eastmea
Senior Member
- Jul 28, 2018
- 159
- 133
Kwanza kabisa niwapongeze wasafi kwa hatua waliyoipiga kwani sio jambo dogo kwa hatua waliyofikia
Wasafi FM ni radio ambayo inapatikana kwa mkoa dar es salaam tu hii ni kutokana na sheria zinavyobana kwani haziruhusu kuanzisha radio kwa mkoa zaidi ya mmoja mpaka pale itakapotimiza miaka mitatu na kuendelea kwani naamini diamond hawezi kushindwa kuanzisha zaidi ya mikoa mitano kwa mkupuo iwe kwa uwezo wake binafsi au kwa udhamini wowote ule ila tatizo sheria haziruhusu
Hakika sanaa imezaliwa upya
Ningependa kumshauri waziri wa hii idara aingalie upya hii sheria kwani ni kizuizi kwa maendeleo ya haraka