Watazindua miradi mingi ya mabilioni ama matrilioni lakini nina mashaka kama wataikamilisha

Salary Slip

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
48,679
149,861
Tangu mwanzo nilikuwa najiuliza hii miradi mikubwa ya mabilioni/matrilion tunayoizindua kila kukicha tutaikimilisha vipi ili hali uchumi wetu huu bado mdogo na hata bajeti yetu yenyewe bado ni tegemezi tu kwa kiasi kikubwa.

Mashaka yangu yaliongezeka zaidi siku ya jana baada ya kusikia tunaomba mkopo kutoka Afrika Kusini kwa ajili ya mradi wa kujenga reli ya kisasa.

Kwa kifupi huu ni ushahidi kuwa tunaingia kwenye miradi mikubwa na mingi kwa wakati mmoja kuliko uwezo tulionao huku tukiwa hatuna uhakika wa fedha za kukamilisha miradi husika kwa wakati.

Hakika hili ni tatizo tena kubwa na linaloweza kuja kutuumbua hapo baadae kwa kushindwa kukamilisha hii miradi kwa wakati na tunaweza kuja kujikuta tuna miradi iliyododa na kusimama kwa miaka mingi kama magofi.

Miradi hii ni kweli tunaihitaji lakini sidhani kama tulikaa chini na kupanga mikakati yetu kwa umakini ni jinsi gani tunaweza kuitekeleza kwa wakati na bila kuathiri sekta nyingine nyeti zinazotegemea chanzo kile kile cha fedha.

Kwa mtazamo wangu,miradi tunayoweza kuikamilisha ni ile ambayo haitegemei fedha zetu za ndani bali inategemea mikopo ya ndani na nje kwa asilimia mia moja(na sidhani kama tuna aina hiyo ya miradi ambayo serikali haichangi hata sent) na pia mikopo hiyo nayo iwe ni ya uhakika vinginevyo yatakuwa ni yale yale.

Kwa kukwepa aibu,tunaweza kulazimisha kwa kuelekeza fedha nyingi katika miradi hiyo tuliozindua kwa mbwembwe nyingi lakini tujiandae kwa matokeo ya maamuzi ya aina hiyo ikiwa ni pamoja na kudorora kwa sekta nyingine nyingi na kupungua kwa uwezo wa serikali kuhudumia wananchi wake.

Mfano hivi sasa wakati tunanua ndege karibu sita kwa mpigo lakuni angali jinsi wabunge wanavyolia na utekelezaji wa bajeti inayoishia mwezo June mwaka huu ambapo miradi mingi kama ile ya maji imekwama huku bajeti ya wizara hiyo ikipewa fedha kidogo sana kulinganisha na fedha zilizokuwa zimetengwa.

Sasa hapo kumbuka bado madeni ya kulipia ndege hizo bado hayajaisha huku tumeanza tena kujipanga kujenga reli ya kisasa,treni ya umeme, kujenga nyumba kama zile za Magomeni nchi nzima,mradi mkubwa wa kuvuta maji kutoka ziwa victoria kupeleka mkoa wa Tabora,n.k..

Ni kweli kabisa miradi hii ni muhimu na tunaihitaji lakini ni bora twende kwa awamu kwa kuangali ni nini vinapaswa kuwa vipaumbele vya kwa sasa kulikoni kuwa na miradi mingi ya mabilioni ambayo tunaweza kabisa tusikimalishe au tukaikamilisha kwa kuathiri vibaya sekta nyingine au kwa kuongeza kwa kiwango kikubwa deni la Taifa na hatimae tukajikuta tunafikia hatua tukawa hata hatukuposheki tena.

Tujipime uwezo wetu kwa kuangalia jinsi tulivyotekeleza Bajeti hii ya trilioni 29.5 bila kusahau mwenendo wa nchi wahisani na mashirika mengine ya kimataifa ya misaada katika kutimiza ahadi zao.

Tusipende figure kubwa kubwa wakati uchumi wetu ni wa figure ndogo tutaishia kuumbuka na kushindwa hata kutimiza vile vichache vilivyo ndani ya uwezo wetu kwa kutawanya fedha kiduchu tulizonazo katika maeneo mengi na matokeo yake huko kote zisitosheleze.
 
Tuache tufanye kazi huu c mda wa siasa, tunachotaka wananchi maendeleo haijalishi njia ipi tutapita. Isije kuwa ndo mnaponda halafu ndo wa kwanza kubuk bombadia na kusoma siti za namba mkitafuta mapungufu
 
Mtaona matokeo yake
 
Kwani we umesahau kasumba za wanasisiasa hawajawahi kukamilisha ahadi zao hivyo sishangai hata huyu asipotimiza
 
Tangu mwanzo nilikuwa najiuliza hii miradi mikubwa ya mabilioni/matrilion tunayoizindua kila kukicha tutaikimilisha vipi ili hali uchumi wetu huu bado mdogo na hata bajeti yetu yenyewe bado ni tegemezi tu kwa kiasi kikubwa.

Mashaka yangu yaliongezeka zaidi siku ya jana baada ya kusikia tunaomba mkopo kutoka Afrika Kusini kwa ajili ya mradi wa kujenga reli ya kisasa.

Kwa kifupi huu ni ushahidi kuwa tunaingia kwenye miradi mikubwa na mingi kwa wakati mmoja kuliko uwezo tulionao huku tukiwa hatuna uhakika wa fedha za

ya

kukamilisha miradi husika kwa wakati.

Hakika hili ni tatizo tena kubwa na linaloweza kuja kutuumbua hapo baadae kwa kushindwa kukamilisha hii miradi kwa wakati na tunaweza kuja kujikuta tuna miradi iliyododa na kusimama kwa miaka mingi kama magofi.

Miradi hii ni kweli tunaihitaji lakini sidhani kama tulikaa chini na kupanga mikakati yetu kwa umakini ni jinsi gani tunaweza kuitekeleza kwa wakati na bila kuathiri sekta nyingine nyeti zinazotegemea chanzo kile kile cha fedha.

Kwa mtazamo wangu,miradi tunayoweza kuikamilisha ni ile ambayo haitegemei fedha zetu za ndani bali inategemea mikopo ya ndani na nje kwa asilimia mia moja(na sidhani kama tuna aina hiyo ya miradi ambayo serikali haichangi hata sent) na pia mikopo hiyo nayo iwe ni ya uhakika vinginevyo yatakuwa ni yale yale.

Kwa kukwepa aibu,tunaweza kulazimisha kwa kuelekeza fedha nyingi katika miradi hiyo tuliozindua kwa mbwembwe nyingi lakini tujiandae kwa matokeo ya maamuzi ya aina hiyo ikiwa ni pamoja na kudorora kwa sekta nyingine nyingi na kupungua kwa uwezo wa serikali kuhudumia wananchi wake.

Mfano hivi sasa wakati tunanua ndege karibu sita kwa mpigo lakuni angali jinsi wabunge wanavyolia na utekelezaji wa bajeti inayoishia mwezo June mwaka huu ambapo miradi mingi kama ile ya maji imekwama huku bajeti ya wizara hiyo ikipewa fedha kidogo sana kulinganisha na fedha zilizokuwa zimetengwa.

Sasa hapo kumbuka bado madeni ya kulipia ndege hizo bado hayajaisha huku tumeanza tena kujipanga kujenga reli ya kisasa,treni ya umeme, kujenga nyumba kama zile za Magomeni nchi nzima,mradi mkubwa wa kuvuta maji kutoka ziwa victoria kupeleka mkoa wa Tabora,n.k..

Ni kweli kabisa miradi hii ni muhimu na tunaihitaji lakini ni bora twende kwa awamu kwa kuangali ni nini vinapaswa kuwa vipaumbele vya kwa sasa kulikoni kuwa na miradi mingi ya mabilioni ambayo tunaweza kabisa tusikimalishe au tukaikamilisha kwa kuathiri vibaya sekta nyingine au kwa kuongeza kwa kiwango kikubwa deni la Taifa na hatimae tukajikuta tunafikia hatua tukawa hata hatukuposheki tena.

Tujipime uwezo wetu kwa kuangalia jinsi tulivyotekeleza Bajeti hii ya trilioni 29.5 bila kusahau mwenendo wa nchi wahisani na mashirika mengine ya kimataifa ya misaada katika kutimiza ahadi zao.

Tusipende figure kubwa kubwa wakati uchumi wetu ni wa figure ndogo tutaishia kuumbuka na kushindwa hata kutimiza vile vichache vilivyo ndani ya uwezo wetu kwa kutawanya fedha kiduchu tulizonazo katika maeneo mengi na matokeo yake huko kot
e zisitosheleze.
We Jamaa uwe unazungumza kwa haki si polojo na upotoshaji,wa makusudi unao fanya haikusaidi,
Mkuu aliomba msaada wa kuunganishiwa na huo umoja,ili akope,na jua kukopa ni sifa ya mtu makini na si umasikini kama
unavyotaka kutuaminisha.
Amini miradi hiyo sio luxualy yote ni vichochezi vya maendeleo.
Ndege mnabeza bule,hamjui kwamba ndege ikitumiwa vizuri,Inaweza leta pesa ya kununulia dawa,kuleta maji,kulipa mishahara etc.
kwangu mimi hiyo miradi yote imelenga kukamilishwa on time.ili itumike kuwahudumia wananchi vizuri.
Hapa kazi tu.
majungu wapelekee hao jamaa zako huko upande wa pili ndio watanunua.!!
 
Kwahiyo mnazindua miradi huku hamna pesa mmategemea kukopa?

Mna una hakika na hiyo mikopo?
 
Tuache tufanye kazi huu c mda wa siasa, tunachotaka wananchi maendeleo haijalishi njia ipi tutapita. Isije kuwa ndo mnaponda halafu ndo wa kwanza kubuk bombadia na kusoma siti za namba mkitafuta mapungufu
Ni maendeleo gani unayaongelea iwapo bajeti ya 2016/2017 haijatekelezwa hata 50% na tumebakiwa na mwezi mmoja tu kukamilisha mwaka wa fedha? Watanzania hatupingi maendeleo, tunachotaka ni realistic planning and budgeting! Sio kufurahisha genge
 
Bila shaka kijana utakuwa mchawi.
Una mawazo yako finyu sana,miradi isipokamilika watakaoumia ni watanzania ukiwemo wewe,jitahidi uwe na mawazo chanya.
 
Sitashangaa kina fulani wakaja na hoja ya kuhakiki kwanza baadhi ya miradi kwenye majimbo kumbe hela hawana.
 
Bila shaka kijana utakuwa mchawi.
Una mawazo yako finyu sana,miradi isipokamilika watakaoumia ni watanzania ukiwemo wewe,jitahidi uwe na mawazo chanya.
Kama hamjajipanga kwanini isikamilike?

Kama mnashauriwa na hamtaki kusikia mtamlaumu nani?
 
Kwahiyo mnazindua miradi huku hamna pesa mmategemea kukopa?

Mna una hakika na hiyo mikopo?
Kote uliko andika niliona akili inaanza kukurudi. Ila ulichoandika hapa afya yako ya akili imezorota kiasi kikubwa. Kuwa na uwezo wa kukopesheka nao ni mtaji. Kwamradi unaochukuwa muda mrefu kukamilika na kuanza uzalishaji kiuchumi si afya kuijenga kwa pesa taslimu. Pesa inayotafutwa ni ya vipande vitatu vilivyobaki kwani kutoka Dar-Moro pesa ipo Moro-Dom mkopo toka Uturuki.Pesa ya ndani inatumika kutoka Dar-Moro kwasababu baada ya miaka miwili na nusu uzalishaji utakuwa umeanza na kuingia katika kuchangia uchumi. Pia ndege imetumia pesa taslimu kwa sababu ndani ya miezi tisa imeanza uzalishaji na kuchangia kwenye uzalishji kwa faida.
 
Tangu mwanzo nilikuwa najiuliza hii miradi mikubwa ya mabilioni/matrilion tunayoizindua kila kukicha tutaikimilisha vipi ili hali uchumi wetu huu bado mdogo na hata bajeti yetu yenyewe bado ni tegemezi tu kwa kiasi kikubwa.

Mashaka yangu yaliongezeka zaidi siku ya jana baada ya kusikia tunaomba mkopo kutoka Afrika Kusini kwa ajili ya mradi wa kujenga reli ya kisasa.

Kwa kifupi huu ni ushahidi kuwa tunaingia kwenye miradi mikubwa na mingi kwa wakati mmoja kuliko uwezo tulionao huku tukiwa hatuna uhakika wa fedha za kukamilisha miradi husika kwa wakati.

Hakika hili ni tatizo tena kubwa na linaloweza kuja kutuumbua hapo baadae kwa kushindwa kukamilisha hii miradi kwa wakati na tunaweza kuja kujikuta tuna miradi iliyododa na kusimama kwa miaka mingi kama magofi.

Miradi hii ni kweli tunaihitaji lakini sidhani kama tulikaa chini na kupanga mikakati yetu kwa umakini ni jinsi gani tunaweza kuitekeleza kwa wakati na bila kuathiri sekta nyingine nyeti zinazotegemea chanzo kile kile cha fedha.

Kwa mtazamo wangu,miradi tunayoweza kuikamilisha ni ile ambayo haitegemei fedha zetu za ndani bali inategemea mikopo ya ndani na nje kwa asilimia mia moja(na sidhani kama tuna aina hiyo ya miradi ambayo serikali haichangi hata sent) na pia mikopo hiyo nayo iwe ni ya uhakika vinginevyo yatakuwa ni yale yale.

Kwa kukwepa aibu,tunaweza kulazimisha kwa kuelekeza fedha nyingi katika miradi hiyo tuliozindua kwa mbwembwe nyingi lakini tujiandae kwa matokeo ya maamuzi ya aina hiyo ikiwa ni pamoja na kudorora kwa sekta nyingine nyingi na kupungua kwa uwezo wa serikali kuhudumia wananchi wake.

Mfano hivi sasa wakati tunanua ndege karibu sita kwa mpigo lakuni angali jinsi wabunge wanavyolia na utekelezaji wa bajeti inayoishia mwezo June mwaka huu ambapo miradi mingi kama ile ya maji imekwama huku bajeti ya wizara hiyo ikipewa fedha kidogo sana kulinganisha na fedha zilizokuwa zimetengwa.

Sasa hapo kumbuka bado madeni ya kulipia ndege hizo bado hayajaisha huku tumeanza tena kujipanga kujenga reli ya kisasa,treni ya umeme, kujenga nyumba kama zile za Magomeni nchi nzima,mradi mkubwa wa kuvuta maji kutoka ziwa victoria kupeleka mkoa wa Tabora,n.k..

Ni kweli kabisa miradi hii ni muhimu na tunaihitaji lakini ni bora twende kwa awamu kwa kuangali ni nini vinapaswa kuwa vipaumbele vya kwa sasa kulikoni kuwa na miradi mingi ya mabilioni ambayo tunaweza kabisa tusikimalishe au tukaikamilisha kwa kuathiri vibaya sekta nyingine au kwa kuongeza kwa kiwango kikubwa deni la Taifa na hatimae tukajikuta tunafikia hatua tukawa hata hatukuposheki tena.

Tujipime uwezo wetu kwa kuangalia jinsi tulivyotekeleza Bajeti hii ya trilioni 29.5 bila kusahau mwenendo wa nchi wahisani na mashirika mengine ya kimataifa ya misaada katika kutimiza ahadi zao.

Tusipende figure kubwa kubwa wakati uchumi wetu ni wa figure ndogo tutaishia kuumbuka na kushindwa hata kutimiza vile vichache vilivyo ndani ya uwezo wetu kwa kutawanya fedha kiduchu tulizonazo katika maeneo mengi na matokeo yake huko kote zisitosheleze.
Wadau wameamua kukupuuza na POROJO zako. Jifanyie tathimini wewe mwenyewe.
 
Back
Top Bottom