Yana mwisho.
 
Back
Top Bottom