Watendaji Baraza la Michezo la Taifa(BMT) badilikeni au mtabadilishwa - Dkt. Abbas

Melubo Letema

JF-Expert Member
Apr 1, 2020
296
268
Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Hassan Abbasi, amewataka watendaji wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT), kufanyakazi kwa bidii na wale watakaoonekana kushindwa kutekeleza majukumu yao Serikali itafuata taratibu za kuwaondoa huenda wanachokifanya sasa kimewazidi ukubwa.

Ameyasema hayo jijini Dar es Salaam alipofanya vikao vya kukagua utekelezaji wa kazi na maagizo ya viongozi kwa Baraza la Michezo Tanzania (BMT) na Taasisi ya Hakimiliki Tanzania (Cosota).

"Katika siri sita za mageuzi na mafanikio ambazo nimekuwa nikiwaeleza siku zote-kuwa na timu yenye ari, maadili na inayojituma ya watendaji ni jambo la muhimu sana katika Serikali yetu ya kimageuzi kufanikiwa malengo ya kuivusha Tanzania. Hapa BMT wapo watu kama hawajaelewa hili," alisema Dkt. Abbasi ambaye alitangaza baadhi ya hatua zilizochukuliwa kutokana na matatizo ya kiutendaji katika Baraza hilo kuwa ni pamoja na kuondolewa aliyekuwa Kaimu Msajili wa Vyama vya Michezo.

"Mtendaji Mkuu pendekeza ndani ya siku saba mtu mwingine wa Kukaimu nafasi hiyo ulete wizarani, huyu Msajili aliyekuwepo hapa amesharejeshwa kwenye majukumu ya taaluma yake."

Dkt. Abbasi pia alitumia kikao na BMT kumuonya mmoja wa watumishi wa idara ya utawala BMT kuwa aamue moja kubadilika au kubadilishwa:

"Wizara inapokea malalamiko mengi kuhusu utendaji wako sasa inawezekana ni majungu au kweli una tatizo. Kazi ya Idara ya utawala ni kufanikisha mambo sio kukwaza watumishi na kuwatengenezea jakamoyo. Sasa wewe nilikuwa niondoke na wewe leo, lakini ngoja tukupe muda kukuangalia zaidi."

Awali akizungumza na Menejimenti ya Cosota, Dkt. Abbasi alisisitiza watendaji hao kukamilisha maboresho ya mifumo yanayoendelea ili wasanii na wabunifu wengine waanze kupata migao yao huku akisisitiza moja ya nguzo kuu za Wizara kwa sasa ni pamoja na kuona utawala na utendaji bora kuanzia Wizarani, taasisi hadi kwa wadau wa sekta zote.

"Wizara ikiongozwa na Mhe. Waziri wetu Innocent Bashungwa na Naibu wake Abdallah Ulega kwa sasa katika nguzo muhimu za mageuzi katika sekta zetu nne tumekubaliana hili la utawala bora kuanzia Wizarani, kwenye Taasisi na hadi kwenye asasi za wadau wetu ni muhimu na tutalisimamia ipasavyo. Zama za uzembe, majungu, mizungu na watu kuwekeza katika fitna na akadabraha zimekwisha. Tunanyoosha mambo, kila mtu alipo anyooke kabisa kabla hatujafika kumnyoosha."
 

Similar Discussions

0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom