Watazamaji wa Wimbo wa Belle 9 'Masogange'waongezeka Youtube

BRN

JF-Expert Member
Nov 18, 2013
4,229
5,258
Kwanza tupeane pole kwa Msiba wa ndugu yetu Agnes.
Kurudi kwenye mada nimepitia kwenye you tube channel na nimegundua watazamaji wengi sana wemeutazama huu wimbo il
i kumuona Agnes au Masogange kama alivyofahimika baada ya kushiriki kwenye wimbo wa video hii. Kabla ya hapo watazamaji wa huu wimbo na wachangiaji walikuwa wachache wasiofikia hata laki moja. Hivi niandikapo kuna watazamaji zaidi ya laki mbili na nusu na watoa maoni zaidi ya mia nne.
Mimi kabla ya msiba wa Agnes nilikuwa najiuliza hivi kuna manufaa yeyote Belle 9 anayapata kutoka kwa Masogange kama hati miliki ya jina la Masogange ambalo limempatia mtu umaarufu?!
Basi, itoshe tu kusema yaliyotokea yanahuzunisha.
Wasalamu.
 
Mimi leo pia ndo nimeutazama, kabla ya hapo sikuujua japo namfollow MasoG insta na twitter!
umeona..ndio nyie mnafanya wafuatiliaji wa huo wimbo wawe wengi..kule ndio alikuibukia ndio maana Belle kalia sana.
 
mm ndio mara ya kwanza kuutazama wimbo huo, video japo nmeangalia kwa kuirusha rusha ila nmemuona. hata wimbo nilikuwa siuelewi kumbe ndani kulikuwa na kiumbe adimu aisee. mbeya tuendelee kula maparachichi haloo!!
 
wakati huo ulitisha sema mambo ya youtube yalikuwa hayajashamiri.
 
wakati huo ulitisha sema mambo ya youtube yalikuwa hayajashamiri.
Ulitisha sana na nlimabiriaga bell9 kufika mbali sana nilikuwa sidhani kama diamond anaweZa fanikiwa kuliko bell 9 maana walitoka kipindi kimoja sema kumbe I was wrong
 
wakati huo ulitisha sema mambo ya youtube yalikuwa hayajashamiri.
si muda mrefu, ila nmemjua zaidi kwa kupitia sakata la dawa za kulevya ndpo picha zake nikawa nazitizama kwa uzuri. clip ya video ambayo niliangalia ni ile anapitapita sebureni alafu mwanaume anamwita kwa mbali Agiiiii!...nili concentrate kutazama umbile la nyuma na utembeaji wake maana ndio kulikuwa kunaniweka attention!!
 
  • Thanks
Reactions: BRN
Bell9! kati ya vijana wa bongo fleva ninaowaelewa sana sema ndiyo hivyo tena, dogo hana bahati. Wimbo wa Masogange, Amerudi nk kati ya vibao bora zaidi
 
Bell9! kati ya vijana wa bongo fleva ninaowaelewa sana sema ndiyo hivyo tena, dogo hana bahati. Wimbo wa Masogange, Amerudi nk kati ya vibao bora zaidi
Ni kweli mkuu yuko vizuri sana
 
Hapa ndio unakuja kugundua mziki ni zaidi ya kipaji nilishangaa 2010 diamond kuchukua tuzo 3 halafu belle 9 hakupata ila leo hilo gepu kati ya diamond na belle hata halisemeki
 
  • Thanks
Reactions: BRN
Back
Top Bottom