Watawala wetu wameshindwa hata hili?

Mkandara

Verified Member
Joined
Mar 3, 2006
Messages
15,472
Points
1,250

Mkandara

Verified Member
Joined Mar 3, 2006
15,472 1,250
Kibunango,
Baba acha kutuvika kamba za shingio mkuu huyu mtu anauliza pengine kama anaweza pata hotel maeneo ya usahilini..
Lini mzungu akajifunza Usafi wa mji kwa kuokota taka kwa mikono mitupu ambayo haina hata gloves?...tena basi hawa wenzetu wana nyenzo za kuokoteza hata vumbi, duh.
Mkuu wangu utanisamehe lakini nadhani propaganda za serikali hii zinatisha na sijawahi ona dunia nzima. Mfano mnalazimisha watu kujiunga na ujenzi wa shule tena huko wilayani kila nyumba ni lazima itoe mtu kisha serikali inatangaza kwa wananchi hao hao walojenga kuwa imeweza kujenga shule kadhaa ktk milaya kadhaa. Hapa unamwambia nani hasa kama mjenzi ni mwananchi mwenyewe?...
Hizi habari za usafi wa mazingira kuhudumiwa na wananchi wenyewe zinatoka wapi haswa? ndio Ujamaa Mambo leo ama, na wakati gani haswa hawa watu wanatakiwa kwenda kazini, huko walikoajiriwa!
Utanisamehe mkuu wangu lugha yangu siku zote huwa nzito nakuomba ipokee kama hoja.
 

Nyani Ngabu

Platinum Member
Joined
May 15, 2006
Messages
84,261
Points
2,000

Nyani Ngabu

Platinum Member
Joined May 15, 2006
84,261 2,000
Tatizo kubwa kwetu sisi ni kwa sababu hatufuati sheria. tungekuwa na serikali inayofuata sheria, basi swal ala usafi wa mazingira lingekuwa ni la kisheria na kila mtu angelazimika kufuata masharti ya usafi wa mazingira.


Huko Singapore, usafi wa mazingira ni la kisheria. Ukitupa kihsungi cha sigara barabarani, adhabu yake ni viboko 10 papo kwa papo. Ukitema chewin barabarani unapata bakora papo kwa papo. Ingawa adhabu hizi ni za kikatili, hiyo ndiyo ilivyo sheria yao na watu wote waniafuata.

Kwa hiyo usafi wa mazingira siyo swala la kujitolea ila ni wala la kisheria.
Hapa tutarudi kule kule...hatufuati sheria kwa vile ndivyo tulivyo~~~~
 

Kibunango

JF-Expert Member
Joined
Aug 29, 2006
Messages
7,744
Points
1,500

Kibunango

JF-Expert Member
Joined Aug 29, 2006
7,744 1,500
Mkandara:
Kuhusu hiyo picha, amini usiamini, hapo kuna wadau toka ulaya na afrika. Lengo lilikuwa ni kutembelea CBO na NGO zinazoshughulika na usafi wa mazingira. Katika picha hiyo wadau hao wanaangalia utendaji wa mojawapo ya CBO mjini Mwanza.

Aidha CBO zimetokana na kamati za maendeleo za mitaa ambazo awali zilikuwa zikifanya kazi kwa kujitolea zaidi. Ili shughuli zao ziwe endelevu, ndio zikazaliwa CBO. Kazi za kujitolea mara nyingi hufanyika katika siku za mapumziko.
Jiji la Mwanza kupitia CBO hizo limeweza kuwa Jiji safi kabisa kwa kushika nafasi ya kwanza mara mbili mfululizo.

Usishangae sana kuona watu hao wakifanya kazi bila ya kuwa na PPE(Personal protective equipment)! Wengi wao wanadai kuwa protective gloves na leg and foot protector zina joto sana, hivyo kuwafanya wasiweze kufanya kazi kwa ufanisi. Ukiingia kwenye Ofisi zao, PPE zote katika utunzaji wa mazingira wanazo, lakini hawazitumii.!


Shughuli za kujitolea Jijini Mwanza.
 

Forum statistics

Threads 1,382,685
Members 526,441
Posts 33,833,804
Top