Watendaji wa bandari yetu wasipobadilika, bandari yetu itakufa! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Watendaji wa bandari yetu wasipobadilika, bandari yetu itakufa!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by The hammer, Mar 2, 2012.

 1. The hammer

  The hammer JF-Expert Member

  #1
  Mar 2, 2012
  Joined: May 17, 2011
  Messages: 2,280
  Likes Received: 1,236
  Trophy Points: 280
  Leo jamhuri ya Kenya imezindua ujenzi wa moja ya bandari kubwa barani Afrika.
  Sote tunajua udhaifu wa bandari yetu,iliyojaa urasimu,wizi wa vifaa nk.....Kwa mtindo huo ipo haja ya kuifanyia marekebisho makubwa bandari hiyo,kiutariwala,utendaji na mfumo ili kuondokana na kero nyingi zilizopo sasa vinginevyo ujio wa bandari hiyo ya majirani zetu bandari yetu itakimbiwa na wengi na hivyo serikali itakosa mapato na kudunisha huduma za jamii na hatimaye itakuwa kama ya kule Tanga.TUNAHITAJI WATENDAJI WABUNIFU,WALIO SAFI NA WACHAPAKAZI ILI KUIONDOA KTK HALI ILIYOPO SASA......TANZANIA NI YETU NA TUTAIJENGA KWA NGUVU ZETU
   
 2. Kiranga

  Kiranga JF-Expert Member

  #2
  Mar 2, 2012
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 34,606
  Likes Received: 6,177
  Trophy Points: 280
  Kikwete kamteua Mgawe mtu aliyekuwa assistant Port Manager, hata hana exposure wala negotiations za kimataifa hajui, board meetings hazijui, huyu ndiye kawa CEO Bandarini kwa kigezo gani sijui.

  PSRC wame wa bully THA kubinafsisha Container Terminal wakati ilikuwa ina run kwa profit! Kisa deal la Karamagi.

  Sasa unategemea innovation gani hapo?

  Then again Kikwete mwenyewe hajawa rais kwa merit, what do I expect?
   
 3. Kimbunga

  Kimbunga Platinum Member

  #3
  Mar 2, 2012
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 13,011
  Likes Received: 1,816
  Trophy Points: 280
  Tumekalia majungu tu. Wakati wenzetu wanazindua mradi mkubwa huko Lamu, TBC1 wanatangaza kwamba wakaazi wa Lamu wameandamana kuupinga huo mradi? Mimi nilitegemea watoe changamoto kwa serikali yetu wao wanaleta majungu ambayo sijayasikia hata BBC zaidi ya raia kadhaa kuonyesha wasiwasi wao lakini Raila na Kibaki wakawahakikishia neema.
  Tukalie tu maneno tuone kama Vision 2025 tutaitimiza hata nusu yake. Tumekuja na single ya kilimo kwanza lakini impact yake siioni. Nchi haina reli huku ina invest kwenye barabara kila kukicha nazo zinaharibika kila kukicja kwa kuwa mizigo ambayo ingepita kwenye reli inapita kwenye barabara.
   
 4. MotoYaMbongo

  MotoYaMbongo JF-Expert Member

  #4
  Mar 2, 2012
  Joined: Jan 7, 2008
  Messages: 1,858
  Likes Received: 200
  Trophy Points: 160
  Ife tu haina faida kwa mlalahoi wa kawaida. Sana wananufaika Mafisadi na familia zao.
   
 5. Kimbunga

  Kimbunga Platinum Member

  #5
  Mar 2, 2012
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 13,011
  Likes Received: 1,816
  Trophy Points: 280
  Mkuu soko la bandari ya DSm lipo tele kazi ingekuwa kuli maintain tu basi. Manchi mengi tu hayana bandari na Tanzania ndio iko strategically kuwahudumia lakini badala ya kuwahudumia tunawafukuza kila kukicha. Nchi nyingi zimekimbilia Mombasa baada ya kuchoka na ubabaishaji wa TZ huku tukiwa tunaangalia tu. Tumezidisha maneno maneno bila kufanya kazi kwa weledi. Hii bandari yetu itabaki kupakua uchafu wa magari toka Japan na Dubai kwa ajili ya Watanzania peke yao na mwisho itashindwa kujiendesha na tutahamia Mombasa ama Lamu; mkuu si unajua tena advantage of economies of scale.
   
 6. Kinyungu

  Kinyungu JF-Expert Member

  #6
  Mar 2, 2012
  Joined: Apr 6, 2008
  Messages: 4,380
  Likes Received: 3,339
  Trophy Points: 280
  Ukifikiria sana mambo ya tz unaweza kulia bure!
   
 7. M

  Mkandara Verified User

  #7
  Mar 2, 2012
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Itakufa mara ngapi? huku majuu ukiulizia kutuma vitu Tanzania wanakwambia kwa nini usitumie bandari ya Zanzibar au Mombasa na watakueleza matatizo kibao ya bandari hiyo. Tumepuuza vitu muhimu kama bandari, reli na usafiri wa ndege acha mbali maji na Umeme kweli bado mnategemea kuna kilichobakia kama sii meli yetu kuzama?
   
 8. Kimbunga

  Kimbunga Platinum Member

  #8
  Mar 2, 2012
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 13,011
  Likes Received: 1,816
  Trophy Points: 280
  Mkuu kumbe ndio maana border za Horohoro na Sirari ziko busy! Wajanja mlishakimbilia MSA; nasikia unatumia muda mfupi kupata mzigo wako tena bila mlungula. Hapa DSM mlungula kwa kila hatua ambayo faili la mzigo wako litapiyia. Kama una gari ukitoka unakutana na jamaa mlangoni wanakuuzia power window zako ambazo walizi clear kabla huja clear gari lako! Uchafu mtupu; hatuko serious kwa lolote.
   
 9. M

  MPadmire JF-Expert Member

  #9
  Mar 2, 2012
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 2,628
  Likes Received: 903
  Trophy Points: 280
  bandari ya dar es salaam ni jina tu limebaki, ilishakufa.

  Watanzania wengi wanapitimisha mizigo yao bandari ya mombasa. Sababu ni urasimu na longo longo nyingi bandari ya dar es salaam.

  Pia kia imebaki jina tu, ndege nyingi zinatua jomo kenyatta nairobi, hivyo watalii wengi wanapitia kenya.

  Tanzania kwishney!!!
   
 10. Kimbunga

  Kimbunga Platinum Member

  #10
  Mar 2, 2012
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 13,011
  Likes Received: 1,816
  Trophy Points: 280
  Mkuu yaani haya mambo yamenifanya nijisikie vibaya mno. Utadhani Tanzania haina watu. Haya mambo yanatufanya tudharaulike kila mahala; Wakenya wanatudharau hadi basi kwa sababu ya upuuzi huu tunaoufanya. Kwa mila zangu mimi kudharauliwa na MKenya hasa mjaluo ni tusi kubwa. Yaani kila kukicha wakenya wanatupiga bao na kendelea kutudharau. Leo wanakuja na mradi mkubwa wa kujenga miundombinu ya kufa mtu, sisi tunakunywa tu togwa. Kenya wanaanza kunywa pombe saa kumi na moja jioni lakini Watanzania ni 24/7! Naona I am losing my temper.

  Ili yasije yakanikuta makubwa najipiga ban kuanzia leo hadi tarehe 15/03/2012 kwa kuwa nikiendelea kuona haya mambo humu ndani naweza tukana nikawa mtwana.
   
 11. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #11
  Mar 2, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  Ni kweli Watendaji wetu wanaowekwa na Rais wetu hawafai; Lakini Hamuoni Kenya wanajaribu kushindana na Tanganyika?

  Hiyo Bandari ya Lamu wanaijenga na kuitangaza ili kutaka UGANDA kuendelea kuitumia na pia kusafirisha OIL iliyogundulika na pia kutaka South Sudan kufanya hivyo as well... kwahiyo hawakufanya kwa Manufaa ya Wakenya, Wamefanya kwa Manufaa ya Utamu wa pesa za nje na miradi ya wakubwa wa nchi hao viongozi wenyewe.

  Ukiangalia Bandari ya Mombasa haina utafauti kiutendaji kama ya Dar ndio Maana Uganda wameamua kusafirisha baadhi ya bidhaa zao kupitia Dar pamoja na kuiita bandari ya Dar imekufa

  Wakenya mnajifanya hamuwajui, kwa kihere here chao; sasa wanajena Airport kubwa karibu na Mpaka na Arusha kuzuia Watalii kutumia Uwanja wa KIA; Mmeona wanalalamika Barabara kuwa inawasaidia watu wa Tanganyika na kulalamika kuwa wanatozwa pesa nyingi na Tanganyika kuingia nchini.

  WAKENYA WAACHENI LAMU ITAISHA KAMA INVESTMENT YA MWENDAWAZIMU
   
 12. K

  Kamundu JF-Expert Member

  #12
  Mar 3, 2012
  Joined: Nov 22, 2006
  Messages: 2,109
  Likes Received: 455
  Trophy Points: 180
  Tatizo la Tanzania kila kitu tunataka serikali ifanye. Je ni kwanini mkuu wa bandari achanguliwe na Raisi??. Kwanini tusijiulize vitu kama hivi kwanza!


   
 13. Sumba-Wanga

  Sumba-Wanga JF-Expert Member

  #13
  Mar 3, 2012
  Joined: Feb 2, 2011
  Messages: 5,387
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 135
  Haya ni maneno ya mkosaji, kutetea watz ambao ni wazembe na wavivu wa kufikiri.
  Hadi leo hii wakenye wanasema Mt Kilimanjaro iko kwako, na sisi wa uzembe wetu tumekaa kimya, tunazungumzia EL atakapokuwa rais.

  wacha watuzidi, that is our fate, hatufai kwa mchuzi wala kwa kukaanga.
   
 14. Sumba-Wanga

  Sumba-Wanga JF-Expert Member

  #14
  Mar 3, 2012
  Joined: Feb 2, 2011
  Messages: 5,387
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 135

  Ni mbaya sana kuona kwamba almost all threads ziko negetive kuhusu watz na serikali yetu.
  sasa sisi tuko proud na kipi?
  What can we do better?
  Inauma sana kuona tunandika threads ambazo zinaisema serikali yetu all, the time lakini bado hakuna kinachofanyika.
  Too bad, what is wrong with us?
  Tumemkosea nini muumba?
  Wakenya wana nini zaidi yetu?
  Hata football inatushinda, tumebakia kushangilia Manchester, Liverpool and chelsea.....
  Shame on us:A S embarassed::shock:
   
 15. Sumba-Wanga

  Sumba-Wanga JF-Expert Member

  #15
  Mar 3, 2012
  Joined: Feb 2, 2011
  Messages: 5,387
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 135
  Na wana make sure wanachagua wenyewe ili waweke watu wao.
  Imagine pamoja na kujua kwamba kampuni ya kalamagi ilipewa mkataba kimyemela bado tu inaendelea na kazi!!!!!
   
 16. Maundumula

  Maundumula JF-Expert Member

  #16
  Mar 3, 2012
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 7,055
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  Bandari ife mara ngapi mbona bandari ya dsm ilishakufa zamani?
   
Loading...