Awali ya yote, pole kwa kazi ngumu ya kuongoza Taifa, ni kazi ambayo ukiwa nje unatamani kuifanya lakini ukiwa ndani unapambana na majukumu mazito ili kutekeleza ahadi ambazo wananchi walihaidiwa. Ama kweli uongozi ni kazi nzito , vile vile ni Jalala nikiwa namaanisha kwamba huwezi kuwafurahisha watu wote, wachache watakupa moyo ila wengi wataishia kubeza na kukosoa bila kujali ugumu wa kazi ya uongozi, ukifanya mazuri mengi wanasema kidogo ila ukikosea hata kidogo sana unaweza hata kufukuzwa kazi.
Nikiachana na huo utangulizi, Leo nimeona niseme duku duku la moyoni kwa niaba ya watendaji wenzangu (Wakurugenzi katika Kata).
Kwanza kabisa Mkurugenzi wa Kata ana majukumu lukuki baadhi yake ni kama ifuatavyo:
Moja ni kusimamia shuguli zote zinazohusu Maendeleo katika vijiji vyote ikiwa ni pamoja na kuvitembelea vjiji hivyo ili kuona hali halisi ya miradi hiyo na changamoto zake.
Kusimamia ukusanyaji wa Ushuru na mapato mapato mengine katika kata.
Ndio mkusanyaji mkuu wa takwimu za Idara zote katika kata na kuaziwasilisha kwenye Idara Husika.
Kuhakikisha ulinzi na usalama katika kata
Ndio kiungo mkuu wa idara zote za serikali katika kata hii ikiwa inajumuisha idara ya Elimu, kilimo,afya,utawala na nyinginezo
Kufanya mikutano hadhara kusikiliza na kubaini kero za wananchi katika viviji vyote ikiwa ni pamoja na kuhakikisha mapato na matumizi ya kila kijiji yanasomwa kwa wananchi.
Muhamasishaji mkuu wa maendeleo katika vijiji vyote na kusaka wadau kuchangia maendeleo ya miradi midigo midogo katika kata.
Hayo ni baadhi tu ya majukumu na ukitazama kwa undani ni majukumu ambayo yanahitaji movement kuzungukia vijiji vyote.
Hivi karibuni wenzetu waratibu elimu kata, wakuu wa shule na walimu wakuu wamekumbukwa na Mheshimiwa Rais kwa kupewa posho kuwarahisishia kazi zao, lakini watendaji kata ambao tuna majukumu makubwa zaidi yao, ukweli ni kwamba tumesahaulika. Majukumu yote niliyotaja hapo juu tunayafanya ya kuzungukia vijiji vyote tunayafanya kwa kutumia sehemu ya mshahara jambo ambalo linapunguza ufanisi katika utekelezaji wa shughuli za mtendaji kata hii ikiwa inahusisha kupunguza kasi ya maendeleo katika kata.
OMBI KWA MHESHIMIWA RAIS MAGUFULI.
Kama ilivyo kwa wenzetu waratibu elimu kata, na wakuu wa shule, na sisi watendaji kata hususan ambao tupo vijijini tunaomba utukumbuke kwa posho angalau hata elfu hamsini(50,000 Tsh), ili tuweze kufanya kazi kwa ufanisi zaidi, kwani sisi watendaji kata tuna mchango mkubwa sana hususan katika swala la maendeleo ya nchi yetu Tanzania. Hiyo posho itatusaidia kuzungukia vijiji vyote katika kata na kuhamasisha kwa ukaribu zaidi miradi ya maendeleo. HAPA KAZI TU.
Natanguliza shukrani za dhati.
WEO.