MpigaKura
JF-Expert Member
- Jan 25, 2007
- 384
- 101
Hatimaye siku si nyingi Tz tutakuwa tunazalisha Mafuta na gesi, Ngoja tuone kama JK atawashkisha waarabu hii dili na kuwanyang'anya wafaransa.
TPDC yagundua mafuta na gesi asilia Mkuranga
HabariLeo; Saturday,January 27, 2007
TANZANIA imegundua Mafuta kwa mara ya kwanza na gesi asilia kwenye Kijiji cha Mkuranga, Mkoa wa Pwani nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam, imefahamika.
Habari kutoka ndani ya Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) na Wizara ya Nishati na Madini zimethibitisha kugunduliwa kwa mafuta na gesi. Ugunduzi huo umekuja baada ya TPDC na kampuni ya Maurel & Prom ya Ufaransa kukamilisha uchimbaji wa kisima uliochukua miezi mitano.
Mratibu wa Mradi wa Mkuranga, George Ngwale alithibitisha kuwapo ugunduzi huo, lakini alikataa kuzungumza zaidi kuhusu suala hilo kwa madai kwamba lilikuwa mikononi mwa Waziri wa Nishati na Madini, Nazir Karamagi."Ninachoweza kusema ni kwamba sasa hivi hatuna (TPDC) mamlaka ya kulizungumzia suala hilo, tunasubiri tamko la waziri, lakini elewa tu kwamba mambo ni mazuri," alisema.
Baada ya juhudi za kumpata Waziri Karamagi kushindikana, Habarileo ilifanikiwa kuzungumza na Ofisa wa ngazi ya juu wa Wizara ambaye alithibitisha habari hizo, ingawa hakutaka kutajwa jina lake gazetini kwa madai kuwa suala hilo lilikuwa mikononi mwa Waziri. Alisema Wizara imepata taarifa za kugunduliwa mafuta na gesi Mkuranga na wanazifanyia kazi taarifa hizo ili kupata maelezo sahihi kabla ya kuutangazia umma kuhusu nishati hiyo muhimu.
"Tunataka kujiridhisha kwanza na taarifa tulizopata kabla ya kutangaza lakini inaonekana mambo ni mazuri" alisema.
Alisema taarifa za awali bado hazijaeleza kama mafuta yaliyopatikana yanatosha kibiashara lakini kama itagundulika ni yakutosha, basi yatasaidia sana kupunguza gharama za kuingiza mafuta kwa kutoka nje kutumia fedha za kigeni.Pia aliongeza kuwa endapo gesi itakuwa ni ya kutosha kibiashara, itaimarisha hazina ya nishati iliyopo nchini hasa katika kutengeneza umeme.
Kisima cha Mkuranga ndicho kitakuwa kisima cha kwanza kutoa mafuta kati ya visima kadhaa ambavyo vimechimbwa ndani na nje ya bahari, na kitakuwa kisima cha tatu baada ya Songosongo na Mnazi Bay kugunduliwa gesi.
Kisima hicho ambacho kilianza kuchimbwa Agosti10 mwaka jana kwa gharama ya Sh bilioni 10, kilikuwa kikamilike baada ya miezi mitatu, lakini kilichelewa baada ya wachimbaji kuongeza mita za kuchimba kutoka 3,200 hadi 3,500. Kwa mujibu wa mkataba wa uchimbaji madini, kampuni ya Maurel & Prom ltd itarudisha gharama za kuchimba endapo mafuta yatapatikana na kitakachobaki, Serikali na Kampuni hiyo zitagawana faida kuanzia siku ya kwanza