WATCH: Oil explorations & projects in Tanzania

MpigaKura

JF-Expert Member
Jan 25, 2007
384
101
Hatimaye siku si nyingi Tz tutakuwa tunazalisha Mafuta na gesi, Ngoja tuone kama JK atawashkisha waarabu hii dili na kuwanyang'anya wafaransa.

TPDC yagundua mafuta na gesi asilia Mkuranga

HabariLeo; Saturday,January 27, 2007

TANZANIA imegundua Mafuta kwa mara ya kwanza na gesi asilia kwenye Kijiji cha Mkuranga, Mkoa wa Pwani nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam, imefahamika.

Habari kutoka ndani ya Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) na Wizara ya Nishati na Madini zimethibitisha kugunduliwa kwa mafuta na gesi. Ugunduzi huo umekuja baada ya TPDC na kampuni ya Maurel & Prom ya Ufaransa kukamilisha uchimbaji wa kisima uliochukua miezi mitano.

Mratibu wa Mradi wa Mkuranga, George Ngwale alithibitisha kuwapo ugunduzi huo, lakini alikataa kuzungumza zaidi kuhusu suala hilo kwa madai kwamba lilikuwa mikononi mwa Waziri wa Nishati na Madini, Nazir Karamagi."Ninachoweza kusema ni kwamba sasa hivi hatuna (TPDC) mamlaka ya kulizungumzia suala hilo, tunasubiri tamko la waziri, lakini elewa tu kwamba mambo ni mazuri," alisema.

Baada ya juhudi za kumpata Waziri Karamagi kushindikana, Habarileo ilifanikiwa kuzungumza na Ofisa wa ngazi ya juu wa Wizara ambaye alithibitisha habari hizo, ingawa hakutaka kutajwa jina lake gazetini kwa madai kuwa suala hilo lilikuwa mikononi mwa Waziri. Alisema Wizara imepata taarifa za kugunduliwa mafuta na gesi Mkuranga na wanazifanyia kazi taarifa hizo ili kupata maelezo sahihi kabla ya kuutangazia umma kuhusu nishati hiyo muhimu.

"Tunataka kujiridhisha kwanza na taarifa tulizopata kabla ya kutangaza lakini inaonekana mambo ni mazuri" alisema.

Alisema taarifa za awali bado hazijaeleza kama mafuta yaliyopatikana yanatosha kibiashara lakini kama itagundulika ni yakutosha, basi yatasaidia sana kupunguza gharama za kuingiza mafuta kwa kutoka nje kutumia fedha za kigeni.Pia aliongeza kuwa endapo gesi itakuwa ni ya kutosha kibiashara, itaimarisha hazina ya nishati iliyopo nchini hasa katika kutengeneza umeme.

Kisima cha Mkuranga ndicho kitakuwa kisima cha kwanza kutoa mafuta kati ya visima kadhaa ambavyo vimechimbwa ndani na nje ya bahari, na kitakuwa kisima cha tatu baada ya Songosongo na Mnazi Bay kugunduliwa gesi.

Kisima hicho ambacho kilianza kuchimbwa Agosti10 mwaka jana kwa gharama ya Sh bilioni 10, kilikuwa kikamilike baada ya miezi mitatu, lakini kilichelewa baada ya wachimbaji kuongeza mita za kuchimba kutoka 3,200 hadi 3,500. Kwa mujibu wa mkataba wa uchimbaji madini, kampuni ya Maurel & Prom ltd itarudisha gharama za kuchimba endapo mafuta yatapatikana na kitakachobaki, Serikali na Kampuni hiyo zitagawana faida kuanzia siku ya kwanza
 
OOh ! Laana hiyo ! Sasa tusubiri tu tuone. Yaani sasa hivi hayo mafuta hayajaanza kujimbwa na kuna walafi ( wala rushwa ) kupita kiasi je yakianza kuchimbwa hayo mafuta ?
 
Hii ni Laana...

Nilikuwa naomba Mungu hayo mafuta wasiyagundue Tanzania mpaka baada ya kama miaka 30 ijayo. Nilikuwa naomba Mungu mafuta yagunduliwe wakati kuna nchi yetu ina Katiba Mpya ya Demokrasia ya Kweli, Elimu angalau ya kidato cha 4 ni 99% kwa raia wote, Uchumi walau 70% uwe mikononi mwa Raia halisi Wtz, na if possible watanzania wenyewe ndio wagundue hayo mafuta, na makampuni ya wTz ndio yachimbe...

But I guess Mungu ana mipango mingine kwa sasa...
 
Mafuta ni laana kubwa sana, watu watakufa, watakosa makazi na CCM wanajiandaa hata kuua kila mtu ili wabakie madarakanin wale wenyewe.

Poleni sana watu wa Mkuranga maana mafuta yenu yata wakaanga wenyewe na ikizingatiwa hata Mbunge wenu ni kilaza badala ya kujadili zahati wachilia mbali hosp anaongelea Mengi na TV yake kama mlimtuma hayo Bungeni.
 
Wenyeji wa mikoa ya PWANI siku zote wamekuwa wakionewa na serikali

Tazama kwa nini wanakataliwa kufanya kilimo kule KAZIMZIMBU

Kwa nini kumejazwa kambi za jeshi kila kona Pwani?

Itakuwa yale yale ya OGONI LAND mara mia wangegundua hayo mafuta MIKOA YA KASKAZINI ambako najua jamaa kule hawataki kuburuzwa kijing jinga

Je unakumbuka wamasai walipogoma kulipa kodi mpaka wapate breakdown ya kodi zao?
 
Wenyeji wa mikoa ya PWANI siku zote wamekuwa wakionewa na serikali

Tazama kwa nini wanakataliwa kufanya kilimo kule KAZIMZIMBU

Kwa nini kumejazwa kambi za jeshi kila kona Pwani?

Itakuwa yale yale ya OGONI LAND mara mia wangegundua hayo mafuta MIKOA YA KASKAZINI ambako najua jamaa kule hawataki kuburuzwa kijing jinga

Je unakumbuka wamasai walipogoma kulipa kodi mpaka wapate breakdown ya kodi zao?

DrWHO hii ilitokea mwaka gani..?? Maana ninavyojua wamasai mimi wala sishangani wao kufanya hivi.
 
ilikuwa wakati wa MKAPA na alikuwa Mwanza katika mambo ay Great Lakes region

kilichotokea wamasai waligoma kulipa kodi ya maendeleo kama sikosei na OLE NJOLAI alipowakoromea na wao wakajibu kuwa wanataka kuona BREAK DOWN kama unavyoona huku ulaya unapewa break down ya council tax na polisi jinsi walivyotumia kodi yako

sasa baada ya kumtolea nje OLE NJOLAI , BM akamtuma PM wake bwana SUMAYE ambaye wamasai walimtolea nje mpaka walipopewa break down ya kodi zao


hiyo ndio kumbu kumbu yangu lakini kama kuna mtu ana version tofauti anakaribishwa kunikosoa
 
Mafuta yamegunduliwa Tanzania rasmi na Wafaransa gonga hapa kwenye uchumi usome kama ilivyoripotiwa na MpigaKura wa JF quoting habari Leo;

Hata kama tutaanza kuchimba kesho sidhani kama kutakuwepo na unafuu wowote wa maisha kwa mtanzania wa kawaida. Tanzania ni ya tatu kwa uchimbaji wa dhahabu Afrika, nini manufaa yake kwa sisi walalahoi??
 
Kama bajeti ya mafuta approximately say 40% ya bajeti yote ni muhimu hizo pesa zitakazopatikana zikachangia bajeti zingine kama vile Elimu na Kilimo cha kisasa. Well inaweza ikatupunguzia matatizo ya Foreign Currency.

Ingawaje wizi ndio utakuwa mkubwa ni muda wa kujiandaa kuweza kuweka mambo sawa. Angalia Hugo Chavez anavyotaifisha vitu kule kwake hata USA wanamkoma, kisa ana mafuta na anawauzia kwa wingi na kuwaambia waache ngebe.
 
Ndugu zangu,

Badala ya kuanza kutengeneza picha ya madhila yanayowaelekea watanzania kwa "ugunduzi" huu ni bora tukachukua hatua za kusoma na kutafiti madhila yatokanayo na utajiri huu wa mafuta kutoka kwa wenzetu waliotangulia ili tuweze kujiandaa kuchukua hatamu ya kuendeleza sekta hiyo kwa manufaa ya watanzania wote.

Natoa changamoto kwa kila mmoja wetu kuchukulia suala la international politics na secuirty strategic implications kwa ugunduzi huo katika nchi yetu.

Kama kuna wasomi wa sekta ya energy (especial social scientists) ni wakati wa kuibuka kutoka mafichoni ili kuchukua lead role ya kuendeleza sekta hiyo nchini. Nyumbani kuna wahandisi na wanauchumi wengi katika sekta hiyo lakini tunakosa wataalamu wa masuala ya kijamii na kiusalama. we need more Social Scientists in this Sector.

Tukichelewa tusije tukaanza kulaumiana.

Tanzanianjema
 
Tanzania to build refinery and oil pipeline

Tanzania has signed a one-year Memorandum of Understanding (MoU) with Noor Oil of Qatar for constructing an oil refinery plant and a 1,200 km pipeline from Dar es Salaam-to-Mwanza.

If the pipeline project will be successful, the investor is thinking of extending it to Uganda, Burundi and Rwanda in the future.

Ms Stergomena Tax-Bamwenda, the Deputy Permanent Secretary at the Ministry of Planning and Economic Empowerment, told that talks were at advanced stages.

"We hope to reach a mutual agreement in the next two to three months," Ms Tax-Bamwenda said. She said: "Our experts and the investors are currently finalising the project ownership structure that should have local participation as well."

The experts are drawn from the ministries of planning; Energy and Minerals; Foreign Affairs; Finance; Justice and Constitutional Affairs; Tanzania Investment Centre (TIC) and Tanzania Petroleum Development Corporation (TPDC). She said that the Qatar oil company want to invest about $ 2.0 bn in the refinery and pipeline that would be implemented concurrently.

"After reaching an agreement the investor will have six months to carry out social, environmental and economic impact assessments before the implementation," Ms Tax-Bamwenda said.

During this period also, Noor Oil will produce project detailed designing. It is estimated that the project, refinery and pipeline, will take three-years to be completed.

Ms Tax-Bamwenda said the refinery and pipeline is important to the country's economy and that is why the project was shifted to the Ministry of Planning. However, the Ministry of Energy and Minerals will continue to coordinate it.

Africommerce International (ACOM), the pipeline's brain child, came up with the idea in early 1990s. The company says that it has so far invested over $ 11 mm, but failed to promote the project. ACOM chairman Elisante Muro said the local participation in the project could have been better implemented at the infant stages.

"It is not fair. We are still the legal owners of the project as per the Parliamentary Investment Committee last year," Muro said.

Two years ago the project was given to Richmond Development Company (RDC) of Houston, Texas after ACOM delayed to develop it. RDC also failed to develop the project after 18 months of exclusivity that ended last December. Tanzania had its own refinery up to the mid 1990s when the Tanzanian and Italian Petroleum Refining (TIPER) stopped production after years of operations since 1969.

TIPER had refinery capacity of 875 kilo-tpy, but at the time of closing, it was operating at 60 % capacity.


Source: East African Business Week
 
mradi wa bomba la mafuta ulianza na RICHMOND. kama habari inavyosema RICHMOND walishindwa kukusanya hela za mradi. Baada ya RICHMOND ikaja kampuni nyingine ya watanzania, AFRI..?? nao wakashindwa kupata pesa.

hawa wa-Qatar inaelekea ni watu wa Kikwete na waarabu kama mnavyowajua pesa iko njenje. tusubiri tuone nini kinaendelea.

bomba la mafuta walilopropose RICHMOND lilikuwa ni la Dar-Mwanza. kenya tayari wanajenga bomba kuelekea Uganda. kama hao wa-Qatar watajenga bomba kuelekea Mwanza, Uganda watakuwa na ushindani mkubwa na wakenya.

Tayari kuna bomba la mafuta la kwenda Zambia. wangeangalia uwezekano wa kurefusha bomba hilo kuelekea Malawi na Congo.
 
Wameamua kutuweka wazi...

Grand oil project

THE government has given a go-ahead to a grand project worth 3.38tri/- in which a crude oil refinery and a Dar es Salaam-Mwanza- Kigoma oil pipeline will be constructed by a consortium of four companies from Qatar, Russia and Germany.

Planning, Economy and Empowerment Minister Juma Ngasongwa said in Dar es Salaam yesterday that the decision to okay the project was reached in Dodoma on Tuesday by the National Investment Steering Committee (NISCO), which sat under the chairmanship of the Prime Minister, Mr Edward Lowassa.

Noor Oil and Industrial Technology Limited (NOIT) from Qatar is co-ordinating the project. “This will be the largest single investment to take place in our country since independence. The project will lead to construction of the biggest oil refinery in East and Central Africa,” said Dr Ngasongwa.

He added that upon its completion, the factory would have the capacity of processing up to 200,000 barrels of crude oil per day. Currently, the Tanzanian Italian Petroleum Refinery (TIPER), which is the only oil processing factory in the country, processes only 17,000 barrels per day. Local consumption is 30,000 barrels per day.

“The excess oil will be exported to our neighbours like Rwanda, Burundi, DR Congo and Uganda using pipelines that are going to be built,” he added. The minister named other companies involved in the project as Roneg Tag from Germany, and Stroytransgas Public Corporation and Zakneftegaz-Promerty both from Russia.

“When completed, Tanzania Petroleum Development Corporation (TPDC) will have ten per cent shares in the pipeline project, whereas the oil refinery will be owned and operated by the consortium and a Tanzanian company,” said the minister. The Tanzanian company has not yet been identified.

The minister added that the shares of the company would be placed at the Dar es Salaam Stock Exchange, where Tanzanians will be allowed to buy up to 49 per cent of the shares.

Dr Ngasongwa said although the timeframe for the project has not yet been discussed, he was optimistic that the three-phase project will start soon after all the groundwork has been laid. He said the government would try to limit its completion to two years.

“The NISCO has also granted the company a strategic investor status, which will allow its smooth operations,” said the minister. The projects will begin with environmental and social impact assessment study.

Successful implementation of the two projects will have substantial economic and social spin-off such as ensuring sufficient petroleum stocks even during acute shortages.

Source: Daily News, Feb 9, 2007
 
I smell kanjanja sijui wewe unasemaje .
Kiko wapi, hebu tufafanulie. Maana kama kuiba hawashindwi kama unavyoona waingereza wanavyotuibia kila kukicha au kwa sababu waarabu?

Kwa taarifa yako hao waarabu nao kila kukicha wanaingizwa mjini na wazungu
 
Mafuta yakipatikana, tumkaribishe Mwenyezi Mungu atuwakilishe kwenye mikataba!
Na Julius Samwel Magodi

WIKI hii pamoja na kutawaliwa na mabomu ya wabunge bungeni ambao walikuwa wakilipuana wenyewe kwa wenyewe kutokana na tuhuma za ama kushiriki katika ubadhirifu wa fedha za walipa kodi au la, kulikuwa na habari ambazo ninaweza kuziita za neema, yaani zile za kupatikana kwa mafuta.

Ingawa wabunge wetu walikuwa bize wakirushiana makombora mazito mazito, lakini Watanzania wengi wanaofuatilia tuhuma zinazoibuka nchini, hawakuona kitu kipya kwani wanajua kashfa kama hizo siku zote hapa nchini huvuma na kisha kuyenyuka mithili ya mafuta ya mgando yaingiapo katika moto.

Sijui kuna nini kinatufanya sisi Watanzania tusichukuliane hatua kali pale ambapo ubadhirifu wa wazi unapojitokeza au kujionyesha. Kigugumuzi hiki cha serikali kushindwa kuwaadhibu watu ambao wanahusika na ufisadi wa fedha za walipa kodi, ndio kitu ambacho kimekuwa kikiwatia hasira wananchi na kushindwa kuwaelewa viongozi wao wakiwamo walioko serikalini.

Hebu acha nirejee katika mada yagu ya leo, baada ya Uganda kugundua akiba yamafuta na huko Kenya kusikika kwa dalili hizo, sasa dalili njema zimeanza kunukia kwa Watanzania baada ya kupata visima vitatu vyenye kuashiria kuwapo kwa mafuta katika eneo la Mnazi Bay, mkoani Mtwara.

Wiki hii, Kamishna wa Nishati na Petroli katika Wizara ya Nishati na Madini, Bashir Mrindoko aliutangazia umma kuwa visima vitatu vilivyochimbwa na Kampuni ya Artumas inayochimba gesi eneo hilo vimiminika vilivyochukuliwa vimeonyesha dalili za kuwepo mafuta machafu.

Alisema vimiminika hivyo, vina kila dalili za kuwepo kwa mafuta na kwamba, kazi inayofanyika ni kubaini kiwango cha vimiminika hivyo na eneo halisi.

Majaribio yaliyofanywa kuhusu eneo la Mnazi Bay, yanaonyesha lina akiba ya kutosha ya gesi asili na bidhaa zingine za nishati.

Vimiminika vilivyopatikana vinaonyesha kiwango cha kati ya 25 na 27 ya ubora, ambavyo kawaida huambatana na mafuta machafu.

Kazi inayofanyika sasa ni kupima kiwango cha mafuta hayo kama yapo ni kiasi gani na yako wapina kwamba sampuli za mapipa 90 zimechukulwa kufanyiwa utafiti huko Marekani.

Kwa hakika kupatikana kwa vimiminika hivyo, kumechochea changamoto ya kuendeleza utafiti wao kwenye eneo hilo.

Ikumbukwe kwamba gesi ya Mnazi Bay iligundulika mwaka 1982, lakini kazi ya uendelezaji ilianza mwaka 2003, serikali ilipotiliana saini na Kampuni ya Artumas kwa ubia na Shirika la Maendeleo ya Petroli (TPC).

Hii ni neema myingine ambayo Mwenyezi Mungu ametujalia tena Watanzania baada ya kutupatia raslimali nyingi mno kama vile madini ya karibu kila aina, wanyamapori, ndege adimu, milima, maziwa na bahari na kutupatia misitu tele ambayo mpaka sasa mingine haijawahi kukanyagwa na mtu tangu duniani iwepo.

Rasilmali zote hizi watu wengi katika mataifa mbalimbali wamekuwa wakitushangaa kwa nini Watanzania tumebakia kuwa masikini, wakati vitu vyote hivi wanavyo wao? lakini jibu la haraka linaloonekana ni kuwa ufisadi umetujaa mno, hatuna uzalendo na hatuwezi kulinda raslimali zetu.

Ni nchi chache sana duniani hujaliwa sana kuwa na rasilmali zote hizi, lakini kinachosikitisha ni njisi ambavyo tumeshindwa kuvifanya viweze kutupatia maendeleo.

Je, hii ni laana ya Mwenyezi Mungu au ni nini? Hawa walafi ambao wanatukwamisha tunashindwa nini kuwakandamizia jela kama anavyosema Masanja Mkandamizaji wa maarufu kama akina Ze Komedi ili wengine waweze kujua kuwa hilo ni fundisho au viongozi wetu nao wanalambishwa utamu wa ufisadi huu?

Mafuta haya ambayo sasa yanaelekea kupatikana, ninaamini kuwa hatayataweza kutunufaisha sisi kutokana na rekodi zetu za nyuma za kuingia mikataba chakavu, yenye usiri mkubwa, mibovu ambayo inaishia kwa baadhi ya maafisa wetu wa serikali kujinufaisha.

Mifano ya mikataba mibovu ambayo serikali iliingia lakini imeshindwa mpaka sasa kuwanufaisha Watanzania ni pamoja na kampuni ya kuzalisha umeme wa mafuta ya IPTL, kuuzwa kwa mashirika mengi ya umma, gesi ya Songosongo, mikataba ya kuzalisha umeme wa dharura mwaka juzi na jana, ile mingi ya madini na kadhalika.

Kama kawaida yetu Watanzania tusitegemee kupata nafuu na mafuta hayo ambayo huenda yatachimbwa hapa nchini kwetu kutokana na ugonjwa wetu wa kuingia mikataba kama vile haiwahusu Watanzania, huku wenzetu wachache wakigeuka kuwa mabilionea.

Nadhani safari hii Watanzania wachache, wenye macho, masikio, tunaoona viziuri, kamwe tusikubali kuingizwa tena mjini na wajanja, rasilmali yetu iachwe iliwe na watu wengine badala ya kuwanufaisha Watanzania wenyewe.

Hivi kweli inaingia akilini mwa mtu kwamba mgeni uliyempa kibali cha kukodisha shamba lako la mahindi kwa ubia kulima, baada ya kuvuna yeye achukue kila kitu halafu wewe uambulie kupewa mabua kwa ajili ya kuezekea ua, mahindi yote achukue!

Ni nchi chache sana duniani ambazo unaweza kupata bahati kama hiyo, ya kupewa ruksa ya kuichezea serikali kadri unavyotaka kwa maana ya kuweka mazingira ambayo unaweza kuwanunua maafisa wanaohusika na masuala ya uwekezaji.

Watanzania sasa tunaitaka serikali katika suala hili la mafuta, mkataba wa kuingia na mchimbaji lazima uwe wa wazi na ambao upate ridhaa ya wananchi kupitia wawakilishi wao wabunge.

Siamini, kama mwekezaji huyo ataweza kuwanunua wabunge wote ili aweze kuiweka nchi katika kona ya ulingo ili aweze kuibia kadri anavyotaka.

Nasema hivyo kwa sababu taratibu za sasa za mikataba kuwa siri na kupitishwa na baraza la mawaziri hakika sio sahihi kwa sababu watu hawa ni wachache ambao hatuamini kama wanaweza kutoa maamuzi siku zote yaliyosawa.

Mikataba karibu yote hii inayoiliza nchi hivi sasa imepitia katika baraza la mawaziri kwa maana nyingine tunaomba mkabata wa mchimbaji wa mafuta mkataba wake upitie katika mikono mingine ambayo ni Watanzania wote au pengine kupitia wawakilishi wao, kama wabunge, madiwani na kadhalika.

Tukichezea hata mkataba wa mafuta, tukifanya uzembe hapo tujue tumekwisha na kwamba hilo jambo linaweza kutuingiza katima vita vya kupigania mafuta.

Ni wazi kuwa watanzania walio wengi hawatakubali kuona kuwa mafuta yanachimbwa hapa nchini lakini hawanufaiki nayo badala yake yananufaisha watu chache.

Ipo mifano mingi ya nchi ambazo zimeingia katika vita kutokana na mikataba ya wawekezaji kushindwa kuwanufaisha. Napendekeza kama vigogo wataendelea kutaka kuikumbatia mikataba hii basi, wananchi tuwaombe wenzetu serikalini watukubalie tumchague Mungu ndiye awe mwakilishi wetu ili tusije tena kuingizwa katika matatizo makubwa ambayo tunayo hadi leo.

Mwandishi wa safu hii ni mhariri wa habari maalum, Anapatikana kupitia baruapepe; juliusmagodi@yahoo.com, simu, 0754 304 336
 
Back
Top Bottom