Watendaji wa ardhi manispaa Sumbawanga acheni kunyang'anya viwanja vya Wenye hati fuateni sheria

Lord OSAGYEFO

JF-Expert Member
Feb 19, 2021
3,086
4,881
Hakika inashangaza sana WATENDAJI wa ARDHI MANISPAA ya SUMBAWANGA kufanya kazi Kisiasa badala ya Kufuata SHERIA zilizopo.

MANISPAA imekuwa Ikiwanyang'anya WAMILIKI wa VIWANJA waliovipata KISHERIA na Wanavimiliki kwa HATI za MUDA Mrefu na kuwapa Watu wengine.

UAMUZI huo Wanadai ulifikiwa kwenye VIKAO vyao vya Ndani.HOJA au SABABU ya Kuwanyang'anya ni MANISPAA kudaiwa FIDIA na Waliokuwa Wamiliki wa hayo Maeneo.Swali la kujiuliza

Je, kwanini MANISPAA haikuwalipa FIDIA Wahusika ?
Je Wahusika mpaka MANISPAA inapima na Kugawa VIWANJA walikuwa wapi kudai FIDIA ya Maeneo yao?

Je MANISPAA fedha ilizozipata kwa KUUZA hivyo VIWANJA kwanini hazikutumika Kulipa FIDIA?
Je WALIOMILIKISHWA na Kuandaliwa HATI wana KOSA gani mpaka Wanyang'anywe hivyo Viwanja walivyovipata KISHERIA?
Je SHERIA inasemaje ya kumnyang'anya Kiwanja Mmiliki Mwenye HATI ya MUDA Mrefu na Kummiliksha MTU Mwingine Bila KUFUTA HATI?
Tunamwomba WAZIRI WA ARDHI atoe Tamko juu ya Huu UHUNI unaofanywa na WATENDAJI wake kwani Tayari kuna MGOGORO MKUBWA baina ya WAMILIKI na Wenye Maeneo na WATENDAJI wa MANISPAA.
 
Dunia imeisha! WanaSumbawanga wanakuja kulalamikia JF??
Zile mbinu za kutatua matatizo kiasili😅 kama kujifukiza hazipo huko siku hizi??
Mkurugenzi kuamkia uwanjani?

Everyday is Saturday.............................. :cool:
 
Huko si kuna radi mpaka za jero ahaaaaaa,Hebu acheni kulia watumie radi mchana kweupeee .Wana sumbawanga mnatuangusha bwana nyinyi sio wa kulalamika.
 
Back
Top Bottom